Manispaa ya Sumbawanga walipeni fidia mliowachukuliwa mashamba yao, acheni kuwalazimisha wamiliki wa viwanja ndio wawalipe fidia

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,578
2,000
Hakika inashangaza Sana kwa UONGOZI wa MANISPAA ya SUMBAWANGA ambayo Mwaka 2004 iliyatwaa MASHAMBA ya Wananchi Eneo la KIZWITE na Kulipima VIWANJA na KUVIUZA.

Kabla ya KUVIPIMA Manispaa iliwafanyia UTHAMINI wenye MASHAMBA na KUWALIPA FIDIA na OFISI ya MKUU wa WILAYA ilihusishwa.

Baada ya hapo VIWANJA vilitangazwa KUUZWA na Watu Walivinunua na KUMILIKISHAWA KWA HATI MILKI za Miaka 66.

Kinachosangaza Kuna WIMBI la WATU WANAVAMIA Viwanja hivyo ambavyo Vina WAMILIKI Halali na Kudai BABA zao ambao Eti ni MAREHEMU hawakulipwa FIDIA.Badala ya MAAFISA Ardhi wa MANISPAA kujiridhisha kwa Kuangalia MAJEDWALI
Yaliyotumika Kuwalipa FIDIA Mwaka 2004 ambayo yapo kwa MKUU wa WILAYA wao Wamekuwa WAKISHIRIKIANA
na hao Watu Kuwataka WAMILIKI Halali
ndio WAWALIPE Fidia wakati Wao MANISPAA ndio WALIOTWAA hayo MASHAMBA na KUPIMA Viwanja na KUVIUZA.

Isitoshe kuna Baadhi ya WAMILIKI Wamekwisha fungua KESI MAHAKAMA KUU na HUKUMU kutoka na kuwa Wao ni WAMILIKI Halali na Wanaodai Fidia Wametakiwa Walipwe na Aliyetwaa Mashamba yao Mwaka 2004.

Ambaye ni MANISPAA Tunaiomba WIZARA ya ARDHI kupitia WAZIRI wake Mh.LUKUVI Aingilie Kati MGOGORO huu Unaosimamiwa na MAAFISA Ardhi wa MANISPAA ambayo Wanafanya Kazi Kinyume na Sheria za Ardhi.

Kuna Baadhi ya Wadai Fidia wamepewa Barua za kuwamilikisha huku Wakijua VIWANJA hivyo Vina WAMILIKI wenye HATI MILKI .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom