Mangula: Walioruhusu magoli hatutawapa nafasi mwaka 2019

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,482
54,837
Kwa ufupi
Mangula alisema hayo jana wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho jijini hapa, kwenye kongamano la kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli na kumpongeza kwa kitendo cha kufichua mafisadi waliokuwa wakitorosha mchanga wa madini lililoandaliwa na chama hicho.
By Jackline Masinde, Mwananchi jmasinde@mwananchi.co.tz
Asema waliofanya hivyo wanajulikana na majina yao yapo.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula amesema waliohusika kukihujumu chama kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kusababisha kushindwa ndani ya majimbo na kata, hawataruhusiwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho na hata uchaguzi wa mwaka 2019.

Mangula alisema hayo jana wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho jijini hapa, kwenye kongamano la kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli na kumpongeza kwa kitendo cha kufichua mafisadi waliokuwa wakitorosha mchanga wa madini lililoandaliwa na chama hicho.

“Walioachia magoli iwe kwa kununuliwa ama kwa uzembe wao au kwa makusudi hawawezi kutumika tena kugombea katika uchaguzi ujao, nasema hapana na kama ukijijua wewe ulihusika kwa namna moja ama nyingine kuingiza magoli kwenye eneo lako usichukue fomu kugombea nafasi yoyote kwenye chama,” alisema.

Alisema majina ya watu waliokihujumu chama wanayo na bado wanaendelea kuwabaini na kuwataka wanachama kutoruhusu kabisa watu dhaifu walioachia magoli kwenye majimbo na kata kuendelea kugombea na kwamba waachane nao kabisa.

“Watu dhaifu dhaifu wanaokubali kuhongeka kirahisi msiwape tena nafasi. Tumejipanga hakuna mtu atakayejaribu tena kutuhujumu uchaguzi ujao, uzuri tunawajua na majina yao tunayo na bado tunaendelea kuwabaini,” alisema.

Aliongeza: “Kumbukumbu zenu tunazo zote nawaambia hakuna, ukijaa na fomu tunakuweka chini na kukusomea madhaifu yako yote kisha tunakuambia haya jitetee kwenye kijiwe chetu, pale hapiti mtu aliyesababisha magoli tumejipanga.”

Pia, Mangula alitumia nafasi hiyo kuwaonya wapinzani aliodai wanadandia treni kwa mbele wakijinadi kuwa kitendo alichokifanya Rais Magufuli cha kuwafichua waliokuwa wakichimba mchanga wa madini kuwa ni mawazo yao waache kwani anachokifanya Rais kimo ndani ya ilani ya CCM.

“Alichokifanya Rais kipo ndani ya ilani ya chama, wapo wanaodandia treni kwa mbele wakidai kuwa wao ndiyo walikuwa na mawazo hayo, nataka niwaambie Rais anatekeleza ilani ya chama chake na hiyo ni moja ya mipango ya chama,” alisema.

Vile vile, Mangula aliwaonya watu wanaoibuka na kutaka kukwamisha kazi anazozifanya Rais kwa kusema kuwa hawataweza na nchi haitashtakiwa kama wanavyodai.

“Niwatoe hofu wanachama na wananchi wote kuwa nchi iko salama, zaidi tumuunge mkono Rais wetu kuwafichua watu wanaoiba mali za nchi, ” alisema.

Katika hatua nyingine Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Sad Kuslawe alisema wanachama wa chama hicho wanamuunga mkono Rais na wameridhika kwa moyo wa dhati na hatua alizozichukua kwa wote waliohusika na wizi wa mchanga wa madini na kuliletea Taifa hasara kubwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Hivi huyu mtu bado yuko kwenye SIASA???Makinikia itawarudisha wengi kwenye kilinge cha siasa
 
Hilo zee lenyewe haliendani na chama likae home lile pensheni yake malumbano na vijana watamvunjia heshima na akumbuke hana kinga kana kina jk
 
M naamini hamna mtu anaependa taifa lake anaeza kuthubutu kupingana na anachofanya mkuu
 
Firwanigga naona unaitamani sana nafasi ya Humphrey Polepole, kila la heri kwenye harakati zako maana huu ni mwaka wa uchaguzi ccm.
 
Bingwa wa magoli ya mkono ni Nape wengine ni photocopy!
 
Aksante Mangula...Mungu akubariki kwa kuhakikisha Taifa haliongizwi na Fisadi.

Bila msimamo wako leo tusingeongelea haya yanayofanyika.



HONGERA SANA SANA SANA COMRADE MANGULA A.K.A MKATAJI
 
Mangula anaposema rais Magufuli anatekeleza ilani ya ccm kwenye suala la madini, pia atuambie wakati wale viongozi wa serikali waliporidhia kutiliana saini mikataba ya hovyo ya madini inayoliingizia hasara taifa walikuwa wanatekeleza ilani ya chama gani?
 
Sijui niandike? Aah mzee amegunda wale wabuge waliopitisha sheria na mikataba ya hovyo na waliosaini mikataba walikuwa wanatekeleza sera na ilani ya TLP.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom