Manung'uniko nafsini: Tabia ya ukosefu wa uungwana wa kibiashara kwa Precision Air! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manung'uniko nafsini: Tabia ya ukosefu wa uungwana wa kibiashara kwa Precision Air!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kisusi Mohammed, Oct 12, 2012.

 1. Kisusi Mohammed

  Kisusi Mohammed JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 442
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Habari za majukumu waungwana, natumai Mungu anatujaalia hali njema na afya za uhakika mpaka tunapata fursa za kupita huku jukwaani na kuweka hisia zetu.

  Ni muda mrefu nimekuwa nikiamini ya kwamba ndege ni usafiri wa haraka na hurahisisha shughuli za kijamii hasa kwa wafanyabiashara na watu wenye kufanya kazi zao kwa kujali muda, bila kusahau makundi yote yanayokwepa usumbufu wa usafiri wa aina tofauti na ndege kwa kuikimbilia ili kupata huduma bora na za uhakika.

  Hivi karibuni nimekuwa nikisiskia abiria wengi wanaopanda Precision ya kuelekea Mwanza wakilalamika kuwa mara wanacheleweshwa, mara ndege zinaahirishwa kienyeji, mara wanacheleweshwa kwa kupitishwa route ndefu bila kupewa taarifa, ila kwa sababu nahisi kuwa route ya Mwanza imekosa usafiri wa uhakika kwa muda mrefu hasa wa ndege kwa hiyo Precision wameamua kuitumia fursa hii kuwanyanyasa abiria wake.

  Wadau naamini sauti za wengi ni sauti zenye mshindo, hebu wahanga na wenye maoni juu ya hili wafunguke hapa tujaribu kutafakari na kutafuta suluhisho ili pesa zetu zisiendelee kutunyanyasa!

  Nna uchungu, nimesafiri toka Dar leo 11/10/2012 tumeondoka Dar saa 12 na dkk 10 jioni, tumeingia Mwanza saa 3 na dkk 10 usiku, si aheri ningepanda ungo wa bibi nikawahi!

  Inauma sana
   
 2. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Nadhani kwa Tanzania kila kitu sasa kiko kwenye grinding halt. Ukipiga simu ndiyo usiseme. Ukienda kuripoti tukio polisi unaulizwa kama una pesa ya kukodisha taxi--- hapa bado hawajataka chao! Ukiwasili uwanja wa ndege kila jambazi anayeitwa afisa kodi uwanjani anatumia sheria zake kukutoa upepo. Ukienda kwa rais yeye siku zote yupo angani na kimwana chake wakijinoma. Kwa ufupi hiyo Precision si precision tena bali precinct of corruption and red tape. Ukitaka kuwahi Tanzania ni kujiua tu ingawa nako kuna gharama. Pia kutolewa upepo ni huduma ya haraka sana ukiachia mbali kuchapwa na polisi.
   
 3. chamakh

  chamakh JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 692
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 60
  I strongly concur with you sir! I travelled one time with Precision Air from Dar to Nairobi yaani acha tu, tulikuwa tuondoke dar saa 11 jioni tukaambiwa tutaondoka saa 12 jioni, then saa 2 usiku ikaja saa 4 usiku and finally saa 5 usiku, yaani nilishindwa kuelewa kabisa utendaji kazi wa hii kampuni
  Awali nilidhani kwa kuingia ubia na Kenya Airways kungeleta ufanisi bora lakini aah wapi naona wakenya wamefanya ujanja wa kujipatia tu abiria wanatoka Dar kwenda Jomo Kenyatta lakini ufanisi wa precision ukisuasua
   
 4. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  yaani naiaubiri kwa hamu hiyo ATCL ya ijumaa ya leo!


  PA, wanadharau...

  kuna siku kutoka dar kwenda mwanza tumesha-check in jioni saa kumi tukakaaaaaaa hadi saa tatu usiku then wakaahirisha safari, halafu kuna abiria anakaa kimara hana hata usafiri na yuko na mtoto!! unajiuliza afanyeje?


  Same thing, mkiwa kule MWZ wana delay na kyahirisha safari, nakubaki kuwatupa La Kairo tu!!

  Si ustaarabu, and siku hizi nadhani bora hata kupanda Basi tu.
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  ATCL may very well be even worse!
   
 6. Kisusi Mohammed

  Kisusi Mohammed JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 442
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Hii inauma sana na inarudisha kama si kuyaua kabisa maendeleo ya nchi yetu, sasa sisi kama wadau na watu tunaoitakia mema nchi yetu inayonyonywa na utawala wake wenyewe tunafanyaje kukabiliana na haya!?
   
 7. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  i understand...few years back badala ya kutushusha MWZ kutoka dar tukafika hadi NRB ndio tukashushwa mwanza kwa sababu za ajabu ajabu...hapo mipango yako yoooote ilishavurugika!
  What i do like abt them ni kwamba they know how to keep time!Just that.
   
 8. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  :nerd::nerd::nerd::nerd::nerd::nerd::nerd::nerd::nerd::nerd::nerd::nerd::nerd::nerd::nerd:
  Rwanda air mpango mzima.....!
  Kenya Airways....!
  Ethiopian Airways...!
   
Loading...