Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 20,690
- 20,450
MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Manji amesema kwamba hawakumsajili Juma Kaseja kwa ajili ya kuifunga Simba SC, bali wamemsajili awasaidie kwenye michuano ya Afrika. Manji ameyasema hayo leo asubuhi makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, siku moja baada ya Yanga kufungwa 3-1 na Simba SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe Uwanja wa Taifa, Kaseja akiwa langoni. Manji alikuwa akimjibu Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali aliyeushutumu uongozi kusajili Juma Kaseja ni makosa. "Huyu mzee nadhani umri umemzidi, lakini nataka nimkumbushe, huyo Ivo Mapunda aliondoka Yanga akiwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita na uongozi wa wakati huo kwa tuhuma za kufungisha kwenye mechi na Simba SC,".
Source: Bin Zubeiry blog
Source: Bin Zubeiry blog