Manispaa Iringa wamlilia Mkurugenzi wao, wasema tumefikia mchapakazi anaondolewa kupisha makada

Kwani wewe mkuu ume sikia kapangwa wapi?

Kituko kwa hiyo kufanya kazi hadi kupangiwa tena...CV si ipo ni kuisambaza basi kama kazi hakuna kupangwa kwake yeye...

Kweli mlizoea vibaya...hahahaaaaaa

Kazi zipo nyingi hata kilimo...tena Iringa vitunguu unakuwa millionea haraka
 
Huyo mkurugenzi wa iringa manispaa alikuwa feki sana. Anaitwa Ahmed Sawa. Aliwahi kuwa mkurugenzi wa manispaa Musoma.

Hana misimamo, na ni mtu mwoga mwoga sana. In short, alikuwa mbabaishaji sana. Ila yupo simple sana, na anapenda kuongea na kila mtu, na vijiwe vya kahawa ni mwenyeji sana.

Hicho ndo kilikuwa kinaficha weakness zake. Lkni, kikazi na uelewa wa mambo alikuwa mweupe sana. Ngoja arudi same kwao akalime. Uzuri ile pick up yake nyekundu inaweza somba nyasi za ng'ombe na mahindi shambani. Jamaa sio fisadi kiujumla, ila ujio wao kipunga kimepita
 
Yeye na Mwenyekt wa CCM Mkoa walichakachua kura za Mwakalebela wakmpa Msigwa
CCM ilishindwa kusoma alama za nyakati na kuweka mgombea asiye sahihi. Swali la kujiuliza ni je, hadi madiwani Sawa na Jesca waliiba kura za CCM? Uchungu wa kukataliwa na wana - Iringa wanamuonea/kumchongea aliyemwagikiwa na damu (CCM ilichinjwa nyang'anyang'a Iringa) Acheni kuonea watumishi kwa kuwaundia zengwe.
 
Ukiona hivo ujuwe kaikwaza CCM. Kwann hakupindua matokeo mpk aruhusu manispaa kuchukuliwa na CHADEMA?
 
Ila ungeandika na mengine uliyofanya au nduguyo aliyofanya basi..

Gari ya serikali na nani alilipia mafuta? maana pesa ya harambee alisema watumbue kwa mengine...

Pia kwa jinsi ulivyoandika wewe hujaona mazuri na mabaya yake bali wewe unasikia tu...hapo sasa

Sasa hivi hana kazi?
Mabaya yake ni kushindwa kuchakachua matokeo, fuatilia halmashauri zote ambako upinzani walishinda wakurugenzi wameondolewa; haijalishi walikuwa na uwezo wa kuwaletea maendeleo wananchi au la!
 
Yeye na Mwenyekt wa CCM Mkoa walichakachua kura za Mwakalebela wakmpa Msigwa
Ah hahahahaaa...usiyoyajua ni kama usiku wa kiza,
Nlikuwepo kwenye chumba ambacho alilazimishwa arudie kuhesabu kuraaaa,
Yaliyotokea mle ni makubwa, kuraaaa zilipitishiwa kwenye dari...
Msigwaaaaa angekubali leo angeusikia kwenye bomba
 
Sijajua jina lake wala utendaji wake lakini kwanini huyu mchapa kazi kaondolewa?
Atatoaje gari la Serikali na kuwapa Urunga Girls km gari katoa mfukoni mwake
ni vingapi kafanya hivyo wakati sio maelekezo ya mwajiri wake Chama tawala
Rais kawaelekezaviongozi wote aliowaapisha kuwa wakatekeleza sera za CCM
huyo Mkurugenzi hakuendana na wenzake ndio maana kachomwa
 
CCM ilishindwa kusoma alama za nyakati na kuweka mgombea asiye sahihi. Swali la kujiuliza ni je, hadi madiwani Sawa na ***** waliiba kura za CCM? Uchungu wa kukataliwa na wana - Iringa wanamuonea/kumchongea aliyemwagikiwa na damu (CCM ilichinjwa nyang'anyang'a Iringa) Acheni kuonea watumishi kwa kuwaundia zengwe.
Anasema watanzania wamuombee,Mungu yupi humsikia asiye tenda haki?
 
Ah hahahahaaa...usiyoyajua ni kama usiku wa kiza,
Nlikuwepo kwenye chumba ambacho alilazimishwa arudie kuhesabu kuraaaa,
Yaliyotokea mle ni makubwa, kuraaaa zilipitishiwa kwenye dari...
Msigwaaaaa angekubali leo angeusikia kwenye bomba
Sasa mwugimbi amemwachaje,hana hata hofu ya Mungu?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom