manufaa ya shirika la wanyamapori tanzania

RIVI SHIRIMA

Member
Jan 22, 2012
31
2
kweli tuna shirika la hifathi la wanyama pori linaitwaTANAPA kwani limetoke kufahamika na wanaozungukwa na hifathi 2 je kwa wanaoishi miko ya mbali wana nufaikaje na HILI SHIRIKA TANAPA
 
Kwanza, sio Shirika la Hifadhi ya Wanyamapori, bali ni Shirika la Hifadhi za Taifa, na linashughulika na uhufadhi kwa ujumla wake katika maeneo ya hifadhi ya Taifa ikiwa ni pamoja na Wanyamapori, makazi ya wanyama hao, kuboresha uoto wa maeneo hayo, ushirikishwaji jamii, n.k. TANAPA wanapeleka makusanyo yao hazina na baadae hupatiwa mgawo kutoka huko hazina kwa ajili ya uendeshaji wa shirika. Hivyo kwa wananchi walioko mbali na hifadhi za taifa wanafaidika kutokana na mapato yanayopelekwa hazina na baadae kutumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo. Zipo faida nyingine za huduma za mazingira tunazozipata kutoka katika hifadhi zetu za taifa. Vyanzo mbalimbali vya maji vimehifadhiwa vyema katika hifadhi hizi za Taifa, na maji haya hutiririka nje ya hifadhi na kutumika kwa shughuli mbalimbali kama kilimo, kunywewa na mifugo na binadamu, kuzalisha umeme, Iko mito mingi tu ambayo vyanzo vyake viko katika hifadhi za taifa na kama sio jitihada zinazofanya na TANAPA leo hii tusingekuwa na maji tunayoyaona yakitiririka kwa kiasi cha sasa katika mito hiyo, kama Pangani, Ruaha, n,k. Zipo faida nyingine kama kuchuja hewa ya ukaa kutokana na uoto wa asili uliohifadhiwa vizuri katika hifadhi hizo hususani misitu. Hifadhi za Taifa pia ni sehemu za kwenda kujipumzisha na mahala pa kujifunzia maisha ya wanyama na mazingira kwa ujumla. Niishie hapo, ila kwa kweli faida ni nyingi.
 
Back
Top Bottom