Manunuzi ya Joseph Mbilinyi Sugu kwenye Soko la Igawilo huko Mbeya Mjini yaleta mtikisiko mkubwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,489
215,328
Leo hii huko Mbeya Mjini kulikuwa na ziara ya manunuzi ya nyanya na mishikaki iliyofanywa na Mbunge wa zamani wa Jimbo hilo bilionea Joseph Mbilinyi ambaye pia anafahamika kama Sugu au Real Jongwe kama anavyofahamika siku hizi, ama waweza kumtambua kama mfungwa wa kisiasa.

Kama masihara tu akaibuka kwenye Soko la Igawilo ambako alienda kununua nyanya na vitunguu, yaani viungo mbalimbali zikiwemo karoti na pilipili hoho kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwake, baadaye wadau wakampeleka hadi eneo la kuchomea mishikaki, ili waitafune kidogo.

Basi bwana kufumba na kufumbua akajikuta amezungukwa na umati ambao haufahamiki ulikotokea! Hakika huyu jamaa anapendwa Mbeya Mjini! Kwa kifupi ni kwamba shughuli za soko ni kama zilisitishwa kwa muda kupisha Sugu anunue nyanya! Yaani ilifika wakati tukahofia kwamba huenda polisi wangevurumisha mabomu ya machozi, maana umati wake unazidi ule wa mechi ya Yanga dhidi Al Hilal ya Sudan kwa Mkapa.

Kwenye Hili nimejifunza jambo moja kubwa sana, kwamba usishindane na aliyejaaliwa, utadhalilika sana. Wazaramo wana msemo mmoja kwamba, "Acholile kachora".

Wewe ulitarajia nini kama Bilionea kaingia kwenye Nyama Choma katika kipindi hiki cha njaa ya kipato na chakula kwa kila mtanzania kwa sasa??

Si walikuja wakijua anaweza kuwanunulia Mishikaki woote waliokuwepo hapo?

Lakini je!
Bilionea huyu aliweza?
Au aliishia blah blahtu?

Lakini iweje wamfuate kwenye mushikaki tu,lakini kwake au ofisini kwake wasiende?
wakati wanapajua na wanampenda??

Matukio Mengine ni ya kupanga tena ya kizamani kidogo.

Huyu ana Test Mitambo,baada ya kusikia mikutano Ruksa very soon!

Haya bwana mleta mada,tupe mrejesho?
 
Ni hivi , Mishikaki yote ilifagiliwa yaani !!
 
Leo hii huko Mbeya Mjini kulikuwa na ziara ya manunuzi ya Nyanya na Mishikaki , iliyofanywa na Mbunge wa zamani wa Jimbo hilo , Bilionea Joseph Mbilinyi , ambaye pia anafahamika kama Sugu au RealJongwe kama anavyofahamika siku hizi ama waweza kumtambua kama Mfungwa wa kisiasa .

Kama masihara tu akaibuka kwenye soko la Igawilo , ambako alienda kununua nyanya na vitunguu , yaani viungo mbalimbali zikiwemo karoti na pilipili hoho kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwake , na baadaye wadau wakampeleka hadi eneo la kuchomea mishikaki , ili waitafune kidogo .

Basi bhana kufumba na kufumbua akajikuta amezungukwa na umati ambao haufahamiki ulikotokea ! Hakika huyu jamaa anapendwa Mbeya Mjini ! kwa kifupi ni kwamba Shughuli za soko ni kama zilisitishwa kwa muda kupisha Sugu anunue nyanya yaani ! Ilifika wakati tukahofia kwamba huenda Polisi wangevurumisha mabomu ya machozi , maana umati wake unazidi ule wa mechi ya Yanga VS Al hilal ya Sudan kwa Mkapa.

Kwenye Hili nimejifunza jambo moja kubwa sana , kwamba USISHINDANE NA ALIYEJAALIWA , UTADHALILIKA SANA , wazalamo wana msemo mmoja kwamba , ACHOLILE KACHORA .
Vp kapicha ili kunogesha
 
Picha picha picha kamandaa
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom