Manispaa ya Ilala bomoeni zile nyumba jirani na jengo la Yanga, zimekuwa maficho ya vibaka

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,073
Mafuriko yaliyolikumba Jiji la Dar es Salaam wakati wa Utawala wa Awamu ya 4 na Mkuu wa Mkoa akiwa Mzee Meki Sadik, wakazi wa Jangwani walihamishwa na kupelekwa Mabwepande na kupewa makazi na miongoni mwao ni wale waliojenga jirani na jengo la Klabu ya Yanga upande wa Barabara ya Morogoro.

Pamoja na wenye hizo nyumba kuondolewa bado nyumba hizo zipo, hazijabomolewa, na kuwa makazi ya vibaka ambao wamekuwa wakipiga wapita njia nyakati za usiku na alfajiri na kuwapora hali ambayo eneo hilo limekuwa hatarishi.

Tunawataka wahusika ambao ni Manispaa ya Ilala izibomoe nyumba hizi kwa ajili ya usalama wa wapita njia.
 
Back
Top Bottom