Manyara: Mwenyekiti na Katibu wa CCM Mbaroni kwa Rushwa

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Manyara inawashikilia mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi tawi la Maisaka Katoi tawi la Babati Bakari Katibu na Katibu wa Tawi hilo Juma Swalehe kwa makossa ya kuomba na rushwa ya Shilingi laki mbili(200,000). Kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya 2007.

Wawili hao waliomba Rushwa toka kwa Mwinjilisti wa Kanisa la Kilutheri la Komoto kwa maelezo kuwa baada ya kupokea fedha hizo wangemuachia kiwanja walichodai kuwa ni mali ya CCM.

Uchunguzi zaidi kuhusana na uhalali wa CCM kumiliki kiwanja hicho na mamlaka ya viongozi hao kuhusiana na mali za chama unaendelea na mara utakapokamilika hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

photo_2020-06-25_12-53-09.jpg
 
Back
Top Bottom