Manji aanza mkakati wa ujenzi wa uwanja yanga

Duniani hakuna cha bure........subirini mtaona.....huyu jamaa kwenye masuala ya ardhi hajambo
Katika dunia ya leo hakuna mtu au taasisi inayoweza kufanya jambo kubwa la uwekezaji bila ya kupeana company,uliza uwanja wa fly emirates umejengwaje au nisikkupeleke mbali sana,uwanja wetu wa taifa umejengwa na serikali yetu pekee? NA WACHINA WAMEONDOKA BAADA YA UJENZI AU BADO WAPO?au draja la kigamboni aujui kama linajengwa na ppf? Acha uzamani ndugu
 
Katika dunia ya leo hakuna mtu au taasisi inayoweza kufanya jambo kubwa la uwekezaji bila ya kupeana company,uliza uwanja wa fly emirates umejengwaje au nisikkupeleke mbali sana,uwanja wetu wa taifa umejengwa na serikali yetu pekee? NA WACHINA WAMEONDOKA BAADA YA UJENZI AU BADO WAPO?au draja la kigamboni aujui kama linajengwa na ppf? Acha uzamani ndugu

Mifano yako katu hailingani.....Manji ni mwenyekiti Yanga halafu ni mbia at the same time.......Emirates ilijengwa kwa mkopo waliochukua Arsenal na wanalipwa na hilo shirika la ndege ada ya matumizi ya jina tu.......uwanja wetu wa taifa hutajua kamwe Wachina wananufaika vipi ila mimi najua........daraja la kigamboni ni suala la kibiashara zaidi kuliko michezo
 
Hapo kwenye red labda neno sahihi ulilotaka kumaanisha ni "Watindiga" ngoja nikuulize....unafikiri Yanga kuna Watindiga kama Simba?
usilete mambo ya ushabiki bali kuwa serious kama wale wazee wa awali (sijui Tabu Mangala and the like) walioweza kumobilise wanachama na kuweza kujenga majengo ya clubs bila tamaa na sio hawa wa sasa wakiongozwa na vijana akina Bakili walioamua kumkabidhi kila kitu mtu ambaye hata 'mafisadi' walimtilia mashaka kwenye nomination ya uwakilishi jimbo la Kigamboni!
Cha kusikitisha zaidi, hao akina Mangala hawakuwa na aina ya mapenzi ya kushikiana hata mapanga lakini hawa wa sasa wanaweza hata kukuua eti kwa upenzi wao kwa timu.
Mimi ni mwananchama mfu wa Yanga, je nyie wanachama hai wa Yanga mtachangia shilingi ngapi katika huo mradi?

 
Kwani huo uwanja wenu wa huko bush utakuwa wa nani kama si wa mzee wa Mogadishu? Hakika nyani haoni kundule huona la mwenzake! Acheni Manji afanye vitu vyake ambavyo MahaRage haviwezi.
ili kupata hela za cement kwa kuanzia amemfukuza kocha na afsa habari mshanunuliwa ninyi,ila najua tarehe tatu ndio mwisho wa manji kuwepo pale jangwani.
 
usilete mambo ya ushabiki bali kuwa serious kama wale wazee wa awali (sijui Tabu Mangala and the like) walioweza kumobilise wanachama na kuweza kujenga majengo ya clubs bila tamaa na sio hawa wa sasa wakiongozwa na vijana akina Bakili walioamua kumkabidhi kila kitu mtu ambaye hata 'mafisadi' walimtilia mashaka kwenye nomination ya uwakilishi jimbo la Kigamboni!
Cha kusikitisha zaidi, hao akina Mangala hawakuwa na aina ya mapenzi ya kushikiana hata mapanga lakini hawa wa sasa wanaweza hata kukuua eti kwa upenzi wao kwa timu.
Mimi ni mwananchama mfu wa Yanga, je nyie wanachama hai wa Yanga mtachangia shilingi ngapi katika huo mradi?

kuna tofauti kubwa ya shabiki,mwqanachama,na mpenzi mara nyingi shabiki huwa hana akili na wengi ndio waliojaa simba na yanga.
 
Yanga itakuwa kama timu za ulaya. Haiwezekani bwana azam ina uwanja halafu timu kongwe zina uchochoro.
 
Kwa aliyekuwa analinganisha na Arsenal.......


Financing for the project proved difficult as Arsenal was not granted any public subsidy by the government. The club therefore sought other ways to generate income, namely by adopting a policy of buying football players for a low transfer fee and selling high as well as agreeing sponsorship deals. Arsenal recouped over £50 million from transfers involving Nicolas Anelka to Real Madrid and Marc Overmars, in a joint deal with Emmanuel Petit to Barcelona. The transfer of Anelka in particular helped fund the club's new training ground, Shenley Training Centre in London Colney, which opened in October 1999.

In Sepptember 2000, Granada Media Group purchased a five-percent stake in Arsenal at a price of £47 million. As part of the acquisition, Granada became the premier media agent for the football club, handling advertising, sponsorship, merchandising, publishing and licensing agreements. The company furthermore invested £20 million in a joint venture, AFC Broadband, to exploit the club's internet viewership. Arsenal chairman Peter Hill-Wood said of the deal: "This partnership will assist us in meeting Arsenal's two strategic objectives. First, to build a world-class team and a new stadium with an increased capacity so that more of our fans can enjoy watching the team. Secondly, to develop the Arsenal brand on a global basis by extending our fanbase around the world." Managing Director Keith Edelman added that the investment would be used directly to fund for the new stadium. The collapse of ITV Digital – part-owned by Granada – in April 2002 coincided with company being tied in to pay £30 million once arrangements for the new stadium were finalised.


The Emirates Stadium sign
After announcing pre-tax loss of £22.3m for the financial year 2001–02, the club formulated plans to reduce their wage bills in order to continue with the stadium work. Investment bank NM Rothschild and Sons was appointed to examine the financial situation at the club and advise whether it was feasible for Arsenal to move on with construction at the end of March 2003. Although Arsenal secured a £260 million loan from a group of banks led by the Royal Bank of Scotland in April 2003, the club suspended work on Ashburton Grove citing in a statement, "We have experienced a number of delays in arrangements for our new stadium project in recent months across a range of issues. The impact of these delays is that we will now be unable to deliver a stadium opening for the start of the 2005–06 season." The cost of building the stadium, forecasted at £400 million, had risen by a £100 million during that period. To combat the financial difficulties, Arsenal throughout the summer of 2003 gave fans the opportunity to register their interest in a relaunched bond scheme via the club website. The club planned to issue 3,000 bonds for between £3,500 and £5,000 each for a season ticket at Highbury, then at Ashburton Grove. Arsenal supporters reacted with surprise to the reintroduction of the bond scheme with AISA chairman Steven Powell adding: "We are disappointed that the club has not consulted supporters before announcing a new bond scheme." Though they never stated how many bonds were sold, Arsenal did raise several million pounds through the scheme.

Sportswear provider Nike signed a contract extension with Arsenal in August 2003 to remain as the club's official kit supplier. This was presented as a solution to the stadium financing; in addition to paying £55 million over seven years, Nike paid a minimum of £1 million each year as a royalty fee, dependant on sales. On 23 February 2004, Arsenal Holdings plc – the club's parent company announced that funding for the stadium was now secured with construction work being able to resume. Wenger said of the announcement: "It has been a big target of mine to participate in pushing the club forward and relocating to a new stadium is a necessity as it will enable us to become of one the biggest clubs in the world." Interest on the £260 million debt was set at a commercial fixed rate over a 14-year period. To refinance the cost, the club planned to convert the money into a 30-year bond financed by banks. The proposed bond issue went ahead on 13 July 2006. Arsenal issued £210 million worth of 13.5-year bonds with a spread of 52 basis points over government bonds and £50 million of 7.1-year bonds with a spread of 22 basis points over LIBOR. It was the first publicly marketed, asset-backed bond issue by a European football club.The effective interest rate on these bonds is 5.14% and 5.97%, respectively, and are due to be paid back over a 25-year period; the move to bonds has reduced the club's annual debt service cost to approximately £20 million a year. In September 2010, Arsenal announced that the Highbury Square development – one of the main sources of income to reduce the stadium debt – was now debt free and making revenue.


On 5 October 2004, Emirates Airline signed a 15-year contract with Arsenal estimated at £100 million. Under the deal, the group secured naming rights to the stadium and shirt sponsorship when the club's deal with O2 expired at the end of the 2005–06 season. The stadium name is often colloquially shortened from "Emirates Stadium" to "The Emirates", although some supporters continue to use the former name "Ashburton Grove" or even "The Grove" for the new stadium, especially those who object to the concept of corporate sponsorship of stadium names. Due to UEFA regulations on stadium sponsors, during European matches the stadium is not officially referred to as Emirates Stadium, as Emirates are not an official sponsor of the Champions League competition; other stadia, such as the Allianz Arena in Munich, have fallen foul of this rule before. UEFA refer to the stadium as Arsenal Stadium, which was the official name of the stadium at Highbury.
 
Yanga itakuwa kama timu za ulaya. Haiwezekani bwana azam ina uwanja halafu timu kongwe zina uchochoro.
angalia 'usiingie' chaka mkuu E GAGNANT.
Timu ina departments na sections tofauti mfano wachezaji, utawala, wapenzi, wanachama, mashabiki nk. Uelewa na ustaarabu wa hawa watu ndio unapelekea ukubwa wa timu, angalau nusu ya hawa wadau wawe na uelewa wa wanachokifanya. Hapa bongo kila unayemuona anashughulika katika milolongo huu ni njaa tu. Bora hao wazee wa enzi hizo unaweza kusema njaa walikuwa nazo lakini kwao maadili na uaminifu kilikuwa kigezo kikubwa na ndio wakaweza kufanya waliyoyafanya.
Ukiangalia sehemu ya timu kama Yanga na jinsi huyu kocha alivyoacha kazi, wachezaji kama Asamoah, Mwape unaona wazi kuwa visionza wadu hawa ziko very low na usitegemee makuu hapo!

 
angalia 'usiingie' chaka mkuu E GAGNANT.
Timu ina departments na sections tofauti mfano wachezaji, utawala, wapenzi, wanachama, mashabiki nk. Uelewa na ustaarabu wa hawa watu ndio unapelekea ukubwa wa timu, angalau nusu ya hawa wadau wawe na uelewa wa wanachokifanya. Hapa bongo kila unayemuona anashughulika katika milolongo huu ni njaa tu. Bora hao wazee wa enzi hizo unaweza kusema njaa walikuwa nazo lakini kwao maadili na uaminifu kilikuwa kigezo kikubwa na ndio wakaweza kufanya waliyoyafanya.
Ukiangalia sehemu ya timu kama Yanga na jinsi huyu kocha alivyoacha kazi, wachezaji kama Asamoah, Mwape unaona wazi kuwa visionza wadu hawa ziko very low na usitegemee makuu hapo!


Mkuu umenena vyema. Kama sungura hana mkia hata digidigi pia hana mkia; hebu tazama jinsi kocha Moses Basena alivyoondolewa pale Msongamanoni na pia angalia jinsi marehemu Mafisango alivyozikwa na jamaa wa pale pale Msongamanoni! Nadhani wenye akili zao wameshanielewa.
 











Uwanja mpya wa Kaunda utakavyokuwa



Na Mahmoud Zubeiry


KLABU ya Yanga ipo katika mkakati wa kujenga Uwanja mpya wa kisasa sambamba na kukarabati jengo la makao makuu ya klabu, liliopo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.

Habari ambazo, BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba tayari mkandarasi amekwishaptikana na amefikia makubaliano na uongozi wa klabu hiyo.


Habari zaidi zinasema, Uwanja mpya wa Kaunda utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 40,000 na eneo la maegesho ya magari yasiyopungua 1,000 na zoezi la ujenzi wa Uwanja huo, litaanza kabla ya tarahe ya mwisho ya mwaka huu.


Inadaiwa mradi huo, utafadhiliwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Mehboob Manji, ambaye amedhamiria kufanya mambo mengine makubwa, kubadilisha kabisa sura na hadhi ya klabu hiyo, ili viendane na klabu nyingine kubwa Afrika.



Wachezaji wakiwa mazoezini Uwanja wa Kaunda wa sasa
Manji amekuwa mfadhili wa Yanga tangu mwaka 2006, wakati klabu hiyo ikiwa chini ya Mwenyekiti, Francis Mponjoli Kifukwe na baada ya kuona jitihada zake za kuifanya Yanga iwe ya hadhi ya juu zinakwamishwa na viongozi, Julai 14, mwaka huu akaamua kujitosa kugombea Uenyekiti wa klabu hiyo, katika uchaguzi mdogo.

Ili kuhakikisha anapata timu nzuri ya kufanya nayo kazi, Manji aliwapigania Clement Sanga, Abdallah Bin Kleb, Mussa Katabaro, George Manyama na Lameck Nyambaya aingie nao madarakani.


Katika timu hiyo, iliyopewa jina ‘Jeshi la Miamvuli’ Sanga alifanikiwa kuwa Makamu Mwenyekiti, Bin Kleb, Manyama na Katabaro wakipata Ujumbe wa Kamati ya Utendaji, wakati Nyambaya alizidiwa kura na Aaron Nyanda.


Uwanja wa Kaunda na jengo la sasa la klabu, vilijengwa kwa nguvu za wanachama wake, chini ya Mwenyekiti wake wa kwanza, Mangara Tarbu miaka ya 1970 pamoja na msaada wa rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amaan Karume.


Ingawa historia inasema Yanga ilizaliwa mwaka 1935 na Simba mwaka 1936, lakini ukizama ndani utagundua kwamba, huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa utani na upinzani wa jadi, baina ya miamba hiyo ya soka nchini.

Kulikuwa kuna timu inaitwa New Youngs, ambayo mwaka 1938 ilisambaratika na baadhi ya wachezaji wake wakaenda kuunda timu iliyokuwa ikiitwa Sunderland, ambayo hivi sasa inajulikana kama Simba.


Kabla ya kutokea vurugu zilizoisambaratisha New Youngs, vijana wa Dar es Salaam walikuwa wana desturi ya kukutana viwanja vya Jangwani kufanya mazoezi na baada ya muda wakaamua kuunda timu yao, waliyoipachika jina Jangwani.



Unavyoonekana Uwanja wa Kaunda hivi sasa
Ndani ya kipindi kifupi tu, timu hiyo iliteka hisia za wengi, waliojitokeza kujiandikisha uanachama wa klabu hiyo. Miongoni mwa waliovutika na uanachama wa klabu hiyo ni Tarbu Mangara (sasa marehemu) na ilipofika mwaka 1926, walifanya mkutano wa kwanza katika eneo ambalo hivi kuna shule ya sekondari ya Tambaza.


Miongoni mwa yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni kuiboresha timu hiyo, ambayo wachezaji wake wengi walikuwa wafanyakazi wa Bandarini na mashabiki wake wengi walikuwa wabeba mizigo wa bandarini.



Hiki ndio choo cha Uwanjda wa Kaunda
Baada ya mkutano huo, timu hiyo ilibadilishwa jina na kuwa Navigation, iliyotokea kuwa moto wa kuotea mbali katika timu za Waafrika enzi hizo, kabla ya uhuru wa Tanganyika. Timu kama Kisutu, Kitumbini, Gerezani na Mtendeni zilikuwa hazifui dafu kwa wana Jangwani hao.

Ikiwa inatamba kwa jina la Navigation, wanachama wa timu hiyo walikuwa wakitembea kifua mbele na kuwatambia wapinzani, kwamba wao ndiyo zaidi. Kwa sababu katika kipindi hicho, Italia ilikuwa inatamba kwenye ulimwengu wa soka, wanachama wa timu hiyo nao waliamua kuibadilisha jina timu yao na kuiita Taliana.


Taliana ilipata mafanikio ya haraka na haikushangaza ilipopanda hadi Ligi Daraja la Pili Kanda ya Dar es Salaam, mwanzoni mwa miaka ya 1930. jina la Taliana waliamua kuachana nalo mapema, kabla ya kuingia kwenye ligi hiyo, hivyo wakaanza kujiita New Youngs.

Lakini kila ilipokuwa ikibadilisha jina, ilikuwa ikifanya vitu pia, kwani wakiwa na jina la New Youngs, waliweza kutwaa Kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali za Dar es Salaam.


Hatimaye ukawadia mwaka mbaya kwa New Youngs, 1938 wakati baadhi ya wachezaji walipojitoa na kwenda kuanzisha Sunderland. Kwa sababu hiyo, waliobaki wakaamua kubadili jina na kuwa Young Africans, jina ambalo mashabiki wake wengi walishindwa kulitamka vizuri hivyo kujikuta wakisema Yanga.

Miongoni mwa wachezaji wa mwanzoni kabisa wa Yanga ni kipa Taha Athumani, Saidia Msafiri na Jamil Ramadhan.

Waliofuatia walikuwa ni kipa Abdulhamid Ramadhan, aliyewika na kuisaidia Tanganyika kutwaa Kombe la Gossage (sasa Challenge) katika miaka ya 1949 na 1950.



Hili ndio jukwaa la sasa la Uwanja Kaunda
Lakini mbali na jengo la makao makuu ya klabu na Uwanja wa Kaunda, Yanga pia ina nyumba Mtaa wa Mafia, ambayo kwa muda mrefu imetelekezwa, ingawa wanaweza kuikarabati kwa kujenga jengo la kisasa la kitegauchumi, katika Kariakoo mpya iliyosheheni maghorofa. Mahelezo na picha kwa hisani ya (Ben Zubeiry)
 

Kutakuwa hakua Shades kwa Watazamaji? Sasa Mvua ikinyesha itakuwaje? Kwahiyo hautakuwa Uwanja wa Kisasa
 
Yanga hawana eneo la kujenga uwanja wa ukubwa huo. Habari za kufikirika tu, uongo mkubwa sana. Tupatieni na fikira za simba nao tuona ndoto feki zao kama jangwani.
 
Ni aibu kwa klabu kama simba na yanga kutegemewa kujengewa viwanja na mtu kwanini wanashindwa kutumia rasilikali watu walizonazo wakati tunaona timu kubwa za ulaya zikiangaika kwenda asia kutafuta masoko na mashabiki si tumebaki kujikomba kwa matajiri ambao wengi wao wana ajenda za siri kumbuka hata hayo majengo yalijengwa na wazee ambao hawakusoma na hawakuwa na pesa kama walionao wanachama na viongozi wa sasa hivi.
 
kumbe Manji ndiye anayejenga Uwanja, mi nilifikiri ni Club kama Club; kwa hiyo Manji huo uwanja ukiisha atakuwa anawakodisha auuu???????.ninachojua ni kwamba akaunti ya Yanga salio ni sufuri, mchango wa Club ni upi??? kazi kwelikweli..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom