Manispaa Iringa wamlilia Mkurugenzi wao, wasema tumefikia mchapakazi anaondolewa kupisha makada

Kilasi Mkuu

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
2,325
719
Ukipita katika mitaa ya manispaa ya Iringa lazima utakutana na habari hii. Watu wanashangaa kilichotokea maana hata ushindi wa usafi kitaifa ilikuwa kazi ya mkurugenzi huyu akishirikianana baraza lake la madiwani.

Nimewashuhudia watu wakisema mtu huyu alikuwa habagui mtu anaweza akamsikiliza mtu hamjui na ofisini kwake hakuna ulazima wa kutoa taarifa ili kuingia, mfano shule ya Iringa Gilrs ilkuwa inahitaji gari wakaitisha harambee wakapata kiasi fulani cha hela walipo enda kwake akawambia hela hizo wafanyie kazi nyingine na yeye akawapa gari na dereva wa manispaa.

Watumishi wote ukiwauluza utasikia mtumishi huyu alikuja kuibadilisha manispaa kweli.

Sasa kumuondoa hivihivi sijui kama ndio tunakoenda. Inakatisha tamaa kwa wachapakazi kwakweli
 
ukipita katika mitaa ya manispaa ya Iringa lazima uta kutana na habari hii.Watu wanashangaa kilicho tokea maana hata ushindi wa usafi kitaifa ilikuwa kazi ya mkurugenzi huyu akishirikianana baraza lake la madiwani.Nimewa shuhudia watu wakisema mtu huyu alikuwa habagui mtu.anaweza akamsikiliza mtu hamjui na ofisini kwake hakuna ulazima wa kutoa taarifa ili uingia.mfano shule ya Iringa Gilrs ilkuwa ina hitaji gari wakaitisha harambee waka pata kiasi fulani cha hela walipo enda kwake akawambia hela hizo wafanyie kazi nyingine na yeye akawapa gari nadereva wa manispaa.Watumishi wote ukiwa uluza uta sikia mtumishi huyu alikuja kuibadilisha manispaa kweli.Sasa kumuondoa hivihivi sijui kama ndio tuna koenda.Inakatisha tamaa kwa wachapa kazi kwakweli
Ni vizuri haki kuwapo
 
Kwa hiyo akakataa pesa ya msaafa akawaambie wafanye mengine sababu pesa ya serikali ipo tu kufanya lolote lile? Mmmmmmmmmm
 
Lazima wwe utakuwa ni mtumishi wa manispaa hapo Iringa,
Mana haya nimeyasikia kutoka kwa mtumishi wa hapohapo,

Aliyeletwa sasa anaitwa nani na alikuwa wapi?
 
Aliona haitoshi mkuu na kukawa na idara ina magari zaidi

Ila ungeandika na mengine uliyofanya au nduguyo aliyofanya basi..

Gari ya serikali na nani alilipia mafuta? maana pesa ya harambee alisema watumbue kwa mengine...

Pia kwa jinsi ulivyoandika wewe hujaona mazuri na mabaya yake bali wewe unasikia tu...hapo sasa

Sasa hivi hana kazi?
 
Lazima wwe utakuwa ni mtumishi wa manispaa hapo Iringa,
Mana haya nimeyasikia kutoka kwa mtumishi wa hapohapo,

Aliyeletwa sasa anaitwa nani na alikuwa wapi?
Sijajua jina lake wala utendaji wake lakini kwanini huyu mchapa kazi kaondolewa?
 
Ila ungeandika na mengine uliyofanya au nduguyo aliyofanya basi..

Gari ya serikali na nani alilipia mafuta? maana pesa ya harambee alisema watumbue kwa mengine...

Pia kwa jinsi ulivyoandika wewe hujaona mazuri na mabaya yake bali wewe unasikia tu...hapo sasa

Sasa hivi hana kazi?
Kwani wewe mkuu ume sikia kapangwa wapi?
 
Mkuu hayo ni Yale unayoyajua wewe na wananchi baadhi machoni mwenu, lakini Kuna mengine ambayo hamyajui, hayaonekani mpaka kwa darubini, ndo yaliyomuandoa hapo IRINGA.
 
Lazima wwe utakuwa ni mtumishi wa manispaa hapo Iringa,
Mana haya nimeyasikia kutoka kwa mtumishi wa hapohapo,

Aliyeletwa sasa anaitwa nani na alikuwa wapi?
Huyu mgeni nadhani katokea wilaya ya Chemba Dodoma kabla ya kupangiwa iringa manispaa.Nilipata fanya naye kazi,ni jembe pia
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom