Manispaa; Ukijenga ghorofa ni sharti uwaezekee vyoo majilani zako usijekuwachungulia

Nafikiri kuna kanuni za ujenzi ambazo zilitoka miaka ya karibuni hapa kwamba ni Kosa kujenga choo bila kuezeka/kuziba paa

Ilileta mgogoro sana kwenye baraza la madiwani wa manispaa ya Temeke
 
kama ni kweli basi hizo sheria ziliandaliwa na watu masikini
Unadhani enzi zaMfalme Daudi wakati alipokuwa akitembea kwenye ghorofa lake ndipo akamuona mke wa askari wake akioga kisha akavutiwa hadi akafanya njama yule askari akafia vitani, je lile bafu lilikuwa limeezekwa au halikuezekwa?
 
Kwa wale ambao hamjui;

Moja ya maelekezo ya ujenzi kutoka manispaa yanayopaswa kuzingatiwa unapojenga nyumba ya ghorofa mtaani kwako, (Sikumbuki kifungu namba ngapi) ni kuhakikisha unawaezekea vyoo na Bafu majilani zako wanao kuzunguka kila upande wasiozidi wanne pande zote. Usipofanya hivo unaweza shitakiwa Kwa kosa la kuingilia faragha ya mtu (Uzalilishaji)
Mwananyamala kwa kopa tunachunguliwa sana NA vyoo vyetu vya ghorofa ......hata yale maghorofa pale Victoria wanatupiga sana chabo.....kumbe sheria IPO ....ngoja siku nipigike
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom