Uchaguzi 2020 Manyara: Viongozi wanaofanya vikao vya usiku kuihujumu CCM wapewa onyo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Hanang mkoani Manyara kimewatahadharisha baadhi ya viongozi wa chama wanaofanya vikao usiku vya kukihujumu Chama hicho.

Kimeonya na kusema hakitasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa kufanya vikao vyao bila kuwa na vibali.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo, Ghaib Lingo, alitoa tahadhari hiyo kwenye mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha wagombea wateule wa ubunge na udiwani uliofanyika kwenye viwanja vya michezo vya Kijiji cha Endasak.

Alisisitiza kuwa kamati ya siasa katika uchunguzi uliofanywa na vyombo vya dola, umebaini kwamba kuna baadhi ya viongozi wa kata tano za wilaya ya Hanang wanaojihusisha na vikao vya usiku huku wakitambua kuwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi.

Lingo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, alisema baadhi ya viongozi hao baada ya majina ya wagombea wao kutoteuliwa na vikao vya juu, wameanza kukaa na wanachama kwenye maeneo yao na kuwashawishi kuinyima kura CCM na badala yake wapigie kambi ya upinzani.

“Nina kata tano ambazo viongozi wa chama wanafanya kazi hizo usiku, nilikuwa nafikiri siku nikiamka vibaya niwashike niwaweke ndani kwa sababu kufanya mikutano usiku bila kibali cha polisi ni kosa. Mimi nitashindwa kukutungia kesi wewe kwani hata leo tumepata kibali cha polisi ndiyo tunakutana hapa,” alisema.

Aliweka bayana kuwa baada ya wagombea wateule wa ubunge na udiwani kutambulishwa kwa wanachama na wananchi kwa ujumla, aliwaomba kuwachagua viongozi walioteuliwa na chama hicho ili waweze kuwaletea maendeleo endelevu.

Mkuu wa wilaya huyo alisisitiza kwamba ili wananchi wa Hanang wamlaumu mwakilishi wao wa ubunge kwamba ameshindwa kutekeleza ahadi za maendeleo, hawana budi kuhakikisha wanawachagua wagombea wateule wote waliopendekezwa na chama hicho.

Alisema ifikapo Oktoba 28, mwaka huu, wanachama wa chama hicho na wananchi wa Hanang kwa ujumla wahakikishe kura za kishindo zinakwenda kwa mgombea wa urais, wabunge na madiwani wa CCM kukamilisha mafiga matatu.

Akiwatambulisha wagombea wateule wa ubunge na udiwani wapatao 33, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Hanang, Mathew Dalema, alisema baada ya wagombea hao kuteuliwa na vikao vya juu vyenye mamlaka ya kufanya hivyo, kazi iliyobakia ni kuwanadi wapigakura ili kushinda kwa kishindo.
 
V
Vikao vya usiku viko kila kona ya nchi, .usiwasumbue huku Hanang
Alisisitiza kuwa kamati ya siasa katika uchunguzi uliofanywa na vyombo vya dola, umebaini kwamba kuna baadhi ya viongozi wa kata tano za wilaya ya Hanang wanaojihusisha na vikao vya usiku huku wakitambua kuwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi. CCM mnafurahisha Sana. Soma hii maneno
 
Mkuu wa Wilaya ya Hanang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo, Ghaib Lingo, alitoa tahadhari hiyo kwenye mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha wagombea wateule wa ubunge na udiwani uliofanyika kwenye viwanja vya michezo vya Kijiji cha Endasak.
Sasa hapo unaenda kuita kuna uchaguzi wakti Dc kesha chagua hivi tunaakili gani?
 
Kuhujumu wengine,sawa Ila mkihisi mnahujumiwa mnaunia. Kama no hivyo haki itendeke kwa wote kwani Tanzania no moja. Ila tutambue kuwa tuko huru kutofautiana kimtazamo, itikadi za kisiasa na kadhalika. Haki na Uhuru wa msingi vinavyo ainishwa kwenye Katina yetu ndio dawa. Vile vile tukatae Sheria za kuletwa kwa hati za dharura Mara nyingi Zina malengo ovu zakuwa Linda, watu ama maslahi ya makundi Fulani. Zaidi dawa Katina iliyopendekezwa na ikakataliwa na kikundi Fulani kwa kuhofia maslahi yao.
 
Upendeleo wa wazi kwa kiongozi wa serikali, atoaje haki kwa vyama vingine?
 
Back
Top Bottom