Manyara, Maisaka: Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Bakari Khatibu Yangu ahukumiwa

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
634
1,000
Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya hakimu mkazi Manyara Mh. Simon Kobero mnamo tarehe 27/ 05/2021 amemhukumu kwenda jela kutumikia kifugo cha miaka 2 au kulipa faini ya sh. 300,000/= mwenyekiti wa tawi la Maisaka kati Wilayani Babati mkoani Manyara Bw, Bakari Khatibu Yangu.

Bakari amehukumiwa baada ya kukiri makosa ya kuomba na kupokea rushwa ya sh. laki mbili toka kwa Mwinjilisti wa kanisa la KKKT, kinyume cha sheria namba 15 ya makosa ya kuzuia na kupambana na Rushwa.
1622190759816.png
 

Attachments

  • File size
    181.5 KB
    Views
    4

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,506
2,000
Huu ndiyo utaratibu wa TAKUKURU siku hizi siyo wa kutoa taarifa ya matokeo ya kesi zilizotolewa maamuzi/hukumu mahakamani?

Kama ndivyo, hii inamaanisha nini kutoka TAKUKURU mkoa wa Manyara? Je, ni kwa sababu aliyehukumiwa ni mwenyekiti wa CCM na kwa hiyo wanataka attention ya wananchi ya kwamba, wafikiri na kusema...;

"...ala, kumbe na wale wa CCM huwa wanashitakiwaga na kuhukumiwa kwenda jela...!!??

I personally don't get the logic of this...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom