Manumba jiuzulu, au kikwete mfukuze kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manumba jiuzulu, au kikwete mfukuze kazi

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by NewDawnTz, Dec 26, 2010.

 1. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  :embarrassed:

  Ninachofahamu ni kuwa Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa mfumo wa Katiba. Kwa mantiki hii ni lazima kila kiongozi, iwe kwa kupenda au kwa kutokupenda awe anaifahamu katiba kabla ya kuridhia kukubali wajibu wake.

  Hii ndiyo sababu hulazimika kula kiapo kwa kutumia katiba hii ikimaanisha ya kuwa tayari wanaifahamu katiba na wako tayari kuitekeleza katika utendaji wao wa kazi wa kila siku. Naamini hata ndugu yangu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (Director of Criminal Investigation - DCI) Bwana Robert Manumba alikula kiapo hiki wakati anakubali jukumu hili kubwa sana katika nchi yetu ya Tanzania.

  Alichokiongea leo kwenye kipindi cha Siasa asubuhi Star TV kimenipa mshituko mkubwa wa uwezo wa Manumba katika kutekeleza majukumu yake.

  Akitakiwa kujibu swali aliloulizwa na Baruan Muhuza kuwa Je kitendo cha Polisi kutumia nguvu nyingi zisizokuwa na sababu ni matokeo ya mapungufu ya katiba, DCI Manumba alianza kujibu kwa kujiamini na kusema ya kuwa "Japo kuwa mimi si mtaalam sana wa Mambo ya katiba....". Hii ni kauli dhaifu sana kutoka kwa mtu kama Manumba.

  Alikuwa ana maanisha nini kusema sio mtaalam wa mambo ya katiba? Je alitaka umma wa Watanzania ujue ya kuwa hana Shahada au Masters ya Katiba? Je alitaka tujue ya kuwa haifahamu katiba? au alitaka kumaanisha nini??

  Na mtu kama yeye kutoa kauli kama hiyo hapo Je Sio ishara ya kuwa wako wengi wa aina yake waliokula kiapo cha katiba lakini hawaijui na hivyo hawawezi simamia itekelezwe?

  Kwa kauli hii nimemtoa Manumba na hata alipozungumzia kurekebisha jeshi la Polisi nilijiuliza zaidi, analirekebisha kivipi wakati katiba yenyewe "Hana Utaalam Nayo"? Au ni marekebisho ya kuendelea kuisigina na kutokuitekeleza katiba?

  Hii inamaanisha wazi tu ya kuwa tusitegemee kuwa na jeshi lenye kulinda katiba (japo ina mapungufu lakini yako mengi ya msingi ya kutekelezwa na ya kawa na manufaa kwa jeshi letu) kwa kuwa wenye jukumu la kuliunda Jeshi hili la Polisi lifanye kazi yake kikatiba hawaijui katiba.


  Manumba kwa upungufu wa kutokuwa na "utaalam" na katiba uliyoapa kuilinda, nakushauri uachie ngazi...la sivyo, Mheshimwa JK timua kazi huyu mteule wako maana amekuabisha kwa kukutania kula kiapo kwa katiba asiyo na "utaalam" nayo
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  yes.... manumba alitakiwa kufahamu misingi yote ya sections za sheria mama zinazohusu polisi pamoja na the whole doctrine of criminal investigation kama alivyothaminiwa na dola kuwa director of criminal Investigation.... cha kushangaza huyu bwana kumbe ni polisi tu wa kawaida kutoka Chuo Cha Polisi Moshi (CCP) ......

  Kwa mantiki hii sioni ajabu polisi kutumia nguvu pasipo lazima na polisi kuvunja sheria na katiba kuhusu haki za binadamu kwani wao wenyewe hawazijui sheria hizo..... polisi watachungaje sheria zisivunjwe kama hawana uwezo wa kutambua kanuni mbali mbali za sheria kabla ya kutekeleza majukumu...

  inashangaza sana....
   
 3. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mweee, jamani wengine tulishasahau kama viongozi wa Tz huwa wanajiuzulu au kufukuzwa kazi. Aanze Edward Hosea kwanza vinginevyo JK wala Manumba hawatatusikia
   
 4. Rwamuhuru

  Rwamuhuru Member

  #4
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika haya ni mapungufu makubwa.

  Mwenyewe nilimsikia lakini nilidhani ya kuwa nimemsikia vibaya.

  Pamoja na ukweli ya kwamba sio utamaduni kwa viongozi wetu kujiuzulu hata kama watakutwa na kashfa kubwa kiasi gani, nadhani Kikwete ana jukumu la kumtia kazi Manumba

  Hakika huu ni upungufu mkubwa kwa mtu wa nafasi kama ya Manumba ambae anajukumu la kuhakikisha wananchi wanalindwa na kupata haki zao za kikatiba wakati wote. DCI na DPP ni miongoni mwa watu kwenye vyombo vyetu vya usalama wanaopaswa kulala na katiba pembeni yao
   
 5. D

  DENYO JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tangu lini paka amfunge kengele mwenzake wote wawili sawa -zamani nilidhani viongozi wa juu wa jeshi kidogo wanafikiri lakini manumba nimemtoa kwenye orodha ya viongozi ni kati ya wale askari amabye akiambiwa na bosi wake twanga anatwanga bila kujua kwanini anatwanga harafu mwisho wa siku anafukuzwa kazi yeye, jeshi limekuwa na mapokezi hayo kwamba afande akisema no question ni utekelezaji-sikuamini kusikia alichokuwa anakiongea manumba -dci manumba ulikuwa uozo mtupu. Deusi kibamba alimwambia kwanini polisi mnakimbilia kuzuia mvua inayotaka kunyesha na kumwacha anayesababisha akilindwa??? Mkurugenzi analazimisha uchaguzi kumfurahisha makamba lakini hatari yake wananchi wanaandamana kwanini wasimhoji mkurugenzi huyu??? Bodi inachelewesha mikopo na stahili za wanafunzi kwa muda mrefu na bila maiijbu wala taarifa sahihi wanafunzi wanagoma unawapiga mabomu kwanini polisi wasihoji bodi? Mkurugenzi anabadili matokeo wananchi wanayakataa polisi wanapiga mabomu kwanini polisi wasimhoji na kumchukulia hatua mkubwa aliyevunja kanuni? Dci alishindwa kabisa kuainisha kwamba amani inaendana na haki utawezaje kulinda amani wakati haki inaporwa? Dci manumbi amechemka na anafaa kuwajibika ajiuzulu -anabaliki polisi kumpiga mbunge aliyekuwa anadai haki-anabariki polisi kuvunja kanuni na sheria za nchi hii kwa kigezo cha kulinda amani -amani gani hiyo pasipo haki? Ni vema polisi kuelewa kuwa hawako juu ya sheria na wajue kwamba nguvu ya umma ni zaidi ya polisi itakuja kuwashukia siku moja
   
 6. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,037
  Likes Received: 7,474
  Trophy Points: 280
  With all due respects guys.... Sikumsikia DCI Manumba akiongea katika kipindi hicho cha asubuhi, lakini kauli/statemet ambauo mtoa mada ameitumia katika kutaka kumuwajibisha au kumhukumu/kumtuhumu DCI, kwangu mimi haijakaa vyema. Kama amekiri kuwa yeye si mtaalamu wa Katiba, hapo kuna tatizo gani, yeye hutenda kazi zake kwa mujibu wa sheria na pia wana miiko yao ambayo utungwaji wake ndiyo hufuata katiba, Polisi si lazima awe mwanasheria, jeshi la Polisi huajiri wataalam mbalimbali wa fani tofauti, hivyo ujuzi wa katiba si hitaji pekee unapojiunga na jeshi la Polisi, kama kuna mtu ambaye alipaswa kushutumia iwapo angetoa kauli ya aina hiyo hapo ni mwanasheria mkuu wa serikali.
  Ningemshangaa kama Manumba angejifanya ufundi wa kuchambua katiba wakati si kazi ya Polisi, Polisi hufanya kazi zao kwa kufuata Acts na Codes (Codes ni sheria zilizorithiwa toka kwa mkoloni).
  Ona mwingine naye anasema kumbe Manumba ni Polisi wa kawaida tu kutoka CCP, je ni Polisi gani wa nchi yeye hii ambaye hakuwahi kupitia CCP? pia aelewe kuwa Manumba ni senior commissioner, hakumaliza tu CCP na kufika hapo alipo, bali alihudhuria kozi tofauti za kipolisi ikiwemo mafunzo ya maafisa wake pale kurasini na mafunzo mengine ya maofisa katika vyuo vya ndani na nje ya nchi.
  Kama kuna udhaifu mwingine aliuonyesha katika mahojiano hayo basi ajdiliwe kwa hayo lakini katika hili mimi sikubaliani hata kidogo na huo unabaki kuwa msimamo wangu, labda kama muwasilisha mada amekosea kitu
  Tusipende kulaumu tu bila kuangalia mambo kwa undani, Jamii forrum inabidi ipewe heshima yake kama maudhui ya uanzishwaji yake yanavyoeleza ni lazima iwe kweli 'Hom of Great Thinkers' na wenye jukumu la kuifanya hali hiyo iendelee ni sisi wenyewe kwa kuacha uvivu wa kufikiri na kuchunguza mambo.
  Naomba kuwasilisha
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  RM ..... tunashukuru kwa mchango wako...... how could someone of top heirachy execute his duties especially that of a state organ without a knowledge of the act that give ways for sections and subs regarding the functions of his/her organ..... hukutakiwa kukosoa katiba bali ungezungumzia katiba inasemaje juu ya jeshi la plolis kwa ujumla...., ambapo mimi nasema dhana ibadilike .... hichi chombo cha dola iwe ni police service na sio police force.... ok RM
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Na mimi sijakuelewa wewe pia hivi wanapoapa kulinda na kuitunza katiba huwa wanaapa kuhusu katiba ipi? ile waliokwenda kuisomea shule au ni ipi? Au ni hii hii wanayosema hawaijui? I mean hawana utaalamu nayo? lool
   
 9. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  ndugu, uliza kwanza hiyo katiba inafundishwa kwenye mitaala yao ya mafunzo? Wale huwa wanasoma katiba ina sura ngapi? Zitaje...
  Akimaliza hapo anakula kiapo cha kuilinda na kuitetea,wakati huo ameshikilia silaha *bunduki au jisu kubwa/sword*
   
 10. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  We hujui unachoongea Mkubwa!DCI ilo neno la Mwiso"I= Investigation" huwezi kufanya kama hujui sheria na katiba ya nchni yako; ndio maana Watanzania maskini wamejaa magerezani kwa kesi za kusingiziwa, raia anayechunguzwa na Polisi lazima apate haki zake za ki-katiba atapata vipi kama Manumba hazijui? angalia uwezo wa Polisi wetu; neno la pili "C=Criminal" hatajuaje criminals kama hajui Sheria na Katiba?!! na la mwanzo "D=Director" yeye ndie anategemewa kuwa kichwa cha kitendo hicho sasa kichwa kikiwa hivyo unavyoelezea hapo juu unategemea nini?? Kwanini alikubali kufanya kazi hasiyoiweza? Kaka Polisi anapaswa kuijua katiba na "Laws of Tanzania" zote kwa umakini siyo kwa ajili ya haki za Mtuhumiwa tu bali pia iliaweze kujua anataka kuchunguza nini na sheria gani imevunjwa sio ubabe na misuri hayo maelezo labda yangetolewa na mkuu wa FFU labda tunge-msamehe siyo DCI! aondoke labda alipewa kama zawadi siyo uwezo
   
 11. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Binafsi sikusikiliza wakati anaongea lakini kama ni kweli Manumba unaongea mambo ya utata! Utafanya vp criminal investigation without laws? And katiba is the motherlaw? Anataka kusema ikitokea mkanganyiko wa kikatiba director/dci atakaa pembeni akiangalia wajuzi wa katiba? Kwa iyo crime against it can't be adhered to by Manumba? Kuna mwingine ni msanii wa uchumi aliwahi kusema hajui kwa nini Tanzania ni maskini,akaongezea kuwa ukiona magari mengi barabaran ujue watz ni matajiri! Kwa mtindo huu tuendako bado ni mbali. Kama manumba hajui anakokwenda je anajuaje kama amepotea?au kila anakofika anajua yuko sahihi hata kama siko alikokuwa anaelekea! Namaanisha crimes anazitambuaje kama hajui sheria mama,katiba? Ukimweleza kuwa tunahitaji katiba mpya atakuelewa?au atadhani wee ni mkorofi mpenda jinai? Ajabu sana! Ila mi sishauri ajiuzulu maana Msafiri anaweza kumweka mshikaji wake wa ajabu ajabu zaidi ya uyu. Si unajua IQ ya sasa ya uyu Msafiri?
   
Loading...