Manka: 'Konda' wa kike anayeishi kiume

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
51,309
2,000
Manka: 'Konda' wa kike anayeishi kiume Send to a friend Thursday, 04 November 2010 13:23 0diggsdigg

Stumai Baraka

Na Florence Majani

UKIMWANGALIA kwa wasiwasi unaweza kudhani kuwa ni mwanamume ukataji wake wa nywele, mavazi na macho yake mekundu vinawafanya wengi wadhani kuwa ni mwanamke.

Namkuta akiwa kazini kwake au ofisini. Ni ndani ya daladala inayofanya safari zake Tabata Segerea kwenda Temeke yupo dirishani ametoa kichwa, anaita abiria kama wafanyavyo utingo wengine wa kiume. Ukimtazama machoni utagundua kuwa yu makini hana muda wa kuchekacheka, amevaa sare zake za kazi suruali na shati za rangi ya bluu ambazo zimemkaa vyema. Anazungumza kisela kama walivyozoea kusema vijana wa sasa.

Huyu ni Stumai Baraka au Manka, mwana mama aliyeamua kufumba macho na kuamua kuitafuta fedha kwa kufanya kazi ya utingo bila kujali jamii inamtazamaje.

Alizaliwa miaka 30 iliyopita katika Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro na kupata elimu yake ya msingi katika Shule ya Lang’ata. Hakufanikiwa kuendelea na elimu ya sekondari kwa kuwa wazazi wake hawakuwa wakijiweza. Alibaki nyumbani akisaidia kazi za kawaida hadi pale alipopata mpenzi ambaye waliamua kuishi pamoja.

“Nilikaa nyumbani muda kidogo, nikapata mpenzi tukaamua kuishi pamoja na mwaka 2000 tulibahatika kupata mtoto wa kiume Anaseli Arnold ambaye ana miaka miaka kumi na moja sasa. Kwa bahati mbaya mwaka 2003 mume wangu alifariki kwa ajali ya gari.”

Baada ya mumewe kufariki maisha yake yalibadilika kwa kiasi kikubwa, mazoea na mapenzi aliyokuwa nayo kwake yalimbadilisha tabia kiasi cha kupata msongo wa mawazo na kisha kuwa mtu tofauti.

“Kipindi cha nyuma sikuwa na maisha ya kiumeume hivi, sikuwa nikivuta sigara wala kuvaa kiume lakini Anorld wangu alipofariki smwaka 2003 nilipatwa na msongo wa mawazo na hapo ndipo maisha yangu yalipobadilika yakawa magumu na ndiyo nikaamua kujichanganya kama unavyoniona,” anasema Manka.

Alijichanganya vipi? Aliingia katika makundi ya vijana wa kijiweni akitumaini kufarijika lakini alijikuta akiangukia katika ulevi, kuvuta sigara na kuishi kisela au kidumedume.

Ili kukabiliana na ugumu wa maisha Manka alifunga safari iliyomfikisha Chalinze, Mkoa wa Pwani ambako alipata kazi ya kuuza duka aliyoifanya mpaka mwaka 2008.

“Ile biashara ya duka ilidumu miaka mitano tu. Mwaka 2008 ilifilisika na 2009 nikaingia rasmi katika biashara ya daladala. Nilitafuta hii kazi mimi mwenyewe lakini nilianzia kwa mjomba wangu. Gari letu lilikuwa likifanya ruti za Tabata Kimanga kwenda Temeke lakini baadaye niliachana nalo na kupata ofisi nyingine ambayo ndiyo niko mpaka sasa hivi,” anasema Manka na kuongeza:

“Tangu wakati huo mpaka sasa wamiliki wa magari wananigombea wanataka nifanye nao kazi, lakini mimi nina msimamo, siwezi kuacha kazi kiholela.”

Maumbile yake yanayoshabihiana na ya kiume yamekuwa yakiacha maswali lukuki kwa wale wanaomuona kwa mara ya kwanza. Wengi wao humshangaa na baadhi kumuuliza au kujikuta wakijisemea peke yao.

“Wakati mwingine nikiwa ofisini kwangu (ndani ya daladala) abiria wanaulizana wao kwa wao, huyu mwanamke au mwanamume, basi mimi nawajibu unatafuta bwana, mke au unasafiri? Wananyamaza na tunaendelea na safari kama kawaida,” anasema.

Lakini Manka anashangazwa na jinsi baadhi ya wanawake na wasichana wanavyomtongoza ilhali wengine wanajua kabisa kuwa ni mwanamke mwenzao... “Nakutana na wanawake wengi, wengine watu wazima na mabinti wadogo, wananitongoza kabisa, baadhi wanafikiri kuwa mimi ni mwanamume na wengine wanajua fika kuwa ni mwanamke mwenzao lakini bado wananiganda. Lakini mimi nawakaushia kwa sababu sasa hivi sitaki bwana, mume wala sitaolewa milele, maisha ya usela ni bora zaidi, najimiliki,” anasema Manka.

Lakini tofauti na hilo, anasema wanaume wengi wanamchukulia kama mwanamume mwenzao na hawathubutu kumtongoza wala kumtania.

Biashara za vyombo vya usafiri zinahusisha jamii hivyo ni aghalabu kwa utingo wa daladala kukumbana na changamoto mbalimbali na Manka kama wenzake, amekuwa akikutana nazo lakini ametokea kuwa mahiri katika kuzikabili.

Kero kubwa anazokutana nazo ni kutoka kwa abiria, hasa wanafunzi na walevi usiku... “Ni kawaida kwa daladala kuchosha, naamka saa 10:00 alfajiri na kulala saa tano au sita usiku kila siku, kasoro siku za mapumziko ambazo ni mara moja kwa wiki mbili."

"Lakini tatizo kubwa liko kwa abiria ambao ni wasumbufu na wakorofi. Utakumkuta abiria anatoa fedha isiyotimia bila kuomba kwanza, ukimwambia anaanza kutoa matusi. Kwa mfano, kutoka Segerea hadi Temeke nauli ni Sh350, abiria akikomea Buguruni anatozwa Sh250 lakini ukimwuliza unaishia wapi ili umtoze kutokana na anapoishia anakujibu kwani gari linakwenda wapi? Sasa huyo si anatafuta kupigwa,” anasema Manka kabla ya kupuliza moshi wa sigara hewani.

Anasema kingine kinachomkera ni wanafunzi ambao anadai kwamba watiwa jeuri na serikali. Analalamika kwamba wengi wao ni wakorofi, wanakaa kwenye siti ukiwaambia wawapishe wakubwa wanatukana ukiwajibu, abiria hao hao wanaanza kukushambulia.

“Mwanafunzi mdogo kabisa kiumri na anaweza kuwa mtoto wako lakini anakutukana, sijui wanaionaje hii kazi, halafu abiria hawamkemei, sasa maadili yanakwenda wapi kama tunawafundisha watoto wawe wakaidi namna hii, lakini mimi mwenyewe ni mkorofi kupindukia nakwenda nao sawasawa.”

“Vilevile tunakutana na askari wa usalama barabarani ambao mimi mwenyewe ndiyo huwa nazungumza nao na kumalizana nao na nimeshawazoea.”

Pamoja na kuwa na changamoto za hapa na pale, biashara ya usafirishaji wa abiria imemnyanyua kiuchumi tofauti na awali kwani sasa hivi ana uhakika wa kuyaendesha maisha yake vyema.

“Biashara hii haina mshahara, unapewa gari halafu unaambiwa umpelekee tajiri kiasi fulani, hiyo inaitwa hesabu ya tajiri, kwa mfano sisi tunatakiwa tupeleke Sh40,000. Hivyo hatuna budi kuwajibika tupate zaidi ya kiasi kinachohitajiwa, kinachobaki ndiyo mshahara wetu.

Kwa fedha hizo nimefungua duka la bidhaa za vyakula, ninawasomesha wadogo zangu, namlea mtoto wangu na mama yangu,” anasema Manka.

Manka anategemea kupumzika biashara hii ifikapo Januari mwakani. Anasema baada ya muda huo atakwenda kupata mafunzo ya kuendesha gari kwani anatarajia kuwa dereva siku za usoni na si utingo tena.

“Ninajua kuendesha gari lakini nataka vyeti vya chuo cha usafirishaji ili nipate na leseni mpya kwa sababu baadaye nataka kuwa dereva wa ukweli,” anasema.

Lakini kama kuna jambo linalomkera Manka kuhusu wanawake wenzake ni wale wanaoishi kwa kutegemea kuuza miili yao. Anasema hayo ni matokeo ya kuchagua kazi... "Mafanikio hayaji kwa kuuza utu, kuwajibika ndiko kunakodhihirisha utu wa mtu."jiko:mwananchi
 

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
51,309
2,000
Manka: 'Konda' wa kike anayeishi kiume Send to a friend Thursday, 04 November 2010 13:23 0diggsdigg

Stumai Baraka

Na Florence Majani

.

Lakini Manka anashangazwa na jinsi baadhi ya wanawake na wasichana wanavyomtongoza ilhali wengine wanajua kabisa kuwa ni mwanamke mwenzao... "Nakutana na wanawake wengi, wengine watu wazima na mabinti wadogo, wananitongoza kabisa, baadhi wanafikiri kuwa mimi ni mwanamume na wengine wanajua fika kuwa ni mwanamke mwenzao lakini bado wananiganda. Lakini mimi nawakaushia kwa sababu sasa hivi sitaki bwana, mume wala sitaolewa milele, maisha ya usela ni bora zaidi, najimiliki," anasema Manka.

Lakini tofauti na hilo, anasema wanaume wengi wanamchukulia kama mwanamume mwenzao na hawathubutu kumtongoza wala kumtania.

jiko:mwananchi

dada zetu wa kibongo kwa kuwatongoza makonda hawajambo
 

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,363
2,000
jamani kwanza tumpe pongezi zake...isipokuw a nimewah pata 2 of them(KATIKA INDUSTRY) i tell you from expirience...you have to be careful... la sivyo SOUND KWA KWENDA MBELE
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom