Manispaa ya Dodoma hamuoni aibu kwa ubovu wa kituo hiki cha daladala?

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Dodoma ni mji ulio katikati ya nchi. Mji ambao ndio uliopewa hadhi ya kuwa makao makuu ya serikali. Sifa hizi chache zinafanya uwe ni mji unaopokea wageni kwa wingi kutoka pande zote za nchi sambamba na ongezeko kubwa la wakazi kwa sasa. Lakini hali ya kituo kikuu cha daladala maarufu kwa jina la JAMATINI inasikitisha. Ukweli hakifanani na hadhi ya mji, vumbi, tope wakati wa mvua, utaratibu wa hovyo wakati wa kuingia na kutoka magari ni kero kubwa. Hakuna ubishi hiki chaweza kuwa ndio kitu cha daladala kibaya zaidi hapa nchini. Wahusika mpo? Au mmelala usingizi?
 
Pale jamatini mvua ikinyesha utadhani bwawa la samaki au shamba la mpunga.Kituo kipo karibu kabisa na ofisi za manispaa.Unapita Tanesco,unakunja shell unanyoosha Sido unaingia manispaa!Wenyewe hawana habari.Wako bize kufukuza machinga mabarabarani tu.
 
Back
Top Bottom