Manji na Gwajima waondolewa Kituo cha Polisi na gari jeupe chini ya ulinzi kuelekea katikati ya jiji

Reucherau

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
756
1,740
MANJI, GWAJIMA POLISI: Yusuf Manji na Askofu J. Gwajima waondolewa Kituo Kikuu cha Polisi Dar na gari jeupe chini ya ulinzi mkali na kuelekea katikati ya jiji.

Baada ya Askofu Gwajima na Mwenyekiti wa Yanga na Mfanyabiashara Yusuph Manji kuwasili kituo cha kati cha Polisi Dar es Salaam na kukaa zaidi ya saa zaidi ya 5, wameondolewa kwenye eneo hilo.

Gwajima na Manji wamepakizwa kwenye gari moja na kuelekea sehemu ambayo kamishina wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro hakutaka kuweka wazi lakini akawaambia Waandishi wa habari waliokua nje ya kituo kuwa taarifa rasmi atazitoa kesho Ijumaa ya February 10 2017.

 
Kimsingi nyuma ya balozi wa nyumba kumi kunawatu vivyo hivyo kwa viongozi wengine wa juu wa chama,serikali,dini,company n.k.
 
Watazungushwa Dar mpaka usiku kisha kutunzwa mahali Fulani pa salama sana wakisubiri mahojiano ya kesho! Heshima lazima irudi! Hivi MKUU wako anakuita kesho halafu wewe unaita waandishi wa habari na kumponda sana kisha unaamua kwenda leo! Maana yake ni kwamba:
1. Huna mamlaka ya kunifanya nitii ratiba yako, inabidi uvunje ratiba yako halafu ufuate ya kwangu! Yawezekana Manji amepanga kwenda nje ya nchi siku ya ijumaa kwa hiyo ratiba yake haiwezi kuingiliwa!
2. Sikuogopi! Kuonyesha kuwa sikuogopi na huwezi kunifanya lolote, sisubiri ijumaa nakuja kesho!
Ili kutetea heshima ya serikali hawa watunzwe mpaka kesho!
 
Naona wakilala ndani hawa jamaa mpaka kesho"
c6ac73bae7d927088c7bbda8e3c5667c.jpg
 
Back
Top Bottom