Manispaa ya Ilala na Polisi wazuia mkutano wa Waislam Jangwani wadai ushaombwa na New Life Ministry

Status
Not open for further replies.

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Jeshi la Polisi nchini na Halmashauri ya wilaya ya Ilala wamekataa ombi la waislam kufanya swala ma mkutano waliokuwa wameupanga kuufanya ndani ya viwanja vya Jangwani leo kupinga filamu inayo mdharirisha mtume Muhamad na uislam kwa ujumla

Sosi: ITV Habari ya saa kumi na mbili Asubuhi
 
nimeisikia hii habari ITV asubuhi hii ... mbona hawakuwaambia tangu jana au ...?
 
Mkutano uliodhamiriwa kuendeshwa na Jumuia za Kiislamu katika eneo la Jangwani siku ya leo umezuiwa na Jeshi la Polisi.

Sababu ilitolewa na jeshi hilo ni kuwa kuna mkutano mwingine eneo hilohilo ambao ulitangulia kuombwa na taasisi iliyotajwa kuwa ni New Life Ministry.
Nia ya mkutano wa Jumuia za Kiislamu ilikuwa ni kuwaeleza Waislamu kuhusiana na kadhia ya picha ya filamu inayoidaiwa kumdhalilisha mtume na Uislamu iliyotengenezwa huko Marekani.
 
Jamani, viwanja vya jangwani si vinatosha kuhost hata mikutano kadhaa?!, ni nillitaka kuona hawa jamaa walivalia makubasi, njiwa na vichaka vya ndevu wanavyotokwa na mapovu dhidi ya creativity ya teja la kimarekani.
 
Kumbe huwa wanaomba kibali!? Mbona last time "tulidanganywa" kwamba waliandamana bila kibali?
 
Mkutano uliodhamiriwa kuendeshwa na Jumuia za Kiislamu katika eneo la Jangwani siku ya leo umezuiwa na Jeshi la Polisi.

Sababu ilitolewa na jeshi hilo ni kuwa kuna mkutano mwingine eneo hilohilo ambao ulitangulia kuombwa na taasisi iliyotajwa kuwa ni New Life Ministry.
Nia ya mkutano wa Jumuia za Kiislamu ilikuwa ni kuwaeleza Waislamu kuhusiana na kadhia ya picha ya filamu inayoidaiwa kumdhalilisha mtume na Uislamu iliyotengenezwa huko Marekani.

Tunatofautiana kwa priorities !!!!!!!! Hivi kweli hao wamarekani watasikia kuwa kuna maandamano jangwani! Kwa effect ipi kwa marekani hata wakiyasikia! Halafu Ndalichako anawaonea!!!
 
Kwa ninavyowajua Waislamu, watafanya huo mkutano na hakuna polisi atakayethubutu kuwagusa sana sana watawapa escort tuu.
 
Tunatofautiana kwa priorities !!!!!!!! Hivi kweli hao wamarekani watasikia kuwa kuna maandamano jangwani! Kwa effect ipi kwa marekani hata wakiyasikia! Halafu Ndalichako anawaonea!!!
Sio lazima wamarekani wasikie, lkn ni lazima Waislamu wote wajue suala hili na walikemee kwa kutoa hisia zao.
 
Taarifa ya habari ya itv ni saa ngapi? Unahisi waliwapigia simu alfajiri kuwaambia hivyo? Issue hapo ni venue ilishakuwa booked. Msiigeuze hii issue kuwa ya kidini sasa jamani!

Thank u aisee, na muda si mrefu hali itaharibika kwenye hii thread!
 
Jamani, viwanja vya jangwani si vinatosha kuhost hata mikutano kadhaa?!, ni nillitaka kuona hawa jamaa walivalia makubasi, njiwa na vichaka vya ndevu wanavyotokwa na mapovu dhidi ya creativity ya teja la kimarekani.

Mkuu maji na mafuta havichangamani!..unadhani CDM na CCM wanaweza kufanya mkutano sehemu moja?, au wanazi wa timu za Simba na Yanga wakaa jukwaa moja?
 
Hivi mwenye mamlaka ya kutoa kibali cha mikutano Jangwani ni nani? Iweje ahalalishe vibali viwili hasa kwa makundi ya jamii mbili zenye itikadi tofauti...Anayetoa vibali ndiye ambaye hakutumia busara
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom