Manguta - for rumba old school members | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manguta - for rumba old school members

Discussion in 'Entertainment' started by Sikonge, Oct 9, 2008.

 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kwa wale wapenzi wa Rumba,
  Nimeipata hatimaye album ya NGUASHI - NTIMBO & LE T.P.O.K. JAZZ na ndani kuna nyimbo nne tu yaani (FACE A) 1. Manguta, 2. Mzazi.
  (Face B) 1. Bolingo ya sens unique, 2. Cheri ago (ntimbo).

  Ntajitahidi kuzirekodi kabla ya X-Mas ili watu wakati wa X-mas wajikumbushe miaka hiyo ya 80 mwanzoni. Ila santuri kidogo imechoka na ntarekodi na nijaribu kuipeleka kwa jamaa wanaozifanyia matengenezo. Nikifanikiwa kuiweka katika hali nzuri zaidi basi ntarudia tena na kuziweka nyimbo kuwa DIGITAL na kuziweka katika link ambayo watu wataweza kwenda na kuvuta.
  Fmes, hii nimeipata duka moja Ufaransa (ONLINE) na jamaa nilifanya kumuuliza kama anayo na alipoangalia stoo akanijibu anayo. Nimenunua na kanitumia. Naangalia hapa naona imetengenezwa Ivory-Coast /Abijan na distribution wamefanya Shakara Music. Naona hii ndiyo inasababisha hii album kuwa ngumu kupatikana. Nafikiri Ivory-coast jamaa si maarufu na huko ndiko alitengenezea.

  NB: Link ya hilo duka ni hii hapa kwa wale wanaotaka kupekua miziki.
  CDandLP.com - La place de marché pour le musique : achat et vente de disques et collectors
   
Loading...