johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,614
- 141,432
Nauliza tu mantiki ya wanasiasa na wananchi kwa ujumla kuratibu bei za vyakula wakati wa mwezi wa Ramadhani. Nijuavyo mimi kufunga ni ibada na tufungapo mambo yanatakiwa kuwa kama yapasavyo na si kutengeneza nafuu/ urahisi fulani katika mfungo. Wale wafungao Kwaresma vitabu vinawataka wasiwe kama wanafiki wenye nyuso za kukunjamana na midomo mikavu bali waenende bila kujulikana kama wapo katika swaumu. Nitashukuru nikipata majawabu, amen!