MANYARA : RC Mnyeti amshukia kama mwewe Mbunge (CCM)

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amemshukia mbunge wa Babati Vijijini (CCM), Vrajlal Jituson kuwa atamchukulia hatua kali endapo ataendelea kuchochea migogoro ya ardhi kwenye eneo hilo.

Mnyeti aliyasema hayo juzi kwenye kijiji cha Maweni wakati akiagiza ng’ombe waliokuwa wakishikiliwa na Serikali ya kijiji hicho kuachiwa kwa kuingia katika jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori Burunge na kurudishiwa wafugaji.

Alisema amepata taarifa kwamba mbunge huyo anachochea wafugaji kuingia kwenye maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya kujinufaisha na kura za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Alimuonya mbunge huyo kuwa akiendelea kuchochea wafugaji wachungie mifugo hifadhini, atamuonyesha kuwa yeye ndiye mkuu wa mkoa wa Manyara.

“Nataka nikwambie mbunge kwamba nakuheshimu sana, sitaki uendelee kuchochea migogoro, na mimi mtu akivunja sheria simkamati aliyevunja, namkamata aliyemtuma kuvunja, sitaki mtu aje kunipapasa sharubu,” alisema.

“Anakuja mwanasiasa kwa njaa ya kura za mwakani anadanganya watu halafu wakipigana na kuuana anakimbilia Dodoma hilo sitalikubali litokee Manyara,” alisema Mnyeti.

Hata hivyo, Jituson alikanusha madai hayo ya uchochezi na kueleza kuwa hakuwahi kufanya hivyo.
Alisema migogoro ya ardhi katika jimbo la Babati Vijijini ilikuwapo miaka mingi hata kabla hajawa mbunge na eneo hilo lina mgogoro wa zaidi ya miaka 10.

Mwenyekiti wa chama cha wafugaji nchini, George Bajuta alipongeza hatua hiyo ya Mnyeti ya kuagiza ng’ombe 774 wa wafugaji kuachiwa.

Bajuta alisema mkuu huyo wa mkoa amefanya jambo jema kwani eneo hilo lina mgogoro wa muda mrefu.

Alisema eneo hilo halina chanzo kingine cha maji zaidi ya ziwani ambapo inabidi mifugo ipite kwa mwekezaji na maeneo ya wafugaji na hifadhi yapo karibu hivyo mifugo ikipelekwa kunywa maji inapita kwenye hifadhi na kushauri jambo hilo liangaliwe vizuri ili kusitokee mgongano na kusababisha vurugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amemshukia mbunge wa Babati Vijijini (CCM), Vrajlal Jituson kuwa atamchukulia hatua kali endapo ataendelea kuchochea migogoro ya ardhi kwenye eneo hilo.

Mnyeti aliyasema hayo juzi kwenye kijiji cha Maweni wakati akiagiza ng’ombe waliokuwa wakishikiliwa na Serikali ya kijiji hicho kuachiwa kwa kuingia katika jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori Burunge na kurudishiwa wafugaji.

Alisema amepata taarifa kwamba mbunge huyo anachochea wafugaji kuingia kwenye maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya kujinufaisha na kura za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Alimuonya mbunge huyo kuwa akiendelea kuchochea wafugaji wachungie mifugo hifadhini, atamuonyesha kuwa yeye ndiye mkuu wa mkoa wa Manyara

Back
Top Bottom