Manispaaa wekeni lami njia ya makaburi ya Ununio tusifukue makaburi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,914
22,060
Kwa ambaye ameenda Aprili akienda leo atashangaa makaburi ya Ununio yalivyoongezeka mji umepanu Kinondoni inasubiri sana yamepangika kwa heshima ukiwaza sana unaweza omba ubakie huko

Kuna njia ya kuingilia makaburini opposite na Kanisa la Lutherani tunaomba Manispaa wekeni lami ile njia imeshatengenezwa kisanii sana mvua ikija unamuona yuleyule anajazia kifusi

Tuheshimu hii sehemu please, ndio mji mwema mpya wa maisha ya watu aka makao ya milele hata kama hawapo tuwape heshima jamani kuanzia wanapoingilia.
 
Sehemu hiyo ndio makaburi ya waanzilishi wa kijiji cha Ununio na ya Wamashomvi ambao ndio wenyeji asili wa Dar es Salaam
Kuna historia kubwa ya waliomo humo sawa na kwenye magofu ya Kaole na Kilwa
 
Nafikiri mleta mada unamaanisha makaburi ya kondo ambayo yapo karibu na ununio.

Hiyo njia yakuingia kwenda makaburini ipo opposite na kanisa katoliki na sio Lutheran Makaburi ya ununio yapo barabarani kabisa karibia na njia ya kwenda ununio beach.
 
Sehemu hiyo ndio makaburi ya waanzilishi wa kijiji cha Ununio na ya Wamashomvi ambao ndio wenyeji asili wa Dar es Salaam
Kuna historia kubwa ya waliomo humo sawa na kwenye magofu ya Kaole na Kilwa
Kina Hela, Shilingi, Chambuso na wengineo. Namkumbuka marehemu Mzee Mfungeni. Mungu awarehemu wote waliotangulia mbele za haki.
 
Mkuu Pdidy, nafikiri leo umeeleweka vilivyo, maana hakuna aliyetoa kasoro kuhusu uandishi...
 
Back
Top Bottom