Manyara Stars(Boys) wamenifurahisha ila mashabiki.....kiboko...

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
23,914
23,079
Leo Vijana wametufurahisha sisi wapenda ushindi kwa timu zetu za Taifa, ikizingatiwa tumeitoa timu ya taifa ya vijana ya Cameroon...., Mashabiki leo ndio wameonyesha kuwa sasa hawataki kuonewa, wameonyesha ili pale mwamuzi wa kati alipoanza kutoa maamuzi yaliyoonekana kuikandamiza Manyara Stars. Mashabiki hao waliokuwa Jukwaa Kuu karibu na maofisa wa CAF, walianza kuwazonga maafisa hao konyesha kukerwa na maamuzi ya refa. Jambo hilo lilisaidia kwani refa alijirekebisha nadhani baada ya kujulishwa kuwa alichokuwa nafanya sio sahihi. Ila kilichonifanya niwaite mashabiki ni kiboko ni kuweza "kusogeza" Bendera ya Shabiki wa Cameroon(ilikuwa bendera ya taifa la Cameroon) iliyokuwa na ukubwa wa eneo karibu 60X120 sentimita bila yeye kujua. Shabiki huyo alikuwa makeke kweli kweli , alikuwa hataki kukukaa kwenye viti huku akiwaziba watazamaji wengine. jinsi "walivyosogeza" bendera yake hata sikuelewa. Shabiki huyo aliangaika kuitafuta kwa kuulizia walio kuwa karibu wala hakupata ushirikiano hivyo hakuipata bendera yake.

Binafsi kitendo cha "kusogeza "Bendera ya shabiki wa Taifa jingine, sio cha kiungwana, na kama mashabiki wa Cameroon wangekuwa wengi, kungetokea uvunjifu wa amani ya kuangalia mpira na watu kukosa burudani iliyowapeleka uwanjani. Nashauri, washabiki tunapoenda mpirani tusifanye vitendo vinavyoeweza kuhatarisha amani likiwamo ili la "kusogeza " bendera ya Timu pinzani. Kumbuka Bendera ya Taifa inagusa hisia za Uzalendo wa mtu. Ningekuwa mimi nimefanyiwa hivyo Cameroon pangechimbika!!
 
Ushindi tumepata lakini kwa timu ya vijeba, tukubali hilo..

Ungewaona hao Cameroon walivyojaza minjemba sijui ungesema nini? tatizo letu tumezidi kuwa waungwana ndo maana timu zetu za vijana hazifanyi vizuri.
 
ushindi wa magoli mangapi?

Baada ya kuwafunga 2-1 kama walivyotufunga wao Yaounde, zikapigwa dakika 120 then ushindi wa penalti 4-2 ndio uliotutoa kimasomaso na kuwabwaga nje ya mashindano wabishi wa Cameroun. Viva Ngorongoro
 
hivi hawa ndo serengeti boyz?
U23 ni Manyara Stars; U20 ni Ngorongoro Heroes; na U17 ni Serengeti Boys; Ya wakubwa bara Kilimanjaro Stars; Ya wakubwa Bara na Zenji Taifa Stars; Ya Wanawake Twiga Stars.............Na Timu yenye mafanikio anga za East Africa na kati ni Mnyama Simba wa Msimbazi Kariakoo...
 
Back
Top Bottom