Manyara: Naibu Waziri Pauline Gekul atuhumiwa kuchochea migogoro ya ardhi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,323
7,963
RC Makongoro Nyerere ametoa tuhuma hizo dhidi ya Gekul na kumtaja pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji, Babati, Abdulrahaman Kololi kwa kuwatuma wananchi kuvamia shamba la mwekezaji

Amemwagiza RPC George Katabazi kuwakamata waliovamia shamba wahojiwe hadi wawataje wanaowatuma, na kudai kuwa Mbunge na Diwani wanahusika na mgogoro huo

Gekul ambaye ni Naibu Waziri amekana shutuma hizo na kusema anashangazwa kwa kuwa yeye amekuwa mpatanishi wa tatizo hilo na sio kuchochea migogoro ya ardhi.

===============

Mkuu wa Mkoa wa Manyara (RC), Makongoro Nyerere amewatuhumu Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Abdulrahaman Kololi kwa kuchochea migogoro ya ardhi kwenye shamba la Dudumera la Kata ya Maisaka.

Gekul ambaye ni mbunge wa Babati mjini na Kololi ambaye ni Diwani wa kata ya Maisaka wanatuhumiwa na Makongoro kuwachochea wananchii ili wavamie shamba la Dudumera ambalo ni la mwekezaji.

Makongoro akizungumza mjini Babati kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo (RCC) leo Jumatano, Novemba 30, 2022 amesema Gekul na Kololi wanawachochea wananchi ili wavamie shamba la mwekezaji na kusababisha vurugu.

Amemwagiza kamanda wa polisi mkoa huo, George Katabazi kuwakamata vijana wanaovamia eneo hilo na kutumia mbinu za kipolisi kuwahoji ili wawataje watu wanaowatuma.

"RPC mkawakamate hao vijana kwani mbunge anahusika na diwani anahusika kuchochea mgogoro ni bora akose hiyo nafasi ili uchaguzi ufanyike na tupate Mwenyekiti mpya wa halmashauri ya mji," amesema Makongoro.

Amesema hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan alifanya ziara ya kutembelea mji wa Babati na kutoa onyo kwa viongozi kutochochea migogoro ya ardhi ila anashangazwa na viongozi hao kufanya hayo.

Hata hivyo, Kololi amesema yeye hawezi kuzungumzia chochote juu ya shutuma hizo huku Gekul akisema anashangazwa na shutuma hizo kwani yeye amekuwa mpatanishi wa tatizo hilo na siyo kuchochea migogoro ya ardhi.

"Juzi kulitaka kuzuka vurugu pale juu ya mgogoro huo, nilifika na polisi tukawapooza wananchi, leo inakuwaje nasingiziwa kuanziaha mgogoro huo," amehoji Gekul.

Amesema wananchi hao hawajavamia eneo hilo kwani walikuwepo zaidi ya miaka 70 iliyopita hivyo hawapaswi kuondolewa hivi sasa labda wapewe sehemu nyingine ya kufidiwa.

MWANANCHI
 
Kwahiyo Makongoro anawaogopa mpaka awafanye vijana chambo
 
Pauline Gekul Nilishangaa alipataje Unaibu Waziri.
Kichwani hayuko sawa, Makongoro yuko sawa 100% kumtaja.
Ni mbunge mwenye njaa kali sana
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom