Manispaa ya Kinondoni watuletea tena duplicate ya majembe auction mart

Monyiaichi

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
1,826
508
Wana JF,
Nimeamua niandike kuhusu zabuni iliyotolewa na manispaa ya Kinondoni kwa kampuni ya Mwamkinga Auction Mart.
Labda niulize swali kwanza, lengo hasa la hizi kampuni ni nini?

Kama ni kwa ajili ya kupunguza shida zitokanazo na makosa ya madereva wanaopaki hovyo sehemu zisizoruhusiwa na barabrani, basi kitakachoendelea hapa mostly ni uonevu na ulaji wa rushwa kama ilivyokuwa kwa majembe, tena manispaa wala haitopata kodi stahiki kwa kuwa wengi watapenda kumalizana njiani bila kufikisha pesa husika kwenye ofisi husika.

Usumbufu bado ni mkubwa, wafanyakazi wa hiyo mart njaa zao ni kali hazina mfano.

Suggestion:
Kwa nini kitengo cha kufuatilia uvunjaji wa sheria barabarani kisiwekwe chini ya jeshi la polisi ambao ni wazoefu na niwahusika wa usalama barabarani?

Au ni swala la kupeana ulaji? Wengine wanaweza kujibu kuwa polisi pia wanakula rushwa, sikatai. Lakini niseme tu ukweli si polisi wote ni wala rushwa, nimeshakutana na polisi wazuri tu na waanaojituma, tena polisi huwa wanapima na extent ya kosa lenyewe kuliko hawa walafi na waongo.

Sijui wenzangu kama mme experience haya na mmeyaonaje.
 
Police wako wachache mkuu, ht hivyo lengo ni kuthibiti watu wasiegeshe magari pembeni ya barabara no matter km wanatoa rushwa au lah
 
Wananichekesha wanavyo tegeshea bodaboda na kuchomoa funguo.yaan wana kaa mbali na kuvizia.

pole kwa waendesha carry a.k.a kirikuu na Maguta maana ndo wateja wao wakuu.
 
Kwa bahati mbaya mm nimepata tabu na hawa watu mara 2.
Sio waelewa kitu cha kwanza, siku ya kwanza gari ilipata hitilafu sinza opposite na Hongera bar, nikawasha harzard nikatoka kwenye gari kwenda kutafuta fundi around, narudi nakuta gari hakuna. Nauliza watu wanasema jamaa wa mwamkinga wamechukua gari kwa hiyo niende yard yao magomeni. Nimefika kule harzard bado zinawaka wakasema ilibidi niwepo around na kuweka triangle mbele na nyuma.

Wakachukua 160, 000/-
 
Back
Top Bottom