Manispaa ya Morogoro hii ni aibu

Nani wa kulaumiwa kutokana na kadhia hii?

  • Mteuzi wao

  • Viongozi husika

  • Wananchi na NMB


Results are only viewable after voting.

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
35,969
40,837
Nimepita mjini Morogoro mtaa uliopo kushoto mwa uzio wa NMB mara kadhaa na kushuhudia hali hii kwenye picha. Najiuliza swali hivi ni kitu gani kinashindikana kuweka mazingira ya mji wenu katika hali ya usafi wakati hapo ni makao makuu ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa yupo hapo, Mkurugenzi wa Manispaa yupo hapo, Mkuu wa wilaya yupo hapo, magari ya taka yapo hapo, ushuru unakusanywa kutoka kwa kila mfanya biashara katika eneo husika....., Enyi viongozi, je hamuoni kama hamuwatendei haki wale mnaowafungia biashara zao kwa kisingizio cha kipindupindu wakati wao wanafanya biashara kwenye mazingira machafu yanayosababishwa na uzembe wenu?
 

Attachments

  • 20160203_084108.jpg
    20160203_084108.jpg
    327.9 KB · Views: 25
  • 20160203_084040.jpg
    20160203_084040.jpg
    375.2 KB · Views: 25
Back
Top Bottom