Manung'uniko ya waislam na miaka 13 baada ya kifo cha Mwl Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manung'uniko ya waislam na miaka 13 baada ya kifo cha Mwl Nyerere

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Luno G, Oct 17, 2012.

 1. Luno G

  Luno G JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 22, 2012
  Messages: 1,883
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180

  [h=5]-Inaeleweka kwamba waislam wanamanung'uniko ya muda mrefu kwamba kuna "mfumo kristo" ndani ya Taifa hili, baadhi ya hoja zinazotumika kuthibitisha udini ni
  1. Suala la kuondoa kipengele cha dini katika sensa
  2. Ubalozi va vatcan nchini Tanzania
  3. Kawachongea chombo cha kiislam BAKWATA
  4. Suala la Mahakama ya kadhi
  5. Suala la OIC
  6. MoU katika ya serikali na taasisi za mashirika ya dini hasahasa mashirika ya kikristi
  7. Kudai kutorudishiwa shule zao ambazo zilitaifishwa wakati wa utaifisishaji
  8. Upendeleo katika katika idara ya elimu kwa madai kwamba wanafunzi wengi wa kiislam wanafelishwa
  9. Upendeleo katika nafasi za uongozi kwa madaai kwamba nafasi zote nyeti huwa zinashikiliwa na wakristo nk nk

  -Mara nyingi madai ya waislam yamekuwa yakifungamana na hoja kwamba Mwl Nyerere ndiye muasisi wa mfumo huu inafikia hatua wanamtukana na kumdhihaki huyu Mzee.

  -Sipo hapa kwaajili ya kubishana kwamba je ni kweli mfumo huu umeasisiwa na Nyerere au lah badala yake nipo hapa kwa ajili ya kuwakumbusha Ndugu zangu waislam kwamba huyo wanaemtukana na kumkashifu aling'atuka madarakani 1985 na kufariki dunia 1999

  - Je hata baada ya kung'atuka 1985 waliofuata kuanzia na Mwinyi, Mkapa hadi sasa Kikwete wamefanya lipi kama sehemu ya kuyashughulikia madai ya waislam?

  - Wapo watakaosema hata baada ya kung'atuka kwa Mwl 1985 bado aliendelea kuiongoza nchi hivyo ilikuwa viguma sana waliomfuata baadae kufanya marekebisho juu ya alichokiasisi Mwl sawa ila vipi hata baada ya kifo chake 1999? Mbona madai ya waislam yanazidi kupamba moto mbona serikali iko kimya?

  MANUNG'UNIKO YA WAISLAM NI MTAJI WA CCM NA UDINI NI MOJA KATI YA SERA ZA CCM
  - Ifike kipindi lazima tutambue kwamba serikali ya CCM inayaacha haya yote sababu inafaidika na manung'uniko haya ya waislam ili waendelee kutawala

  - Kwanini serikali isiwaite waislam na kuzungumza nao na badala yake wanakaa kimya na kuwaacha wajifanyie mambo yao ambayo baadhi ni hatari kwa mustakabali ya Taifa hili? Rejea uendeshaji wa Radio Iman

  - Wapo watakaosema oooh serikali inawaogopa maaskofu sasa kati ya serikali na maaskofu nani mwenye nguvu? kama serikali inawaogopa maaskofu ina uhalali gani wa kuitwa serikali?

  WAKATI WA MABADILIKO UMEWADIA
  - Ndugu zangu waislam kama serikali ya CCM imeshindwa kuyashughulikia madai yenu basi ni wakati sasa wakugeukia chama chengine iwe CUF, NCCR, CHADEMA, ADC au chochote kile kitakachoweza kuyashughulikia madai yenu

  NARUDIA TENA KUSEMA KWASASA TATIZO SIO NYERERE TATIZO NI SERIKALI YA CCM.

  Ahsanteni
  [/h]
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
   
 3. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,072
  Likes Received: 10,426
  Trophy Points: 280
  Waislam wanachosha jamani......khaa...
   
 4. UPOPO

  UPOPO JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 1,371
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  sana!!!Wachukua hatua ,mobilize wenziwe waje na miradi ya maendeleo,tumieni resources zilizopo kusaidia vizazi vilivyopo na hatimae kila kaya itaishi kwa amani na upendo. Kwani wakristo hizo shule na vitega uchumi wakati huo walijengewa na serekali,mbona nyingi zilijengwa wakati wa ukolono?wao walikuwa wanafanya nini!
   
 5. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
   
 6. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  makes a lot of sense, comrade!!
   
 7. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,135
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu LUNA naomba kujibu hoja zako kama ifuatavyo.

  [1] Suala la kuorodhesha kipengele cha dini katika sensa.Huo ulikuwa ni msimamo wa serekali kwakuwa serekali yetu haiendeshwi kwa kufuata imani ya dini yoyote.Ikiwa waIslam walitaka kujua idadi yao walikuwa na wajibu wa kujihesabu wenyewe na si kutegemea serekali.

  [2] Ubalozi wa Vatican Tanzania.Hili nalo ni suala dogo sana mbona Iran ina ubalozi Tanzania au hujui Iran ni nchi ya kiIslam.

  [3] Kama serekali iliwaundia BAKWATA kwanini waIslamu wasiunde chombo chao wenyewe ?.

  [4] Mahakama ya Kadhi.Inashangaza kidogo kama si sana waIslam wanalalamikia serekali kuwaundia chombo BAKWATA hapo hapo wanataka waundiwe chombo kingine mahakama ya kadhi !.Serekali imeshasema waIslam waanzishe na kuiendesha mahakama ya kadhi sheikh mkuu Simba kashateua kadhi mkuu malalamiko ya nini tena.

  [5] Ukisoma madhumuni ya OIC kamwe hautataka Tanzania ijiunge na OIC labda kama umijifungia katika sanduku la udini.

  [6] MOU baina ya serekali na mashirika ya kikristo.Ungeenda KCMC au Bugando ungeelewa serekali ina maanisha nini,muIslamu anayelalamika sana sana utakuta anaishi Buguruni na Mbagala hajatembelea Tanzania akaona mahospital teule yanafanya nini.

  [7] Kama zipo shule za waIslam zilizotafishwa na serekali bado hazijarudishwa mpaka leo waIslam wana haki ya kuzidai.Ifahamike kuna baadhi ya shule za kikristo hazijarejeshwa mpaka leo Iiboru ni mfano mzuri.Angalizo kwa waIslam isijekuwa shule wanazozidai ni zile zilizokuwa zikimilikiwa na Agha Khan.

  [8] Hakuna upendeleo historia iko wazi wakristo walipata elimu kuliko waIslamu kwasababu za kihistoria zaidi.

  [9] Hakuna upendeleo wa wanafunzi wa kikristo dhidi wanafunzi wa kiIslam.haya ni madai mfu yanayotolewa na wanaharakati wasiopenda kufanya utafiti.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
   
 10. b

  bdo JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,711
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Kwanza,inaonekana unawakilisha au unawasemea waislaam wenzako, japo ulijitahidi kujivua uhalisia wako, hivyo naona ni hisia zako kama mwislamu.
  Pili,hivi kuna shule ngapi za waislamu zilizotaifishwa na serikali?
  Tatu,hivi wakristo wanachombo gani cha msingi kama ilivyo Bakwata kwa waislam?je chombo hicho cha wakritu kiliundwa na serikali kama Bakwata ilivyoundwa na serikali kama ni kweli?(ushahidi unahitajika kuthibitisha kuwa serikali ndio iliunda BAKWATA)\
  Nne,OIC hilo ni swala linalojulikana kabisa TZ si nchi ya kiislaam (zaidi unataka kuleta ubishi)
  Tano; Hivi inakuwaje waislaamu wao wakiwa na issue zao wanachoma makanisa?
   
 11. b

  bdo JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,711
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Kwanza,inaonekana unawakilisha au unawasemea waislaam wenzako, japo ulijitahidi kujivua uhalisia wako, hivyo naona ni hisia zako kama mwislamu.
  Pili,hivi kuna shule ngapi za waislamu zilizotaifishwa na serikali?
  Tatu,hivi wakristo wanachombo gani cha msingi kama ilivyo Bakwata kwa waislam?je chombo hicho cha wakritu kiliundwa na serikali kama Bakwata ilivyoundwa na serikali kama ni kweli?(ushahidi unahitajika kuthibitisha kuwa serikali ndio iliunda BAKWATA)\
  Nne,OIC hilo ni swala linalojulikana kabisa TZ si nchi ya kiislaam (zaidi unataka kuleta ubishi)
  Tano; Hivi inakuwaje waislaamu wao wakiwa na issue zao wanachoma makanisa?
   
 12. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hawa jamaa watalalamika mpaka mwisho wa dunia! sisi tunajenga mashule,vyuo vikuu,hospitali,real estate n.k
   
 13. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,699
  Likes Received: 7,956
  Trophy Points: 280
  "Hakuna ubongo nje ya kichwa, lakini si kila kichwa kina ubongo"

  Remarks;
  Mwana Mtoka Pabaya
  (1970 - 2060)
  Ikwiririan
  Philosopher & Political Critic
   
 14. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,135
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
   
 15. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,135
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  mkuu,nimeipenda hii.
   
 16. Kwetu Iringa

  Kwetu Iringa JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
   
 17. M

  MTK JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  -Inaeleweka kwamba waislam wanamanung'uniko ya muda mrefu kwamba kuna "mfumo kristo" ndani ya Taifa hili, baadhi ya hoja zinazotumika kuthibitisha udini ni
  1. Suala la kuondoa kipengele cha dini katika sensa
  A: Ni kukidhi mahitaji ya secular state; Serikali yetu haina dini kwa hiyo haihitaji kujua dini za watu ili kuandaa mipango ya maendeleo
  2. Ubalozi vatican nchini Tanzania
  A: Vatican ni dola (City state) kwa hiyo uwakilishi wake katika nchi zote duniani ni wa kibalozi.
  3. Kawachongea chombo cha kiislam BAKWATA
  A: BAKWATA ilikusudiwa kuwasaidia kuratibu mambo yao vizuri zaidi maana walikuwa wanahangaika tu kama kondoo wa mijini wasiokuwa na mchungaji.
  4. Suala la Mahakama ya kadhi
  5. Suala la OIC
  A: 4 na 5 nikama katika no. 1; Ni kukidhi mahitaji ya secular state; serikali isiyo na dini inayoheshimu imani za wananchi wake wenye imani na madhehebu mbali mbalimabli.
  6. MoU katika ya serikali na taasisi za mashirika ya dini hasahasa mashirika ya kikristu.
  A: MoU ilikuwa ya kuainisha jinsi ya kuendesha taasisi za kikristu shule, hospitali nk. kwa manufaa ya watanzania wote waislamu included pasipo mgongano na misuguano.
  7. Kudai kutorudishiwa shule zao ambazo zilitaifishwa wakati wa utaifisishaji
  A: Hili halina mashiko kwa sababu wakristu walipoteza shule nyingi zaidi katika utaifishaji huo, na waislamu hawajawahi kukatazwa kusoma au kutibiwa katika shule na hospitali za kikristu; watafute jingine hili ni wash out!
  8. Upendeleo katika katika idara ya elimu kwa madai kwamba wanafunzi wengi wa kiislam wanafelishwa.
  A: Tatizo lao ni kujikita zaidi katika madrasa na itikadi za kimujahedina na kusahau elimu dunia, ikifika mitihani haiulizi Osama bin Laden aliuawa nchi gani! wanaangukia pua na kuwalaumu wakristu!
  9. Upendeleo katika nafasi za uongozi kwa madaai kwamba nafasi zote nyeti huwa zinashikiliwa na wakristo nk nk
  A: Hili linatokana na jibu la no. 8; umujahedina!! wakati ambapo serikali inaendeshwa kitaaluma wala sio kitalibani, wakishindwa usaili wanawalaumu wakristu. lol!

  Bottom line: Ndugu zetu waislamu hebu jaribu sana kuwa sehemu ya ufumbuzi wa tatizo badala ya kuwa sehemu ya tatizo lenyewe! Binafsi naamini wakristu hawana tatizo na uislamu wenu bali wanachukizwa na kukerwa sana na tabia ya waislamu ya kuangalia kila jambo katika sura ya ukristu na uislamu tu!

  Kuchoma taasisi za kikristu na vurugu za kihayawani hakutaweza kamwe kuififisha imani ya kikristu sana sana vitendo nyenu vinawaimarisha wakristu katika imani na umoja wao. Wakristu hawatauacha ukristu wao eti kwa sababu waislamu watatuua, la hasha!! wananchi wa afrika ya kusini licha ya ubabe, vitisho na mauaji ya kutisha hawakusambaratika bali walijiimarisha katika umoja wao na kufanikiwa kuwabwaga makaburu; wakristu vivyo hivyo.
  Kasi ya waislamu kulielewa hilo itawasidia sana kujitambua na kuwa sehemu ya ufumbuzi wa matatizo yao babdala ya kuendelea kuwa sehemu ya tatizo.
  Waislamu wakumbuke mambo mawili muhimu sana:
  1: KIENDACHO HURUDI na
  2: Ukimya au kutokulipiza kisasi kwa wakristu kwa vitendo hivi vya kihayawani katu wasikuchukulie kwamba ni woga au udhaifu bali ni matokeo ya malezi na mafundisho ya imani yetu wakristu, WAACHENI HAWAJUI WALITENDALO na kuuachia utukufu wa mwenyezi Mungu kwamba atalipatia ufumbuzi tatizo lililopo badala ya kumwaga na kuharibu mali za waliomo na wasio kuwemo kwa visingizio hewa!
  Wakristu wakifikishwa mahali; between a rock and a hard place itakuwa hadithi ya kumfungia paka kwenye chumba kisha uanze kumuadhibu; kuna siku watasema LIWALO NALIWE! hapatatosha! na vita huwa haina macho; hakuna anayeweza kusema kwa uhakika kwamba atakuwa salama, awe mkristu ua awe muislamu.
  TUZINDUKE
   
 18. stineriga

  stineriga JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 2,033
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Kuna tofauti kubwa sana juu ya familia za kikristo na kiislam, familia za kikirsto wameweka elimu dunia mbele, waislam tunatanguliza mbele madrasa elimu dunia nyuma!

  Kwenye familia ya kiislam mtoto anaweza kuamka tu asubuhi na kusema hataki shule anataka kuolewa au anataka kuwa mvuvi na hakuna baba au mama ambaye atamfanya chochote, na ukweli ni kwamba atakwenda kuozeshwa au kwenda kwa bwana na wazazi wakifurahia tu, au atakuwa mvuvi na kufurahia vihela vidogo viodgo bila ya wao wazazi kuangalia future ya mbeleni ya huyo mtoto itakuwaje!

  Lakini kwenye familia ya kikristo mtoto aamke tu asubuhi halafu aseme hataki shule ataanzia anzia wapi???
   
 19. m

  mikogo Senior Member

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni rahisi kutoa maneno ya kejeli
  si rahisi kuto majibu ya hoja zilizopo mezani
  ni kweli hakuna ubongo nje ya kichwa lakini si kila kichwa kina ubongo.
  Wana jf tafakuri yenye ukweli kwa maana ya ukweli na si ubingwa wa kejeli utatutoa kwenye hili.

  Hakuna mwenye kuchekelea kubezwa.

  Tutajenga amni kwa kuheshimiana.
   
 20. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mimi naona hata dunia yenyewe ni mfumo kristo tuichome moto tutengeneze nyingine.
   
Loading...