Manyara: Mtu mmoja amefariki katika ajali ya basi la Mtei na gari dogo

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Basi la Kampuni ya Mtei lililokuwa likitoka Babati kuelekea jijini Dar es Salaam limegongana na basi dogo katika eneo la Himiti mjini Babati

Inadaiwa kuwa Mwanafunzi wa Shule ya msingi Silver ya mjini Babati ndiye aliyefarika katika ajali hiyo
=====

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Silver mjini Babati mkoani Manyara, amefariki dunia baada ya kutokea ajali kati ya basi la Kampuni ya Mtei kugongana na basi dogo aina ya Hiace.

Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara, Augostino Senga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo asubuhi ya leo Mei 15, 2019 katika eneo la Himiti mjini Babati na kumtaja mwanafunzi aliyefariki kuwa ni Osiligi Paul mwenye umri wa miaka mitatu na miezi mitano.

Kamanda Senga amesema ajali hiyo imehusisha basi la Scania Kampuni ya Mtei na basi dogo aina ya Hiace.

Amesema mwalimu wa Shule ya Silver ambayo zamani ilikua ikiitwa Deborah, Francis Mollel (36) amejeruhiwa kwenye ajali hiyo pamoja na mwanafunzi Lightness Emmanuel (6) na wakala wa Mtei Paul Shilala (28) wamepata majeraha na wapo Hospitali ya Mrara mjini Babati.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi la Mtei kuipita gari nyingine bila tahadhari na kugongana na basi dogo kwenye barabara hiyo ya Babati-Kondoa.

"Dereva wa basi dogo, Daniel Godfrey (25) naye alijeruhiwa miguuni yupo Hospitali ya Mrara akipatiwa matibabu ila dereva wa basi la Mtei alikimbia na tunamtafuta, amesababisha ajali kwa uzembe wake,’’ amesema Kamanda Senga.


1557907555142.jpeg


1557907504014.jpeg
 
Pole wafiwa
  • Dereva wa bus amesomea ana cheti na daraja lake la leseni ni la juu kabisa
  • Kadhalika dereva wa bus dogo
  • Inaonekana dereva wa bus kubwa amehama site kwenda upande usio wake
  • Je vyeti vinaepusha ajali?
 
Pole wafiwa
  • Dereva wa bus amesomea ana cheti na daraja lake la leseni ni la juu kabisa
  • Kadhalika dereva wa bus dogo
  • Inaonekana dereva wa bus kubwa amehama site kwenda upande usio wake
  • Je vyeti vinaepusha ajali?
Vyeti haviepushi ajali bali madereva ndiyo wanaepusha ajali kwa kuzingatia mafunzo waliyopata mpaka wakapewa vile vyeti. Huyo dereva wa basi la Mtei inatakiwa apigwe mvua ya miaka mingi gerezeni ili madereva wenye akili ndogo kama yeye wasifanye ujinga huo. Umefika wakati wa hukumu za ajali zinazosababishwa na uzembe wa madereva kuwa miaka 30 mpaka maisha kama wabakaji wanavyofungwa. Dereva anayeua kwa uzembe kama huyo ni zaidi ya mtu aliyebaka!
 
Inauma sana ajali kutokea katika barabara nyeupe kama hiyo. Watu wengine hasa madereva ni kama mashetani au mavampire hawatulii mpaka waueue
 
Sawa kiongozi?Nilidhani na wewe ni moingoni mwa wana jamvi wanaokurupuka kuandika kabla ya kufikiri.

OK.Kama amejazia na umeliona hilo samehe kwa kukuuliza hivi" una akili sawa sawa kweli wewe?"Wakati kumbe una masalaa kibao.

Hahahahaha!!!
Kwema mkuu, amejazia nyama.Wakati nauliza hapakua na taarifa yoyote ya ziada ukiachana na kifo cha huyo mtoto.
 
Weupe wa barabara unadanganya.Ni sawa na wanawake/wanaume weupe wanavyodanganya midume/mijike kujikoki (sijasema waaojichubua/wanao scrub).

Barabara giza/kona kona madereva wana kuwa makini, ajali hazitokei.Ni sawa na wanawake/wanaume weusi walivyo makini.

Maeneo yangu hayo back 46 years,Himiti,Gendii,Maweni,Nakwa ya mashariki/magharibi,Angoni,Sigino,Magugu,Magara,Mlima Logia,Dareda,Kidasii,Nangwa,Masakta,Endasaki,halafu Galapo,Mwamire nk.

Kudadadeki walahi,Desiii akhamisaa,ghwalang'u!!!!

Sheria za barabarani zilianza kuzingatiwa,ajali zilipungua sana.Inabidi madereva wakaziwe ili wasisababishe ajali.

Kipindi sasa Polisi wa barabarani wamekuwa wakali ingawa na mimi mara kadhaa rungu limenishukia vibaya sana kwa kuzembea barabarani.

Hahahahaha.

Inauma sana ajali kutokea katika barabara nyeupe kama hiyo. Watu wengine hasa madereva ni kama mashetani au mavampire hawatulii mpaka waueue
 
Vyeti haviepushi ajali bali madereva ndiyo wanaepusha ajali kwa kuzingatia mafunzo waliyopata mpaka wakapewa vile vyeti. Huyo dereva wa basi la Mtei inatakiwa apigwe mvua ya miaka mingi gerezeni ili madereva wenye akili ndogo kama yeye wasifanye ujinga huo. Umefika wakati wa hukumu za ajali zinazosababishwa na uzembe wa madereva kuwa miaka 30 mpaka maisha kama wabakaji wanavyofungwa. Dereva anayeua kwa uzembe kama huyo ni zaidi ya mtu aliyebaka!
Na Dereva akiwa ni miongoni mwa waliopoteza maisha kwenye ajali atafungwa nnani??
 
Kama dereva aliyefanya uzembe akifariki basi hakuna wa kumfunga. Inakuwa kama jambazi aliyefia kwenye tukio!
Mimi nafikiri Askari waliojazana narabarani wajenge mazingira rafiki kwa madereva badala ya kuwajaza hofu pamoja na hasira kwa kuwabambikizia makosa. Hii itawapunguzia stress madereva wawapo barabarani. Mf wa makosa ya ubambikiziaji na pale askari anapojificha vichakani kwenye maeneo ya kuendesha speed 80 kwa saa kwa magari ya abiria, kisha dereva akaenda kukitana na askari wengine baada ya km 6 na kuambia umepigwa torch huko utokako kwenye eneo la speed 50 kwa saa. Hapo dereva lazima awe na hasira kwani hakuna sehemu aliovunja sheria. Na hata dereva akimkatalia basi hutoa picha na speed ya gari lake. Kumbuka kwamba askari aliyepiga torch dareva hakumuona kwani alijificha eneo ambalo si la 50 kwa saa.
 
Back
Top Bottom