Manyara: Baba mbaroni kwa kuwabaka binti zake watatu

Polisi wanamshikilia baba mwenye miaka 57 mkazi wa Kijiji cha Ndaleta mkoani Manyara kwa tuhuma za kuwabaka binti zake watatu wenye miaka 15, 17 na 18. Wizara ya Maendeleo ya Jamii imesema watoto hao tayari wamepatiwa matibabu na wanaendelea kupatiwa msaada wa kisaikolojia.

---
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 57, mkoani Manyara Kaskazini mwa Tanzania anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania kwa tuhuma za kuwabaka watoto wake watatu wa kike alhamisi ya juma lililopita.

Akitoa taarifa jijini Dodoma mapema leo, Mkuu wa Mawasiliano katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Prudence Constantine amesema kuwa baba huyo anadaiwa kuwafanyia tendo hilo la kikatili mabinti zake hao wenye umri wa miaka 15, 17 na 18 katika Kijiji cha Ndaleta, wilaya ya Kiteto.

Constantine alisema kuwa wizara imesikitishwa na taarifa za tukio hilo na inapenda kutoa taarifa kuwa tayari mtuhumiwa yupo mikononi mwa polisi kwa taratibu zaidi za kisheria.

Aidha, amesema kuwa watoto wameshapatiwa huduma za kiafya na wanaendelea kupatiwa huduma za msaada wa kisaikolojia na kijamii.

Mkuu huyo alisema kuwa hivi karibuni kwenye jamii kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukatili kwenye makundi yote ya jamii ikiwemo watoto.

Hivyo alisema kuwa Wizara inawaomba wananchi kuungana kupinga ukatili wa makundi yote kwa ujumla wake na kutoa taarifa mapema kwenye vyombo vya serikali na vyombo vya kijamii vinavyoweza kutoa msaada wa haraka pale tukio linapotokea.

Chanzo: BBC
Huyo mzee nae hakuona wanawake mpaka awabake watoto wake wa kuzaa ilihali sikuizi hata wa buku buku wapo.
 
Back
Top Bottom