masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,171
Leo katika gazeti la leo Nipashe, limesikika " Mangula awavaa Maaskofu, Mahakama ya Kadhi".
(uk. 1,tar 10/4/2015)
Mzee Mangula amesikika akiwalaumu Maaskofu kutokana na msimamo wao na tamko la kutounga mkono aidha uandaaji wa kura ya maoni na vile vile kulipinga kabisa jaribio la uingizaji wa suala la Mahakama ya Kadhi katika rasimu ya katiba na hivyo basi kuwa moja ya dondoo katika sheria.
Mangula amesema leo kuwa hakuna kitu kama hicho na mimi nampongeza kwa hilo.
Hata hivyo suala zima bado ni utata mtupu.
Siamini kuwa CCM ilikuwa imelala muda wote huo hadi serikali ina contemplate kuliingiza suala la Mahakama ya Kadhi bungeni.
Na kwa vile lilishatayarishwa kwa uwasilishwaji bungeni, hii ilikuwa kwa ridhaa na vikao vipi vya chama?
Na je kama hakuna vikao vya chama kupendekeza suala hili na kulipeleka bungeni, chama kina maoni gani juu ya hili, na jaribio hili.
Chama ni cha wanachama na very fast kinaanza kugeuka kuwa gulio tu la wasaka uongozi badala ya uwakilishaji wa sera za wanachama wake.
CCM ni ya wanachama wa dini zote, rangi zote, makabila yote na rangi zote.
Mangula lazima atambue kuwa Maaskofu hawakuamka asubuhi na kutoa tamko lao, tamko lilitoka kutokana na failure ya CCM kuona hatari inayoikabili nchi ikiwa ni pamoja na mifarakano ya kidini.
Watanzania tumetoka mbali katika umoja wetu na kimoja kilichosaidia ni kuondoa dini kama issue ya kisiasa.
Jaribio hili la kuchanganya dini na siasa ni baya, lakini mbaya zaidi ni CCM kukaa kimya ikitazama michakato ya kidini iki flourish bila kuyakemea.
Moja wapo ya ahadi za mwana CCM ni Fitina kwangu ni mwiko, na Nitasema kweli daima