Manyara: Mzee wa miaka 58 abaka watoto watatu akiwemo mwanaye wa kumzaa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,300
5,434
Jeshi la Polisi Mkoani Manyara limethibitisha mwanaume mmoja ajulikanae kwa jina la Simon Zakalia (58) kushikiliwa kwa tuhuma za ubakaji wa watoto watatu Wilayani Hanang mkoani humo akiwemo binti yake.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, Limited Mhongole amesema mtuhumiwa huyo alitenda ukatili huo mwaka 2021 na 2022, mbapo tukio la kwanza anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi akiwa shambani.

“Juni 2021 katika Kijiji cha Masakita, msichana mwenye umri wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Masakita aligundulika amebakwa na mtuhumiwa, baada ya kumvizia wakati akitoka shambani.

“Kumbukumbu zinaonyesha alimlaghai kwamba atampa shilingi mia tano ili asitoe taarifa nyumbani kwao.

"Mtuhumiwa anatuhumiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 13, mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Masakita, alimpeleka shambani na kumfanyia tendo hilo. Hiyo ilikuwa mara ya pili kumbaka mhanga huyo anayeishi na bibi yake.

“Pia Machi, 2022 mtuhumiwa alimbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 12 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba, alimlazimisha kufanya kitendo hicho shambani huku akimtishia kuwa atamuua akitoa siri kwa bibi yake, kwani mhanga anaishi na bibi yake.

"Mtuhumiwa huyo tayari amekamatwa na yupo mahabusu.

"Chanzo cha kugundulika matukio haya ni mtuhumiwa kumfuata binti yake na kumtaka wafanye mapenzi ndani ya nyumba ya bibi yake, binti akamwambia atangulie shambani anamfuta, baada ya mtuhumiwa kuondoka ndipo binti akatoa taarifa kwa jirani.

"Jirani akamfikishia bibi yake, bibi naye akatoa taarifa shuleni, kikafanyika kikao, binti akawataja wahanga wenzake wawili. Uchunguzi unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa pindi Mahakamani uchunguzi ukikamilika,” - Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, Limited Mhongole.

Mhongole ameongeza kuwa ni vema jamii ikatazama suala hilo kwa umakini, kwani uchunguzi unaonyesha kuwa kuna watoto wanaoishi na bibi zao wanafanyiwa udhalilishaji kwa kuwa walezi wao wanakuwa hawana muda wa kuwaangalia muda mwingi.

Ameshauri wazazi kuwa makini na kuzingatia malezi ya watoto.



Source: Huheso-foundationorg
 
Nyege mbaya sana jamani mhhhhhhhh mzee wa miaka 50 upo active. HUNA mwanamke anaeeleweka puchu. Mikono imekuwa migumuuuu mhhhhh kubaka tuuu hata nahis huyu kasha tia mpaka mbuzi au wanyama the same like.....
 
Nyegez mbaya sana
IMG-20220414-WA0002.jpg
IMG-20220414-WA0003.jpg
 

Attachments

  • IMG-20220414-WA0003.jpg
    IMG-20220414-WA0003.jpg
    90.2 KB · Views: 16
  • IMG-20220414-WA0003.jpg
    IMG-20220414-WA0003.jpg
    90.2 KB · Views: 21
Back
Top Bottom