Manyara: Mwenyekiti wa Kijiji ashikiliwa na TAKUKURU kwa tuhuma za rushwa ya ngono

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
8D820F46-49F9-4248-BB43-6E27DDE25C22.jpeg

A2B7917B-0B37-41FC-8953-BBA9C9D3EA5A.jpeg
 
Wako wengi tuu..

Tembelea tovuti ya Pccb utaona hizo taarifa.

Zimewekwa kwa kil kanda.
 
Isijekuwa walichelewa kidogo wakakuta kicheche mzee amekwisha zama. Waseme ukweli kama walichelewa kidogo wakakuta tayari...
 
Hivi kuhusu ile habari ya TAKUKURU KUIACHIA CCM WATUHUMIWA WA RUSHWA KURA ZA MAONI,imeishia wapi??.Nauliza tu.
 
Nimefikiria kwa sauti jinsi mhemko wa kingono unavyokuwa umemtawala mtu kipindi anaelekea kupokea hiyo rushwa!

Huyo mzee nadhani aliteswa sana na hako kasichana pamoja na mazingira ya maandalizi ya kupokea huo 'mgao' wa rushwa.

Inawezekanje kuvaa condom kabla halafu ukawa mbali na hadi vurumai la kukamatwa, kitu kikawa bado kinasoma tu hakishuki!

Inamaana pale alichezeshwa mchezo na hako kabinti, kwamba avae kwanza condom kahakikishe, halafu mlango ndiyo ukapigwa teke au ilikuwaje!

Dah! Mzee kakutwa na balaa uchi wa mnyama huku akichuruzika na udenda wa ashiki, kavishwa puto kimasihara na mzigo hajapewa, hili fumanizi lilipangwa na watu wenye akili kubwa!

Tuseme hako kabinti ni kajanja sana'eegh?

Ivi baada ya sekeseke hili kupita, watakuwa wanaangalianaje!

Nimejaribu kujenga picha ya tukio, nimeshindwa kuelewa vurugu la fumanizi la dakika2 lilivyochukua sura humo chumbani!

Jinsi mzee alivyokutwa na vijana wadogo wa ofisi makamo ya wajukuu zake akiwa kapandisha mihemko ya kupokea rushwa!

Ninadhani ni afadhali ya kukamatwa na rushwa ya pesa, mtu anakuwa kavaa nguo zake, lakini hii ya kukamatwa ukiwa uchi umevalishwa na kielelezo kabisa huku rushwa yenyewe haujaipokea, ninadhani tukio la kudhalilisha zaidi ya kukamatwa, maana haijawahi kutokea.
 
TAKUKURU wangefanya kazi ya namna hii kwenye kura za maoni ya vyama mbalimbali vya siasa wangekua wameisaidia sana nchi. Kule kwenye hizo kura kuna rushwa za kila aina kuanzia za pesa, madaraka na rushwa za ngono

Rushwa kwenye siasa ni mbaya zaidi kwa sababu athari zake zinasambaa kwenye eneo kubwa na madhara yake kwa taifa hayapimiki

Wakati tukiwapongeza TAKUKURU kwa kutoa taarifa hii ya Mwenyekiti wa Kijiji ambayo jinsi ilivyo imeshamdhalilisha huyo mtuhumiwa wa rushwa ya ngono, tuwaombe pia wasiwe na kigugumizi cha kuchukua hatua kama hizi za kuwadhalilisha watuhumiwa wa rushwa kwenye siasa hasa wale wa kura za maoni badala ya kukimbia jukumu lao la kisheria na kudai eti kuviachia vyama vyenyewe vichukue hatua!!
 
Back
Top Bottom