Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Mnafanya umoja kimagroup sasa , au kimtaa, mpak inafikia hatua ya chama kinarun mkoa mzima na mnaitisha kikao cha mkoa , si hatar hyo...alaf manyara sio far from Kilimanjaro , ni useles kutengeneza chama cha namna hiyo tena Kwa ukubwa huo , angalau ingekuwa Songea au katavi huko hapo inaweza ikamake sense , japo bado ni very dangerous
Hahahaa....roho mbaya Tu we si useme kabila lako ushirikiano sifuri!!hahahaaaaa
 
Hapo Mkuu wa Mkoa wa Manyara, yuko sahihi. Hawa watu wa mkoa huo tajwa wana ubinafsi sana.
Na bado mtazidi kubaki maskini kwa akili hizi mfu, kilimanjaro inazidi kupaa tu kimaendeleo
Ona vijiji vya kilimanjaro utadhani upo uholanzi
FB_IMG_15755750529514181.jpeg
 
Ila wakati mwingine hawashiriki misiba ya wengine, wakitegemea uvyama wao.
Wanakuwa wabinafsi. Madhara yake kupeana fursa hasa pale mtu wa kabila husika anapokuwa nafasi ya juu, kupuuzia shughuli za watu wa kabila wengine sababu ye anajua ana backup ya kabila lao, kabila likiwa na watu wengi mwishowe wanatengeneza himaya yao. Wataanza kuwa na benki yao ya kukopeshana, watatafuta eneo ambalo watajenga wao tu.
Ni vitu vidogo ukivichukulia kawaida ila vina madhara mbeleni.
 
Hili ni suala la miongozo na sera tu; kwa mfano unaweza ukasema wananchi wa "Kilimanjaro" au chama cha "Wachagga". Siyo wananchi wote wa Kilimanjaro ni Wachagga. Upande wa pili ni kuwa lengo kubwa ni nini? Sasa hapa kunahitajika mwongozo na utaratibu wa jinsi gani vyama hivi vinaweza kuwepo bila kuonekana vya kikabila.Mfano uliotolewa hapo juu una ukweli; kama kwenye eneo fulani watu wa kabila fulani ni wachache zaidi je wanaweza kushikirikiana na watu wa makabila mengine?

Hapa Marekani tumeona madhara haya mahali fulani. Kuna vyama vya makabila ya Wanigeria (Ibo, Yoruba n.k). Na wao wako ndani sana kwenye hili la ukabila. Ikatokea kuna Mnigeria fulani alikufa toka mojawapo ya makabila madogo kabisa.. mbona ilikuwa kasheshe katika kuandaa mazishi. Sijui walitatuaje. Lakini tuna vyama vya Watanzania na vinashirikiana na vinahusisha Watanzania wa makabila yote na hatuulizani "we kabila gani".

Ni bora kuwa na vyama kushirikiana visivyo na sura ya kabila (nadhani sura ya mahali fulani inaweza kuhalalishwa). Ukisema "Watu kutoka Tanga" au "Watu kutoka Tabora" na katika seti hiyo ukajikuta unahusisha watu wengi sana kuliko ukiwa na seti iliyoandikwa "Kabila fulani".

Inahitajika kujadilika na watu kutoa mawazo ya kuona kama kuna ulazima wa kuwa na vyama vya aina hii na kama viwepo basi viongozwe kwa taratibu gani. Kufuta bila kujadiliana au kutoa nafasi kwa mawazo mbadala kutolewa ni kuwa na uhodhi wa fikra.
 
chezea Wachaga ila mtapata majibu. Tumefika patamu Wachaga waandamane kupinga ubaguz wa wazi wazi dhidi ya uwepo wetu maana tunapoelekea watatutoa roho kama Hitlar kwa Israel
Mlipokuwa mkijenga Mitandao ya kikabila hamku project mbeleni kuwa litakuja fumuka ? Yaani Tanzania Ina makabila 120 mkajiona wote 119 wajinga kasoro ninyi tu? Kuwa hayo makabila yote 119 hawajui umuhimu wa mitandoa ya kikabila kwa ajili ya kujipendelea kwenye ajira,vyeo,fursa ,tenda nk ? Hamkuliona Hilo kuwa mbeleni litawaletea shida?
 
Tukiwa tunaishi pekee katika eneo fulani (kama dunia) ni ngumu kujua ujinga au uerevu wetu lakini kwenye dunia tunayoshare na wengine hata kupitia teknolojia ni rahisi kujua ujinga wetu ulipo.
Naona uelewa mdogo unatusukuma kwenda tulikokukataa na tusikokutaka, werevu wanaomba tusifike huko.
 
Mwaka 2007, Prof. Rwekaza Simpho Mukandala, alifuta vyama kama hivi UDSM. Miongoni mwa vyama hivyo ni KAGERA UNIVERSITY STUDENTS ASSOCIATION (KAUSA) kilikuwa kikubwa mno nami nilikuwa kiongozi.
Kulikuwaga na SOUTHERN SQUARE pale UDSM
 
Back
Top Bottom