Manispaa Ubungo yapitisha bajeti ya billioni 84, kwa mwaka wa fedha 2019/2020

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,260
2,000
IMG-20190227-WA0047.jpg


Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo yapitisha Makadirio ya beti ya 2019/2020 Kutumia Kiasi cha Tsh Billioni 84.6

Akisoma Hotuba yake Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo,Mh Boniface Jacob, amefanunua kuwa katika pesa hizo serikali itatoa ruzuku ya Billioni 65.5,Millioni 750 ni michango ya Wananchi na billioni 18.4 ni Makusanyo ya ndani.

Ambapo katika matumizi yake fedha hizo,Billioni 72.3 ni Mishahara ya watumishi,Na kiasi cha billioni 12.3 zimeelekezwa katika miradi Mbalimbali ya Maendeleo

Aidha ameweka msisitizo kuwa Kiasi cha billioni 8.3 sawa na Asilimia 60,za mapato yanayokusanywa na Halmashauri zitatumika kwa ajili ya Miradi ya maendeleo

Mstahiki meya ametaja Vipaumbele 11 vya Halmashauri vilivyomo katika Bajeti hiyo
πŸ‘‰πŸ½kuboresha utoaji huduma kwa jamii kwa kuongeza pesa za kujengea Makao makuu ya Halmashauri kiasi cha Millioni 700
πŸ‘‰πŸ½Kuanza kujenga Hospitali ya wilaya kwa kiasi cha Tsh Millioni 250
πŸ‘‰πŸ½Kutenga fedha za kujenga machinjio ya kisasa kiasi cha Tsh Millioni 250
πŸ‘‰πŸ½Kutenga fedha Kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Mbezi( kwa ajili ya wamachinga) Kiasi cha Tsh millioni 300
πŸ‘‰πŸ½Kuimarisha Utawala bora kwa kuwatengea fedha za kiinua Mgongo wenyeviti wa Serikali za mitaa wanaomaliza muda wao mwaka 2019
πŸ‘‰πŸ½Kuongeza Mapato kwa kuboresha miundombinu ya ukusanyaji,kubuni vyanzo vipya,Uanzishaji wa stendi za daladala Mloganzila na Msumi,Uanzishwaji wa Masoko mapya Kiasi cha Tsh Billioni 1.7 zimetengwa
πŸ‘‰πŸ½Kuongeza kiwango cha Uzoaji taka Ngumu kwa manispaa kwa Kununua Vifaa vya ubebaji taka kama magari na mitambo,Kiasi cha Tsh billioni 3.02 kimetengwa
πŸ‘‰πŸ½Ujenzi wa Mabweni ya Wavulana na Wasichana shule ya Sekondari Goba TshMillioni 230 zimetengwa
πŸ‘‰πŸ½Kutoa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake,Vijana na Walemavu Kiasi cha Tsh billioni 1.38 zimetengwa
πŸ‘‰πŸ½Kupima maeneo ya Umma,kwa kutoa hati miliki na kutwaa Maeneo ya miradi ya uwekezaji Kiasi cha Tsh billioni 1.4 zimetengwa
πŸ‘‰πŸ½Kwa kuboresha na Kujenga Miundombinu ya Elimu Msingi na Sekondari kwa kujenga madarasa na Nyumba za walimu,Kiasi cha Tsh billioni 1.168 zimetengwa kwa kazi hiyo.
MWISHO
Mstahiki meya amesisitiza kuwa,Halmashauri ni chombo cha wananchi ambacho kimewekwa kisheria katika kukuza uchumi na kusogeza ajira kwa Vijana ili kupunguza Umasikini hasa wa kipato ili Kujiletea Maisha Bora

IMETOLEWA NA
OFISI YA MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA UBUNGO
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom