Manji aanza mkakati wa ujenzi wa uwanja yanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manji aanza mkakati wa ujenzi wa uwanja yanga

Discussion in 'Sports' started by KIM KARDASH, Sep 24, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [h=2]Monday, September 24, 2012[/h][h=3]MANJI KUJENGA UWANJA WA KISASA JANGWANI, UTAKUWA BAAB KUBWA TANZANIA NZIMA HAKUNA[/h]

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Uwanja mpya wa Kaunda utakavyokuwa[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Na Mahmoud Zubeiry
  KLABU ya Yanga ipo katika mkakati wa kujenga Uwanja mpya wa kisasa sambamba na kukarabati jengo la makao makuu ya klabu, liliopo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
  Habari ambazo, BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba tayari mkandarasi amekwishaptikana na amefikia makubaliano na uongozi wa klabu hiyo.
  Habari zaidi zinasema, Uwanja mpya wa Kaunda utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 40,000 na eneo la maegesho ya magari yasiyopungua 1,000 na zoezi la ujenzi wa Uwanja huo, litaanza kabla ya tarahe ya mwisho ya mwaka huu.
  Inadaiwa mradi huo, utafadhiliwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Mehboob Manji, ambaye amedhamiria kufanya mambo mengine makubwa, kubadilisha kabisa sura na hadhi ya klabu hiyo, ili viendane na klabu nyingine kubwa Afrika.
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Wachezaji wakiwa mazoezini Uwanja wa Kaunda wa sasa[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Manji amekuwa mfadhili wa Yanga tangu mwaka 2006, wakati klabu hiyo ikiwa chini ya Mwenyekiti, Francis Mponjoli Kifukwe na baada ya kuona jitihada zake za kuifanya Yanga iwe ya hadhi ya juu zinakwamishwa na viongozi, Julai 14, mwaka huu akaamua kujitosa kugombea Uenyekiti wa klabu hiyo, katika uchaguzi mdogo.
  Ili kuhakikisha anapata timu nzuri ya kufanya nayo kazi, Manji aliwapigania Clement Sanga, Abdallah Bin Kleb, Mussa Katabaro, George Manyama na Lameck Nyambaya aingie nao madarakani.
  Katika timu hiyo, iliyopewa jina ‘Jeshi la Miamvuli’ Sanga alifanikiwa kuwa Makamu Mwenyekiti, Bin Kleb, Manyama na Katabaro wakipata Ujumbe wa Kamati ya Utendaji, wakati Nyambaya alizidiwa kura na Aaron Nyanda.
  Uwanja wa Kaunda na jengo la sasa la klabu, vilijengwa kwa nguvu za wanachama wake, chini ya Mwenyekiti wake wa kwanza, Mangara Tarbu miaka ya 1970 pamoja na msaada wa rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amaan Karume.
  Ingawa historia inasema Yanga ilizaliwa mwaka 1935 na Simba mwaka 1936, lakini ukizama ndani utagundua kwamba, huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa utani na upinzani wa jadi, baina ya miamba hiyo ya soka nchini.
  Kulikuwa kuna timu inaitwa New Youngs, ambayo mwaka 1938 ilisambaratika na baadhi ya wachezaji wake wakaenda kuunda timu iliyokuwa ikiitwa Sunderland, ambayo hivi sasa inajulikana kama Simba.
  Kabla ya kutokea vurugu zilizoisambaratisha New Youngs, vijana wa Dar es Salaam walikuwa wana desturi ya kukutana viwanja vya Jangwani kufanya mazoezi na baada ya muda wakaamua kuunda timu yao, waliyoipachika jina Jangwani.
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Unavyoonekana Uwanja wa Kaunda hivi sasa[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Ndani ya kipindi kifupi tu, timu hiyo iliteka hisia za wengi, waliojitokeza kujiandikisha uanachama wa klabu hiyo. Miongoni mwa waliovutika na uanachama wa klabu hiyo ni Tarbu Mangara (sasa marehemu) na ilipofika mwaka 1926, walifanya mkutano wa kwanza katika eneo ambalo hivi kuna shule ya sekondari ya Tambaza.
  Miongoni mwa yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni kuiboresha timu hiyo, ambayo wachezaji wake wengi walikuwa wafanyakazi wa Bandarini na mashabiki wake wengi walikuwa wabeba mizigo wa bandarini.
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Hiki ndio choo cha Uwanjda wa Kaunda [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Baada ya mkutano huo, timu hiyo ilibadilishwa jina na kuwa Navigation, iliyotokea kuwa moto wa kuotea mbali katika timu za Waafrika enzi hizo, kabla ya uhuru wa Tanganyika. Timu kama Kisutu, Kitumbini, Gerezani na Mtendeni zilikuwa hazifui dafu kwa wana Jangwani hao.
  Ikiwa inatamba kwa jina la Navigation, wanachama wa timu hiyo walikuwa wakitembea kifua mbele na kuwatambia wapinzani, kwamba wao ndiyo zaidi. Kwa sababu katika kipindi hicho, Italia ilikuwa inatamba kwenye ulimwengu wa soka, wanachama wa timu hiyo nao waliamua kuibadilisha jina timu yao na kuiita Taliana.
  Taliana ilipata mafanikio ya haraka na haikushangaza ilipopanda hadi Ligi Daraja la Pili Kanda ya Dar es Salaam, mwanzoni mwa miaka ya 1930. jina la Taliana waliamua kuachana nalo mapema, kabla ya kuingia kwenye ligi hiyo, hivyo wakaanza kujiita New Youngs.
  Lakini kila ilipokuwa ikibadilisha jina, ilikuwa ikifanya vitu pia, kwani wakiwa na jina la New Youngs, waliweza kutwaa Kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali za Dar es Salaam.
  Hatimaye ukawadia mwaka mbaya kwa New Youngs, 1938 wakati baadhi ya wachezaji walipojitoa na kwenda kuanzisha Sunderland. Kwa sababu hiyo, waliobaki wakaamua kubadili jina na kuwa Young Africans, jina ambalo mashabiki wake wengi walishindwa kulitamka vizuri hivyo kujikuta wakisema Yanga.
  Miongoni mwa wachezaji wa mwanzoni kabisa wa Yanga ni kipa Taha Athumani, Saidia Msafiri na Jamil Ramadhan. Waliofuatia walikuwa ni kipa Abdulhamid Ramadhan, aliyewika na kuisaidia Tanganyika kutwaa Kombe la Gossage (sasa Challenge) katika miaka ya 1949 na 1950.
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Hili ndio jukwaa la sasa la Uwanja Kaunda[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Lakini mbali na jengo la makao makuu ya klabu na Uwanja wa Kaunda, Yanga pia ina nyumba Mtaa wa Mafia, ambayo kwa muda mrefu imetelekezwa, ingawa wanaweza kuikarabati kwa kujenga jengo la kisasa la kitegauchumi, katika Kariakoo mpya iliyosheheni maghorofa.
   
 2. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kila la kheri!
  Angalieni isije kuwa kama suala la kocha Tom Saintfiet ambaye alipokelewa kwa mbwembwe na mikakati mikubwa lakini utekelezaji umeishia almost zero!
  Kubalianeni na Lowassa kwa kutoa kwanza elimu then ustaarabu ukishaingia mioyoni mwa watu nio mlete vitu kama huo uwanja!
   
 3. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu hata huchuji, mambo mengine kama ya huyu Shabiki wa Simba aliyekuja kutuchafulia mazingira ya Club yetu ulitakiwa kuyachunia tu, anyway lengo wanatakiwa wapate ujumbe kuwa hivi ndivyo mikakati ya maendeleo inavyopangwa siyo kila siku mnaambiwa kutajengwa uwanja Bunju na tayari Waturuki wameshaingia mkataba wa kufanya kazi hiyo hata mchoro wa namna kitakavyokuwa hakuna,chezea MahaRage nyinyi...mkija kushtuka mmeshachelewa Jamaa atakuwa ameshajijengea msingi wa maisha yake binafsi na ya ukoo wake mzima kule Mogadishu
   
 4. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  'Utanitambuaje kama nimeokoka? , ..., tazama matendo' (Bonny Mwaitege).
   
 5. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,544
  Likes Received: 10,475
  Trophy Points: 280
  Inawezekana!!
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  vitendo zaidi na si maneno kwenye magazeti tuu
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Duniani hakuna cha bure........subirini mtaona.....huyu jamaa kwenye masuala ya ardhi hajambo
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  All the best!
   
 9. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  umeleta hoja ya msingui mkuu.
  Kama unalijua lile jengo la 'aitel' pale Morocco ni mali ya umma lakini huyu bwana nasikia alitumia kiwanja kile kama dhamana na kupata mikopo benki then akalijenga na 'anakamua' mpaka pesa zake zikiisha. Niliwahi kusikia Umoja wa Wazazi(?) wakilalamika na kusema wanaona hata aibu kusema wanachopata pale kwa jinsi kilivyo kidogo.
  Pia angalia lile jengo la Quality Plaza, yale ya Ubungo vyote ni Utata Mtupu.
  Uzuri wa huyu 'mwenyekiti' wanaomjua wanasema ni mjasiriamali mzuri sana na hard worker lakini akikutana na 'manunda' anajua sana kuyalalia haswa!

  Sasa, huu uwanja utakuwa wa Yanga au Mwenyekiti!!?

   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Tatizo watani wetu ni ubishi.....hata asome vipi akishakuwa mwana Yanga humpindui.......majuzi nimebishana na mmoja wao tena lawyer mzoefu lakini wapi....kwake yeye Manji ni kama Yesu
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  kila la keri ila mafuriko yakija mtapona??au mnanjijengea tu
   
 12. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye red labda neno sahihi ulilotaka kumaanisha ni "Watindiga" ngoja nikuulize....unafikiri Yanga kuna Watindiga kama Simba?
   
 13. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,732
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Poleni wanasimba roho inauma eee, manji gogogogogoooo,.
   
 14. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Kwani huo uwanja wenu wa huko bush utakuwa wa nani kama si wa mzee wa Mogadishu? Hakika nyani haoni kundule huona la mwenzake! Acheni Manji afanye vitu vyake ambavyo MahaRage haviwezi.
   
 15. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Wahandisi walipewa kazi ya finishing na kufanya marekebisho yatokanayo na madhara ya dhambi katika ulimwengu huu. Hakuna kinachoshindikana panapo fedha. Kwa taarifa yako nenda kaone Naura Springs Hotel huko Arusha, imejengwa juu ya mto Naura hakuna mafuriko hata kama itakuja el-nino inayotajwa na watu wa hali ya hewa.

  Usiwe na hofu na mafuriko labda kama kiroho kinakuuma kwamba usiowapenda sasa wanachanja mbuga kufikia maendeleo ya kweli badala ya maneno mengi ya yule mzee wa Mogadishu.
   
 16. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Huyu jamaa alifungulia bomba au aliminya chupa ya maji? Hiyo jet mbona kubwa sana ikilinganishwa na kitundu cha sehemu hiyo? Kama ndivyo alivyo kwa kweli akifika kileleni ndani ya mtu bila shaka mtu huyo atakuwa kama amevunjikiwa yai la kuku wa kisasa.

  Kwa hiyo jezi yake, anajitambulisha kuwa ni shabiki wa upande wa pale msongamanoni.
   
 17. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,363
  Likes Received: 6,701
  Trophy Points: 280
  ha ha ha ha!!hawa simba wana visa sana kiongozi!!!
   
 18. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  hata liverpool walichora na ku-share hiyo michor kwenye mitandao but nothing happened

  pipe dream
   
 19. Tisha-TOTO

  Tisha-TOTO JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2012
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 1,173
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Mimi ni Yanga lakini I hate media hypes kama hizi. This is fnckiug rubbish!

  Kwani mkiwa modest na kupanga mipango yenu kimya kimya haiwezekani bana??!!

  Sasa ninyi freaking media crowd mnataka nini sasa.....a well learned and a smart cookie like Manji naye aanze kuonekana ana akili nyanya kama Rage?
   
 20. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  Mkumbuke hizi habari zimevuja wla hazijatolewa rasmi bado.Ingekuwa kwa rage angikuwa ameitisha press confrerece zamaaaaai! Kwa manji (yanga)tutakapo ita waandishi kuwaelezarasmi ujue kazi inaa nza keshoyake
   
Loading...