Manispaa ya Iringa fungueni barabara

Msisina

Senior Member
Aug 23, 2019
194
162
Nikiwa katika ziara fupi hapo Iringa, kuna mambo machache yamenisisimua sana juu ya kufunguka kwa mji huu kimaendeleo kwa siku zijazo:-

Mosi, ni zaidi ya miongo miñne sasa kumekuwa na mpango wa ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara mashuhuri ya Capetown to Cairo yenye kipande cha KM 3 kinachopita eneo la sabasaba na Chuo Cha Ualimu Kreluu, ambalo ni katikati ya mji wa Iringa. Barabara hii ni mbovu sana na yenye mashimo makubwa na hata ikifanyiwa msawazo bado ni shida pindi tu ikiruhusiwa kutumika, kwani inategemewa na wakazi wengi.

Hivi ingewekwa kwenye mpango wa karibuni wa ujenzi wa lami, ingefaa sana kutumika kwa usafiri wa ndani ikiwemo Bajaji. Hali hiyo itasaidia kupunguza mchuano mkali wa waendesha Bajaji hao na Mamlaka za Manispaa hiyo, kwa Madai ya nao waruhusiwe kupita katika njia kuu. Aidha, barabara hiyo utakuwa ni njia pacha ya barabara inayotumika zaidi muda wote (Dodoma road) inayopitia eneo la Lugalo kuelekea Kihesa.

Pili, kwakuwa Sasa Tanroad wanajenga barabara kiungo (diversive road) kutoka njiapanda ya Chuo Kikuu cha Iringa (junction ya Dodona road) kwenda Stendi kuu ya Igumbilo, nashauri wataalamu waone uwezekano wa kuweka 'Roundabout' kwenye makutano hayo ya junction ya barabara ya Dodoma eneo la TRM.

Ushauri huo ni wa msingi kwani itasaidia kupunguza ajali pamoja na msongamano utakaotokana na uwepo wa njia moja tu ya kuingia katika njia nchepuko hiyo, inayolengwa kutumika zaidi na magari yote makubwa, kwani pia itasaidia sana kupunguza msongamano wa magari katikati ya mji.
 
Back
Top Bottom