Manji anakwepa hukumu ya EPA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manji anakwepa hukumu ya EPA?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Kiranja, Oct 28, 2008.

 1. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2008
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa kwamba, Yussuf Manji, amechanganyikiwa kwa kula unga, huku baadhi ya watu wakidai kwamba amelogwa na Simba, wakati ndugu zake wakawa wanasema tokea jana alizidisha kubwia unga hadi akachanganyikiwa, na alipokwenda kupimwa Agakhan leo ndio akatoroka na kuendesha gari kwa fujo huku akitaka kugonga akaenda Gymkana Club. Pale club wahindi wenzake walipombembeleza akawa anawatimua hadi ndugu zake na watu wa Yanga, akiwamo Jamal Malinzi ndio wakafanikiwa kumuondoa.

  Habari ndio hiyo. Huyo ndiye mfadhili wa CCM na Swahiba wa JK na kundi lake
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  JF wakati mwingine mhhhhhhhh, haya bwana umesikika...teh teh teh teh teh
   
 3. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Duh! hii kali kama kweli...
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hata mimi nimesikia kutoka kwa watu wa Gymkana na watu wa Yanga, tena wote viongozi waandamizi wanaoheshimika. Si jambo jema la kufurahia lakini tuangalie haya madawa, sheria inasemaje?
   
 5. m

  mutua12 Member

  #5
  Oct 28, 2008
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe ni simba, mkubali bao acha lolongo bwana, lete uthibitisho
   
 6. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mh!!! Manji naye amekuwa teja??? Haya tunasubiri nondo za uhakika isije kuwa ni udaku tu kutoka kwa washindani wenzake katika ma-deal yao!!!
   
 7. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu, you have to know that money is not everything thats why do not get suprise that those who are said to be prosperous, their lives are a mess!
   
 8. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Ni kweli Ibra nakubaliana na wewe i'ts funny kwamba watu tunaenda mbio kukimbiza shilingii lakini wenye hizo shilingi za kutosha nao wanafanya mambo ya aibu mbele ya jamii kutokana na shilingi zao.....Sasa sijui lipi bora kuwa na pesa au kuwa nazo kidogo japo za kubadilisha mboga tu???
   
 9. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mkuu mimi naamini hivi (ni imani yangu binafsi) kwa binadamu sijui kama wengine watakubaliana, nazo ni :-
  1. There is a place for possession in our inner being that are to be filled with money
  2. There is a place in our inner being that are to be filled with a lover (spouse)
  3. There is a place in our inner being that are to be fille with a child (family)
  4. There is a place in our inner being that are to be filled with God only

  Ukipata ya 4 naamini nyingine hata zisipozibwa bado unaweza kuishi lakini ukipata hizo 3 bila ya 4, your life will be a mess!
   
 10. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mimi mtizamo wangu ni kuwa utajiri ni kama uwakili vile. Haimfai mwanasheria kutokusimama thabiti kuwatetea wale walio katika kuonewa. Laiti tungefahamu hili, basi hata Tanzania yetu usingekumbwa na ufisadi kiasi hiki.

  Uwakili wa fedha unakuwa hivi, uwe na magari mengi ili wapende wenzio,
  ujenge nyumba nyingi ili walale wenzio,
  uanzishe/ujenge shule nyingi, ili wasome watoto wa wenzio,
  ujenge hospitali nyingi ili watibiwe wenzio,
  ujenge barabara ili wapite wenzio,
  **bila kusahau kuchangia harusi ili wenzio wakafurahia na wake/waume zao.

  Sasa yote haya, waweza kujitendea mwenyewe kwa vile una fedha?, ukiwa na nyumba achilia mbali ukubwa wake, unalala chumba kimoja, ndani ya gari wakalia kiti kimoja n.k
  Je, yafaa kuwa milionea halafu ukaishi mwezini mwenyewe?

  Wanadamu tunapotea pale tunaposahau kuwa sisi ni mawala tu wa mali iliyomo humu duniani na wala sio wamiliki. Tungefahamu hili, tusingekimbizia fedha hata kama ya ufisadi huko Uswisi, uingereza n.k. Sasa tafakari, je wenye fedha wengi wanajichukulia kama mawakili tu?

  Watu wenye majina makubwa na ambao daima wanakumbukwa duniani, ni wale waliotimiza UWAKALA wao kadri walivyoweza, na wala sio wale waliokuwa mamilionea!!
   
 11. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,186
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  Mie nilidhani anauza tuu kumbe hata wenyewe anabwia! JK mu-add huyu jamaa kwenye ile list ya drug dealers!
   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,246
  Likes Received: 5,626
  Trophy Points: 280
  kwa nini asikamatwe aulizwe amepata wapi hizo dawa za kulevya hawa ndio wanowauzia watoto wetu madawa ya kulevya halafu pesa wanawamwagia yanga kujifisha
  haya jakaya habari ndio hiyo
   
 13. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,246
  Likes Received: 5,626
  Trophy Points: 280
  jk mwenye anabwia chuji akikorofishana na mama salama
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Date::10/28/2008
  Manji wa Yanga augua ghafla, akimbizwa hospitali
  Na Vicky Kimaro
  Mwananchi

  SIKU moja baada ya kuishuhudia Yanga ikiichapa Simba bao 1-0, mfadhili mkuu wa klabu hiyo, Yusuf Manji ameugua ghafla na kukimbizwa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam kwa matibabu.

  Mwenyekiti wa klabu hiyo, Imani Madega alisema jana jioni kuwa Manji alipatwa maradhi hayo juzi wakati akijitayarisha kwenda kazini, saa 3,00 asubuhi, lakini ghafla alianguka na kukimbizwa hospitali ambako alihudumiwa.

  "Unajua inawezekana ni furaha za ushindi na kuwa na shughuli nyingi, inawezekana kulimfanya apatwe na hali hiyo…inawezekana pia alikuwa na malaria ya muda mrefu na kutokana na kuwa hayo na pia ugumu wa mchezo ndipo ikaibuka.

  "Baada ya kufanyiwa vipimo Aga Khan, Madega alisema kuwa Manji aligundulika kuwa na malaria kali na uchovu, mwili ulikuwa umechoka kwa mawazo akapewa dawa na kumshauri apumzike nyumbani.

  "Lakini leo (jana), ghafla saa 11.00 alfajiri akatoka nyumbani bila ya kueleweka akielekea maeneo ya Viwanja vya Gymkhana, lakini walinzi wake walimfuata na kumrudisha tena hospitali," alisema Madega.

  Madega alisema hali ya mfadhili huyo inaendelea vizuri baada ya kuchomwa sindano ya kumtuliza.
  "Hali inaendelea vizuri na kuwataka wapenzi na mashabiki wa Yanga kutulia katika kipindi hiki ambacho mfadhili wao anasumbuliwa na homa. Najua yatazungumzwa mengi, lakini cha muhimu ni kutulia na kumuombea mfadhili wetu aendelee vema na matibabu," alisema Madega. Manji amekuwa akiifadhili Yanga kwa kipindi cha miaka miwili sasa.
   
 15. D

  Dungulee Member

  #15
  Oct 29, 2008
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 17
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kiranja unajua jana ilikua siku ya wahindi(DIWALI) hivyo inawezekana jamaa manji ikawa ndio style yake ya kujirusha.Ila nahisi karibu awe Teja sasa
   
 16. P

  PWIDA Member

  #16
  Oct 29, 2008
  Joined: Jun 20, 2007
  Messages: 53
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 25
  Asante sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!! Heri mtu akiyatenda hayo uliyoyasema. Uwakili huu ni muhimu kwa jamii.
   
 17. m

  mnyama Member

  #17
  Oct 29, 2008
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda ndo staili yake ya kukwepa Rungu la JK kwa mafisadi wa EPA. Au Rungu la EPA ndo limemchanganya hadi akabwia dozi kubwa ya ungwa.
   
 18. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2008
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wakati naweka hii habari hapa, watu waliibeza, nadhani JF tujifunze uvumilivu. Na tujue kuwa humu JF kuna watu wa kila aina na mara nyingi JF imekuwa ya kwanza
   
 19. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2008
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Niliambiwa kwamba amekwenda South Africa kwa matibabu, lakini katika system za Mwalimu Nyerere International Aiport, jina la Yusuf Mehboob Manji, aliyezaliwa Oktoba 14, 1975, mwenye pasi namba AB 052416 ya Tanzania, halijaonekana, labda kama kasafiri kwa ndege ya kukodi na pasi yake ya Marekani ama kimoja wapo. Patamu hapo.
   
 20. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2008
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu data zako ninazikubali!
   
Loading...