Manyara: Rushwa ya elfu 20 yawaponza Mwenyekiti na Katibu wa Baraza la ardhi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi kata ya Bwawani wilayani Kiteto Stevin Thadayo Tollya pamoja na Katibu wake Maiko Robert Lemabi wamekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kuomba rushwa kiasi cha Shilingi elfu ishirini (20,000).

Taarifa ya Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara imesema wawili hao walikamatwa kwa nyakati tofauti baada ya kuomba rushwa ya Tshs 20,000 kutoka kwa mwananchi mmoja aliyetaka kufungua Shauri la Ardhi katika Baraza la Ardhi kata ya Bwawani.

Mwananchi huyo alitoa taarifa katika ofisi za TAKUKURU wilayani Kiteto tarehe 24-07-2019 ambapo mtego uliandaliwa na hivyo baada ya kutumiwa kiasi hicho (cha rushwa) ambacho walikipokea, watuhumiwa hao wakakubali kufungua shauri husika.

Wawili hao walikamatwa kwa nyakati tofauti na kufikishwa ofisi za TAKUKURU kwa mahojiano na hatimaye kupatiwa dhamana, huku wakisubiri kufikishwa mahakamani wakati taratibu za kisheria zitakapo kamilika.

IMG-20190904-WA0030.jpeg
 
Back
Top Bottom