Manji aanza mkakati wa ujenzi wa uwanja yanga

Wewee Yanga hakuna Watindiga wewe,ulishawahi kuona Yanga imesajili kwa kuonyesha picha ya Mwenyekiti amemshika bega mchezaji tajwa msajiliwa halafu wakashangilia,umeshawahi kusikia katika mkutano wa Yanga taarifa ya mapato na matumizi ikasomwa kisanii na wana Yanga wakashangilia,umeshawahi kuona wana Yanga wamechangia rambirambi za mpendwa wao zikaliwa na Viongozi wao na wao wakakaa kimya,umeshawahi kuona Yanga imeuza wachezaji nje wana Yanga wasihoji fedha iliyopatikana imetumikaje badala yake wakazidi kukamuliwa kwa kuchangishwa kwenye mkutano mkuu....hivi unafahamu kuwa kupata taarifa ya mapato na matumizi hata kwa wewe mshabiki njaa wa huko madongo kuporomoka kwako unakoishi ni haki yako? halafu unajisifia kwa kuchangishwa,kama kuchangishwa pasipo kupata maelezo ya kina ya sababu za kuchangishwa au mapato yaliyopatika katika mwaka wa fedha uliotangulia yametumikaje ni ujanja basi mimi binafsi nitakuwa Mtindiga namba 1 kwani siwezi kukubali hata siku 1.

yaani hicho chote ulichoandika ndo kimedhihirisha namna gani ulivyo mtindiga tena aliyekomaa hadi anatoa unga...! Tena we hujui chochote kuhusu hata hiyo yanga yako. Ila kwa kukusaidia tu hebu kumbuka habari za Costa na Amri said ilikuwaje? Yanga haikuingia cha kike? huyo twite mwenyewe mbona mmekubali kurudisha pesa kama sio utindiga ni nini? Eti klabu kubwa ina wasomi lakini inakuja kuburuzwa na mzee Akilimali ambaye hata ukimpa The Guardian hajui kilichoandikwa kama sio utindiga nini? Timu yenye washabiki wa kuridhisha lakini wanaosubiri kulipiwa na kupewa kadi za bure na mwenyekiti kama sio utindiga ni nini..? Mkadanganywa kagere anakuja, mkasubiri u/taifa holaaa...! Kama sio utindiga nini..? Kama uwanja jengeni kwa kuwa ni kitu muhimu na cha maendeleo, na pia kitaleta changamoto kwa simba nao kuacha longolongo. Wasichotaka watu ni hizi kelele na tambo zisizo na maana. Isije ikawa kama msanii underground anayewadanganya rafk zake kila wakati anaenda kutoa single lakini wapi. Anaishia kuwaimbia kijiweni hadi anafulia. Chukueni hatua hatutaki stori.
 
Mifano yako katu hailingani.....Manji ni mwenyekiti Yanga halafu ni mbia at the same time.......Emirates ilijengwa kwa mkopo waliochukua Arsenal na wanalipwa na hilo shirika la ndege ada ya matumizi ya jina tu.......uwanja wetu wa taifa hutajua kamwe Wachina wananufaika vipi ila mimi najua........daraja la kigamboni ni suala la kibiashara zaidi kuliko michezo
hawa jamaa walivyofungwa Mbeya wakasema ni Kocha, wakaishia kumfukuza na viongozi wengine. Juzi mchezo wa Simba ilikuwa wafungwe na hawa watu walivyo wajinga (samahani sina neno lingine zaidi ya hilo) hawajasema lolote maana njaa zao zimepata mtu anayezijua. Jana Bukoba wamefungwa nipo hapa nangoja sababu watakayotoa ....ukweli ukibaki pale pale kuwa mpira wa timu hii sasa unaendeshwa kwenye media zaidi ya uwanjani!
Ninachotaka kujua ni kama watamfukuza huyo M/kiti wa sasa (ambayo ni ngumu) ambaye anataka kuwajengea huu uwanja na uwe mwisho wa hilo wazo.
Lakini kama hapo kwenye red, hilo wazo lingekuwa relevant endapo kungelikuwa na makubaliano rasmi ya mradi huu na sio ya "nipe uenyekiti nijenge ghorofa/uwanja".
Wajinga ndio waliwao kweli

Wahandisi walipewa kazi ya finishing na kufanya marekebisho yatokanayo na madhara ya dhambi katika ulimwengu huu. Hakuna kinachoshindikana panapo fedha. Kwa taarifa yako nenda kaone Naura Springs Hotel huko Arusha, imejengwa juu ya mto Naura hakuna mafuriko hata kama itakuja el-nino inayotajwa na watu wa hali ya hewa.

Usiwe na hofu na mafuriko labda kama kiroho kinakuuma kwamba usiowapenda sasa wanachanja mbuga kufikia maendeleo ya kweli badala ya maneno mengi ya yule mzee wa Mogadishu.
 
Kweli Mtani, hakuna kinachoshindikana panapo fedha..
1. Hivi yule Mhandisi ambae alisaini mkataba kuanza kazi ya ujenzi wa uwanja utakaobeba washabiki 40,000 na paking ya magari 1,000, kazi yake inaendeleaje?
2. Na vipi kuhusu ile safari yenu ya kuelekea mji wa "maendeleo ya kweli" mmefika, au bado mnachanja mbuga?
 
[h=2]Monday, September 24, 2012[/h][h=3]MANJI KUJENGA UWANJA WA KISASA JANGWANI, UTAKUWA BAAB KUBWA TANZANIA NZIMA HAKUNA[/h]

Uwanja mpya wa Kaunda utakavyokuwa

Na Mahmoud Zubeiry
KLABU ya Yanga ipo katika mkakati wa kujenga Uwanja mpya wa kisasa sambamba na kukarabati jengo la makao makuu ya klabu, liliopo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Habari ambazo, BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba tayari mkandarasi amekwishaptikana na amefikia makubaliano na uongozi wa klabu hiyo.
Habari zaidi zinasema, Uwanja mpya wa Kaunda utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 40,000 na eneo la maegesho ya magari yasiyopungua 1,000 na zoezi la ujenzi wa Uwanja huo, litaanza kabla ya tarahe ya mwisho ya mwaka huu.
Inadaiwa mradi huo, utafadhiliwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Mehboob Manji, ambaye amedhamiria kufanya mambo mengine makubwa, kubadilisha kabisa sura na hadhi ya klabu hiyo, ili viendane na klabu nyingine kubwa Afrika.

Wachezaji wakiwa mazoezini Uwanja wa Kaunda wa sasa
Manji amekuwa mfadhili wa Yanga tangu mwaka 2006, wakati klabu hiyo ikiwa chini ya Mwenyekiti, Francis Mponjoli Kifukwe na baada ya kuona jitihada zake za kuifanya Yanga iwe ya hadhi ya juu zinakwamishwa na viongozi, Julai 14, mwaka huu akaamua kujitosa kugombea Uenyekiti wa klabu hiyo, katika uchaguzi mdogo.
Ili kuhakikisha anapata timu nzuri ya kufanya nayo kazi, Manji aliwapigania Clement Sanga, Abdallah Bin Kleb, Mussa Katabaro, George Manyama na Lameck Nyambaya aingie nao madarakani.
Katika timu hiyo, iliyopewa jina ‘Jeshi la Miamvuli’ Sanga alifanikiwa kuwa Makamu Mwenyekiti, Bin Kleb, Manyama na Katabaro wakipata Ujumbe wa Kamati ya Utendaji, wakati Nyambaya alizidiwa kura na Aaron Nyanda.
Uwanja wa Kaunda na jengo la sasa la klabu, vilijengwa kwa nguvu za wanachama wake, chini ya Mwenyekiti wake wa kwanza, Mangara Tarbu miaka ya 1970 pamoja na msaada wa rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amaan Karume.
Ingawa historia inasema Yanga ilizaliwa mwaka 1935 na Simba mwaka 1936, lakini ukizama ndani utagundua kwamba, huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa utani na upinzani wa jadi, baina ya miamba hiyo ya soka nchini.
Kulikuwa kuna timu inaitwa New Youngs, ambayo mwaka 1938 ilisambaratika na baadhi ya wachezaji wake wakaenda kuunda timu iliyokuwa ikiitwa Sunderland, ambayo hivi sasa inajulikana kama Simba.
Kabla ya kutokea vurugu zilizoisambaratisha New Youngs, vijana wa Dar es Salaam walikuwa wana desturi ya kukutana viwanja vya Jangwani kufanya mazoezi na baada ya muda wakaamua kuunda timu yao, waliyoipachika jina Jangwani.

Unavyoonekana Uwanja wa Kaunda hivi sasa
Ndani ya kipindi kifupi tu, timu hiyo iliteka hisia za wengi, waliojitokeza kujiandikisha uanachama wa klabu hiyo. Miongoni mwa waliovutika na uanachama wa klabu hiyo ni Tarbu Mangara (sasa marehemu) na ilipofika mwaka 1926, walifanya mkutano wa kwanza katika eneo ambalo hivi kuna shule ya sekondari ya Tambaza.
Miongoni mwa yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni kuiboresha timu hiyo, ambayo wachezaji wake wengi walikuwa wafanyakazi wa Bandarini na mashabiki wake wengi walikuwa wabeba mizigo wa bandarini.

Hiki ndio choo cha Uwanjda wa Kaunda
Baada ya mkutano huo, timu hiyo ilibadilishwa jina na kuwa Navigation, iliyotokea kuwa moto wa kuotea mbali katika timu za Waafrika enzi hizo, kabla ya uhuru wa Tanganyika. Timu kama Kisutu, Kitumbini, Gerezani na Mtendeni zilikuwa hazifui dafu kwa wana Jangwani hao.
Ikiwa inatamba kwa jina la Navigation, wanachama wa timu hiyo walikuwa wakitembea kifua mbele na kuwatambia wapinzani, kwamba wao ndiyo zaidi. Kwa sababu katika kipindi hicho, Italia ilikuwa inatamba kwenye ulimwengu wa soka, wanachama wa timu hiyo nao waliamua kuibadilisha jina timu yao na kuiita Taliana.
Taliana ilipata mafanikio ya haraka na haikushangaza ilipopanda hadi Ligi Daraja la Pili Kanda ya Dar es Salaam, mwanzoni mwa miaka ya 1930. jina la Taliana waliamua kuachana nalo mapema, kabla ya kuingia kwenye ligi hiyo, hivyo wakaanza kujiita New Youngs.
Lakini kila ilipokuwa ikibadilisha jina, ilikuwa ikifanya vitu pia, kwani wakiwa na jina la New Youngs, waliweza kutwaa Kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali za Dar es Salaam.
Hatimaye ukawadia mwaka mbaya kwa New Youngs, 1938 wakati baadhi ya wachezaji walipojitoa na kwenda kuanzisha Sunderland. Kwa sababu hiyo, waliobaki wakaamua kubadili jina na kuwa Young Africans, jina ambalo mashabiki wake wengi walishindwa kulitamka vizuri hivyo kujikuta wakisema Yanga.
Miongoni mwa wachezaji wa mwanzoni kabisa wa Yanga ni kipa Taha Athumani, Saidia Msafiri na Jamil Ramadhan. Waliofuatia walikuwa ni kipa Abdulhamid Ramadhan, aliyewika na kuisaidia Tanganyika kutwaa Kombe la Gossage (sasa Challenge) katika miaka ya 1949 na 1950.

Hili ndio jukwaa la sasa la Uwanja Kaunda
Lakini mbali na jengo la makao makuu ya klabu na Uwanja wa Kaunda, Yanga pia ina nyumba Mtaa wa Mafia, ambayo kwa muda mrefu imetelekezwa, ingawa wanaweza kuikarabati kwa kujenga jengo la kisasa la kitegauchumi, katika Kariakoo mpya iliyosheheni maghorofa.

HUU NI KUZARA YANGA.MTU ANAKOJOLEA UKUTA
 
Kweli Mtani, hakuna kinachoshindikana panapo fedha..
1. Hivi yule Mhandisi ambae alisaini mkataba kuanza kazi ya ujenzi wa uwanja utakaobeba washabiki 40,000 na paking ya magari 1,000, kazi yake inaendeleaje?
2. Na vipi kuhusu ile safari yenu ya kuelekea mji wa "maendeleo ya kweli" mmefika, au bado mnachanja mbuga?
Ha ha ha mkuu umeifuukua hii mada atie?
 
Hii ilikua plani ya uwanja wa Yanga, kabla ya kujengwa, ni huu uwanja wao wa kisasa wanaoutumia hivi sasa, ambao hubeba mashabiki 40,000 na una pakingi yenye uwezo wa kubeba magari 10,000.
wp_ss_20160826_0001.png
 
[h=2]Monday, September 24, 2012[/h][h=3]MANJI KUJENGA UWANJA WA KISASA JANGWANI, UTAKUWA BAAB KUBWA TANZANIA NZIMA HAKUNA[/h]

Uwanja mpya wa Kaunda utakavyokuwa

Na Mahmoud Zubeiry
KLABU ya Yanga ipo katika mkakati wa kujenga Uwanja mpya wa kisasa sambamba na kukarabati jengo la makao makuu ya klabu, liliopo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Habari ambazo, BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba tayari mkandarasi amekwishaptikana na amefikia makubaliano na uongozi wa klabu hiyo.
Habari zaidi zinasema, Uwanja mpya wa Kaunda utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 40,000 na eneo la maegesho ya magari yasiyopungua 1,000 na zoezi la ujenzi wa Uwanja huo, litaanza kabla ya tarahe ya mwisho ya mwaka huu.
Inadaiwa mradi huo, utafadhiliwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Mehboob Manji, ambaye amedhamiria kufanya mambo mengine makubwa, kubadilisha kabisa sura na hadhi ya klabu hiyo, ili viendane na klabu nyingine kubwa Afrika.
Wachezaji wakiwa mazoezini Uwanja wa Kaunda wa sasa
Manji amekuwa mfadhili wa Yanga tangu mwaka 2006, wakati klabu hiyo ikiwa chini ya Mwenyekiti, Francis Mponjoli Kifukwe na baada ya kuona jitihada zake za kuifanya Yanga iwe ya hadhi ya juu zinakwamishwa na viongozi, Julai 14, mwaka huu akaamua kujitosa kugombea Uenyekiti wa klabu hiyo, katika uchaguzi mdogo.
Ili kuhakikisha anapata timu nzuri ya kufanya nayo kazi, Manji aliwapigania Clement Sanga, Abdallah Bin Kleb, Mussa Katabaro, George Manyama na Lameck Nyambaya aingie nao madarakani.
Katika timu hiyo, iliyopewa jina ‘Jeshi la Miamvuli’ Sanga alifanikiwa kuwa Makamu Mwenyekiti, Bin Kleb, Manyama na Katabaro wakipata Ujumbe wa Kamati ya Utendaji, wakati Nyambaya alizidiwa kura na Aaron Nyanda.
Uwanja wa Kaunda na jengo la sasa la klabu, vilijengwa kwa nguvu za wanachama wake, chini ya Mwenyekiti wake wa kwanza, Mangara Tarbu miaka ya 1970 pamoja na msaada wa rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amaan Karume.
Ingawa historia inasema Yanga ilizaliwa mwaka 1935 na Simba mwaka 1936, lakini ukizama ndani utagundua kwamba, huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa utani na upinzani wa jadi, baina ya miamba hiyo ya soka nchini.
Kulikuwa kuna timu inaitwa New Youngs, ambayo mwaka 1938 ilisambaratika na baadhi ya wachezaji wake wakaenda kuunda timu iliyokuwa ikiitwa Sunderland, ambayo hivi sasa inajulikana kama Simba.
Kabla ya kutokea vurugu zilizoisambaratisha New Youngs, vijana wa Dar es Salaam walikuwa wana desturi ya kukutana viwanja vya Jangwani kufanya mazoezi na baada ya muda wakaamua kuunda timu yao, waliyoipachika jina Jangwani.
Unavyoonekana Uwanja wa Kaunda hivi sasa
Ndani ya kipindi kifupi tu, timu hiyo iliteka hisia za wengi, waliojitokeza kujiandikisha uanachama wa klabu hiyo. Miongoni mwa waliovutika na uanachama wa klabu hiyo ni Tarbu Mangara (sasa marehemu) na ilipofika mwaka 1926, walifanya mkutano wa kwanza katika eneo ambalo hivi kuna shule ya sekondari ya Tambaza.
Miongoni mwa yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni kuiboresha timu hiyo, ambayo wachezaji wake wengi walikuwa wafanyakazi wa Bandarini na mashabiki wake wengi walikuwa wabeba mizigo wa bandarini.
Hiki ndio choo cha Uwanjda wa Kaunda
Baada ya mkutano huo, timu hiyo ilibadilishwa jina na kuwa Navigation, iliyotokea kuwa moto wa kuotea mbali katika timu za Waafrika enzi hizo, kabla ya uhuru wa Tanganyika. Timu kama Kisutu, Kitumbini, Gerezani na Mtendeni zilikuwa hazifui dafu kwa wana Jangwani hao.
Ikiwa inatamba kwa jina la Navigation, wanachama wa timu hiyo walikuwa wakitembea kifua mbele na kuwatambia wapinzani, kwamba wao ndiyo zaidi. Kwa sababu katika kipindi hicho, Italia ilikuwa inatamba kwenye ulimwengu wa soka, wanachama wa timu hiyo nao waliamua kuibadilisha jina timu yao na kuiita Taliana.
Taliana ilipata mafanikio ya haraka na haikushangaza ilipopanda hadi Ligi Daraja la Pili Kanda ya Dar es Salaam, mwanzoni mwa miaka ya 1930. jina la Taliana waliamua kuachana nalo mapema, kabla ya kuingia kwenye ligi hiyo, hivyo wakaanza kujiita New Youngs.
Lakini kila ilipokuwa ikibadilisha jina, ilikuwa ikifanya vitu pia, kwani wakiwa na jina la New Youngs, waliweza kutwaa Kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali za Dar es Salaam.
Hatimaye ukawadia mwaka mbaya kwa New Youngs, 1938 wakati baadhi ya wachezaji walipojitoa na kwenda kuanzisha Sunderland. Kwa sababu hiyo, waliobaki wakaamua kubadili jina na kuwa Young Africans, jina ambalo mashabiki wake wengi walishindwa kulitamka vizuri hivyo kujikuta wakisema Yanga.
Miongoni mwa wachezaji wa mwanzoni kabisa wa Yanga ni kipa Taha Athumani, Saidia Msafiri na Jamil Ramadhan. Waliofuatia walikuwa ni kipa Abdulhamid Ramadhan, aliyewika na kuisaidia Tanganyika kutwaa Kombe la Gossage (sasa Challenge) katika miaka ya 1949 na 1950.
Hili ndio jukwaa la sasa la Uwanja Kaunda
Lakini mbali na jengo la makao makuu ya klabu na Uwanja wa Kaunda, Yanga pia ina nyumba Mtaa wa Mafia, ambayo kwa muda mrefu imetelekezwa, ingawa wanaweza kuikarabati kwa kujenga jengo la kisasa la kitegauchumi, katika Kariakoo mpya iliyosheheni maghorofa.
Safi sana Manji , vitu vyako tumeona , mwezi decemba yanga kuchezea ligi kaunda .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom