Manispaa Ilala yanyang’anywa TSh 3 bilioni ya Uboreshaji wa Machinjio ya Vingunguti

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
2,239
2,000
1550641825062.png

Dar es Salaam. Serikali imeinyang'anya Manispaa ya Ilala, mkoani Dar es Salaam Sh3 bilioni ilizoipatia kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kimkakati wa machinjio ya kisasa ya Vingunguti.
Uamuzi huo umetokana na manispaa hiyo kushindwa kutekeleza kwa wakati mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Sh8.5bilioni.

Hayo yameelezwa na naibu waziri wa fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo.
Amesema Serikali ilitoa Sh3 bilioni kati ya Sh8.5 bilioni kukamilisha mradi wa machinjio ya Vingunguti kuanzia Mei, 2018, lakini hadi sasa fedha hizo hazijatumika.

“Fedha haziwezi kukaa kwa mwaka mzima bila matumizi ilihali kuna maeneo mengine ambako fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi, hivyo tunazichukua fedha hizi na Manispaa ya Ilala mtalazimika kuomba upya mtakapokuwa mmejipanga," alieleza Dk Kijaji.
Alibainisha kuwa kwa mujibu wa taratibu za fedha za Serikali zinazopelekwa kwenye miradi zinatakiwa zianze kutumika ndani ya miezi mitatu lakini Manispaa ya Ilala haijazitumia fedha hizo huku karibu Mwaka wa Fedha ukikaribia kumalizika.

"Tunaiangusha dhamira njema ya Mheshimiwa Rais Dk John Pombe Magufuli ya kuwahudumia Watanzania waliosubiri kuhudumiwa, ndio maana tukaanzisha miradi hii ya kimkakati ya kuongeza mapato ya halmashauri na mkaleta maandiko yenu Serikali ikatoa fedha kumbe hamko tayari na mnatukwamisha kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi," alisema.

"Tumewapatia fedha mmeshindwa, kwa hiyo wana Ilala na wana Vingunguti, kwamba Serikali yao ina dhamira njema lakini wapo wanaotuangusha hivyo tutazichukua fedha hizi mpaka hapo Manispaa ya Ilala watakapoleta mpango kazi unaotekelezeka na si huu ambao hawakujiandaa," alisisitiza.

Dk Kijaji alisema kuwa kabla ya kuomba fedha za miradi ya kimkakati ni lazima masuala yote ya upembuzi yakinifu yawe yamefanyika na kama hayakufanyika basi manispaa ilimdanganya katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na waziri mwenyewe ambaye aliridhia Ilala ipewe fedha hizo.
Naye naibu kamishna wa bajeti wa wizara ya Fedha, Dk Charles Mwamwaja, alisema kuwa manispaa ya Ilala, imekiuka mkataba ama makubaliano ya kupewa ruzuku ya Sh8.5 bilioni kwa ajili ya mradi huo na ni lazima sheria ya fedha ichukue mkondo wake kwa kuzirejesha fedha hizo Mfuko Mkuu wa Hazina hadi watakapo kuwa tayari.

Kwa upande wake ofisa mipango wa manispaa ya Ilala, Ando Mwankuga, alikiri kuwa kulikuwa na ucheleweshaji wa kuanza kutekeleza mradi huo kwa kile alichodai ni kuchelewa kwa mchakato wa kufanya ununuzi na mabadiliko ya mara kwa mara ya kiufundi kutoka kwa mtaalam mshauri wa mradi huo.

"Ucheleweshaji huu si wa makusudi bali ilikuwa ni kuhakikisha tunafuata taratibu zote za ununuzi na kuhakikisha mradi utakaojengwa uwe na ubora unaotakiwa na unaolingana na thamani ya fedha na tunatarajia kuanza kuutekeleza Machi 10, 2019" aliongeza.

Manisapaa ya Ilala, ilikuwa miongoni mwa halmashauri na manispaa 17 nchini zilizopatiwa ruzuku na Serikali kiasi cha zaidi ya shilingi 147 bilioni katika awamu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati itakayochochea upatikanaji wa mapato ya ndani na kuzijengea uwezo Serikali za mitaa na miradi hiyo inatakiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 18 kuanzia Mei, 2018.

Chanzo:-https://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Manispaa-Ilala-yanyang-anywa-Sh3-bilioni/1597296-4989952-format-xhtml-iq67dfz/index.html
 
HORSE POWER

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
1,718
2,000
Ni maamuzi muafaka dhidi ya watendaji wazembe.Kama ule uzembe mwingine 'kabambe' wa ucheleweshaji wa ujenzi wa stendi ya mabasi ya mikoani pale Mbezi.Waziri Jafo asingetishia kuwanyang'anya zile bilioni 50,mpaka leo mradi ungekua haujaanza.Watendaji wetu wamezoea kusukumwa sukumwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Abshallom

JF-Expert Member
May 19, 2018
224
500
Afisa Mipango alifanya kazi yake, ndio maana aliandika andiko na kuandaa bajeti ya Mradi wa Machinjio. Tatizo kwa Serikalini kama hujui linaanziaga Manunuzi, na Ofisi ya Mhandisi, kwa sababu hao ndio wanaratibu input nyingi.
hivi hiyo halmashauri kuna afisa mipango?kama yupo analipwa mshahara wa kazi gani?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hasheem Kaz

Member
Sep 4, 2018
32
125
Write your reply...Labda walikosea bajeti, waliandaa bajeti isiyotosha. Hivyo wanaogopa kugusa hela na mradi usihishe.
Au wanajisahaulisha zikae muda mrefu watu wasahau, mwisho waanze kuzinyogoa mdogo mdogo.
 
GAS STATE

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
1,771
2,000
NI AIBU SANA KWA WANA Dar haiwezekani pesa ije then ikalishwe tu hapo pana walakini mbaya zaidi kuna baraza la madiwani sijuwi linafanya kazi gani ila huenda ikawa kutuzuga kumbe afisa kaambiwa subirisha mradi hadi pesa ipokwe iende ktk maeneo ya chama chetu siasa mbaya kwakweli. kama kachelewesha mradi hadi pesa kupokwa je atachukuliwa hatua gani, haya ndio mambo Makonda ayakomalie kwani yanahusu uchumi wa mkoa wake sio kwenye issue za Kitaifa zisizo na effect kwa Dar
 
Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,031
2,000
View attachment 1027005
Dar es Salaam. Serikali imeinyang'anya Manispaa ya Ilala, mkoani Dar es Salaam Sh3 bilioni ilizoipatia kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kimkakati wa machinjio ya kisasa ya Vingunguti.
Uamuzi huo umetokana na manispaa hiyo kushindwa kutekeleza kwa wakati mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Sh8.5bilioni.

Hayo yameelezwa na naibu waziri wa fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo.
Amesema Serikali ilitoa Sh3 bilioni kati ya Sh8.5 bilioni kukamilisha mradi wa machinjio ya Vingunguti kuanzia Mei, 2018, lakini hadi sasa fedha hizo hazijatumika.

“Fedha haziwezi kukaa kwa mwaka mzima bila matumizi ilihali kuna maeneo mengine ambako fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi, hivyo tunazichukua fedha hizi na Manispaa ya Ilala mtalazimika kuomba upya mtakapokuwa mmejipanga," alieleza Dk Kijaji.
Alibainisha kuwa kwa mujibu wa taratibu za fedha za Serikali zinazopelekwa kwenye miradi zinatakiwa zianze kutumika ndani ya miezi mitatu lakini Manispaa ya Ilala haijazitumia fedha hizo huku karibu Mwaka wa Fedha ukikaribia kumalizika.

"Tunaiangusha dhamira njema ya Mheshimiwa Rais Dk John Pombe Magufuli ya kuwahudumia Watanzania waliosubiri kuhudumiwa, ndio maana tukaanzisha miradi hii ya kimkakati ya kuongeza mapato ya halmashauri na mkaleta maandiko yenu Serikali ikatoa fedha kumbe hamko tayari na mnatukwamisha kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi," alisema.

"Tumewapatia fedha mmeshindwa, kwa hiyo wana Ilala na wana Vingunguti, kwamba Serikali yao ina dhamira njema lakini wapo wanaotuangusha hivyo tutazichukua fedha hizi mpaka hapo Manispaa ya Ilala watakapoleta mpango kazi unaotekelezeka na si huu ambao hawakujiandaa," alisisitiza.

Dk Kijaji alisema kuwa kabla ya kuomba fedha za miradi ya kimkakati ni lazima masuala yote ya upembuzi yakinifu yawe yamefanyika na kama hayakufanyika basi manispaa ilimdanganya katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na waziri mwenyewe ambaye aliridhia Ilala ipewe fedha hizo.
Naye naibu kamishna wa bajeti wa wizara ya Fedha, Dk Charles Mwamwaja, alisema kuwa manispaa ya Ilala, imekiuka mkataba ama makubaliano ya kupewa ruzuku ya Sh8.5 bilioni kwa ajili ya mradi huo na ni lazima sheria ya fedha ichukue mkondo wake kwa kuzirejesha fedha hizo Mfuko Mkuu wa Hazina hadi watakapo kuwa tayari.

Kwa upande wake ofisa mipango wa manispaa ya Ilala, Ando Mwankuga, alikiri kuwa kulikuwa na ucheleweshaji wa kuanza kutekeleza mradi huo kwa kile alichodai ni kuchelewa kwa mchakato wa kufanya ununuzi na mabadiliko ya mara kwa mara ya kiufundi kutoka kwa mtaalam mshauri wa mradi huo.

"Ucheleweshaji huu si wa makusudi bali ilikuwa ni kuhakikisha tunafuata taratibu zote za ununuzi na kuhakikisha mradi utakaojengwa uwe na ubora unaotakiwa na unaolingana na thamani ya fedha na tunatarajia kuanza kuutekeleza Machi 10, 2019" aliongeza.

Manisapaa ya Ilala, ilikuwa miongoni mwa halmashauri na manispaa 17 nchini zilizopatiwa ruzuku na Serikali kiasi cha zaidi ya shilingi 147 bilioni katika awamu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati itakayochochea upatikanaji wa mapato ya ndani na kuzijengea uwezo Serikali za mitaa na miradi hiyo inatakiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 18 kuanzia Mei, 2018.

Chanzo:-https://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Manispaa-Ilala-yanyang-anywa-Sh3-bilioni/1597296-4989952-format-xhtml-iq67dfz/index.html
Naona huyu mama very soon atakuwa full minister wa wizara ya fedha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangawizi

JF-Expert Member
Jun 25, 2009
3,382
2,000
Makonda aeleze imekuwaje. Kama stand ya mabasi. Dar kuna shida kubwa ya kutoa maamuzi sababu wengi wa wanaokaa katika nafasi hizo wana ajenda binafsi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom