figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
MANISPAA YA KINONDONI YAPATA MFADHILI KUSAIDIA KUKUSANYA TAKA NA KUJENGA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MBOLEA ITOKANAYO NA TAKA
Manispaa ya Kinondoni imepata mfadhili wa kutekeleza mradi wa ukusanyaji taka katika Manispaa ya Kinondoni na kujengwa kiwanda cha kutengeneza mbolea zitokanazo na taka hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kinondoni, leo Jumatano 27/01/2016 muda wa saa 4 asubuhi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob amesema "Mradi huu umefadhiliwa na Manispaa ya Hamburg Ujerumani na unagharimu shilingi bilioni 3.5 za Kitanzania".
Kiwanda hicho cha kutengeneza mbolea itokakanayo na taka zitakazokusanywa kutoka Manispaa ya Kinondoni, kitajengwa eneo la Mwabepande Kinondoni. Kiwanda hicho kikubwa cha mbolea itokanayo na takataka, kitasaidia upatikanaji wa ajira kwa wakazi wa manispaa hiyo zaidi ya 500.
"Eneo limeshapatikana eneo la Mwabepande, kilichobaki ni kuanza utekelezaji tu, ni fursa pia kutoa ajira kwa Watanzania, wakati huo huo kufanya manispaa yetu ya Kinondoni katika hali ya usafi" aliongeza Mstahiki Meya wa Kinondoni.
Kwa upande wake mwakilishi wa Manispaa ya jiji la Hamburg Ujerumani ambaye pia ni Mshauri Mtaalam wa mradi huo, Dk. Florian Kolsch amesema atakuwa karibu kushauri na kutekeleza ili kuhakikisha mradi huo unafanikiwa na kuhakikisha Manispaa ya Kinondoni inakuwa katika hali ya usafisiku zote.