Mangula ana wewezeka Kumjibu SLaa!!

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
864
Nimesoma Gzt la Raia Mwema la Tarehe 28Nov 2o12 na kushangazwa sana na Kauli ya Mangula kuwa Waziri Gerdon Lwenge ni Mwaadilifu Wakati Taarifa ya Tathimini ya Uchaguzi wa NJOMBE imemtaja kuwa ametoa Rushwa na tarifa zipo TAKUKURU watu wanaendelea kutoa Ushahidi hadi sasa.

Hata hivyo taarifa za TAKUKURU NJOMBE zinaonyesha kuwa Kamanda wa PCCB aitwaye Richard Samila alimukamata Gerson Lwenge katika mazingira ya Rushwa na kuhojiwa kwa masaa kadhaa mnamo tarehe 31/7/2010.
Pia Kamanda huyo wa PCCB alifanikiwa kuwakamata Wafuasi wa Waziri Gerson Lwenge (SAMSON KIWEHELO,BENITO MSOVELA,HENNRY MAWATA) wakiwa na gari T542 AUJ mali ya Waziri Gerson Lwenge.

Wafuasi hao walikamatwa wakiwa na mipira ,nguo,fedha ambapo walikuwa wanagawa kwa wapiga kura ili Waziri Lwenge apite. Picha zinaonyesha wazi katika magazeti ya Mwananchi . Sasa ni kwa Vipi Philipo Mangula aseme kuwa Gerson Lwenge ni muadilifu wakati hata vyombo vya habari vimeandika kuwa alikamatwa na Rushwa?? Mangula anashughulika na Rushwa Ipi ??;

Mangula anasema alimushuhudia YONO KEVELA kwa macho yake akitoa Rushwa lakini hakutoa taarifa PCCB. Lakini pia Mangula huyo huyo ambaye ni muumini wa Nyerere alishindwa kumushuhudia GERSON LWENGE akitoa Rushwa na wala hana taarifa kuwa alikamatwa na rushwa wala hajasoma magazeti ya Mwananchi yaliyo andika habari za Rushwa.
Mimi nimefuatilia habari katika magazeti na hata PCCB hakuna taarifa zinazo onyesha kuwa Nyimbo na Kevela wametoa Rushwa au wamekamatwa na Rushwa!!!

Kama Kweli Mangula anataka kusafisha Wala Rushwa basi ni bora anze na Nyumbani kwake Njombe ambako na yeye ni Mtuhumiwa.
Nyaraka kadha za Malalamiko zinamtaja Mangula katika kashifa.
Mangula ondoa kwanza Kibanzi kwenye jicho lako Kumbuka usafi lazima uanzie nyumbani kwako Njombe na Si Arusha kama unavyo elekezwa na Summaye.

Hiii Ni habari ya mahojiano ya Mangula katika Raia Mwema:

Mwaka 2010, jimboni kwangu kwenyewe, Njombe Magharibi. Kulikuwa na wagombea watatu; Thomas Nyimbo, Kevela (Stanley Kevela ‘Yono') na Mhandisi mmoja(Gerson Lwenge), ambaye alikuwa ni mgeni kabisa katika siasa za chama chetu, lakini Mhandisi Msomi. Nyimbo na Kevela ni wazoefu, na Nyimbo alikuwa anatetea kiti chake.

Wawili hawa (Nyimbo na Kevela) walitumia fedha nyingi kuhonga ili wapate ushindi. Ni jimboni kwangu, nami niliviona kwa macho yangu vitendo vile vya rushwa. Watu wakalalamika, chama kikajiridhisha kwamba kweli wawili hawa wameshinda kwa sababu ya rushwa. Nyimbo ndiye aliyeongoza kwa kupata kura zaidi ya 7,000, akanyang'anywa ushindi.

Baada ya kunyang'anywa ushindi, baadhi ya viongozi wetu walionufaika na fedha zake za rushswa, wakamshawishi aende upande wa pili. Wakasema NEC ya CCM yenye wajumbe wasiofika 2000 imeshindwa kuheshimu uamuzi wa viongozi wake wa ngazi ya jimbo pamoja na wanachama wake wanaofikia 7,000, kwamba hiyo ni kuwadharau viongozi na wanachama, wakamshauri (Nyimbo) agombee kupitia chama kingine.

Chama kikarejesha jina la yule Injinia. Kwa kweli alikuwa hawezi hata kumiliki jukwaa wakati wa kampeni kwa hiyo walichokuwa wakifanya wapiga debe wake, ni wao kumsemea kwa muda mrefu na kisha yeye kupewa muda mfupi tu wa kusalimia wapiga kura. Nilisema jimbo langu haliwezi kuongozwa na mbunge mtoa rushwa ili kupata uongozi. Tulipambana na Nyimbo na hatimaye tukashinda kwa asilimia zaidi ya 70, yeye akaambulia asilimia 26. Kwa hiyo, ninaposema walioingia madarakani kwa njia ya rushwa katika uchaguzi wetu huu wa ndani watanyang'anywa ushindi namaanisha hivyo, hatutanii. Tayari tumepokea malalamiko kibao hapa, tutayachambua, tutawaita wahusika wajieleze, na ikithibitika kweli kwamba ushindi wao ulipatikana kwa sababu ya rushwa, watanyang'anywa.

Raia Mwema: Suala la rushwa umelizungumza kwa mifano. Wasiwasi wangu uko kwenye kumaliza makundi, na hasa makundi ya kwenye mbio za urais 2015. Miongoni mwa wanaotajwa kuongoza makundi hayo, wanadaiwa kuwa na nguvu nyingi ndani ya chama chenu kiasi kwamba endapo mtawagusa tu, basi huo unaweza ukawa ndiyo mwisho wa CCM kushika dola. Tuambie; mtatumia njia gani kuwabaini vinara wa makundi hayo na wapambe wao, na kisha kuchukua hatua dhidi ya watu kama hao wenye nguvu ya fedha na ufuasi mkubwa ndani ya chama chenu?

Mangula: Hakuna mtu yeyote anayeweza kuchukua nguvu ya kikao. Vikao ndivyo vina uwezo usio na kikomo. Chama ni vikao. Kwa hiyo, kama kuna mwanachama yeyote ndani ya CCM au mpambe wake anayejiona ana nguvu kuliko vikao vya chama, huyo anajidanganya. Ilani ya sasa ya CCM, utekelezaji wake unaishia 2015. Utaratibu wa Chama chetu ni kwamba ikifika Mei, 2015, mwanachama yeyote anaweza sasa kuanza kutangaza nia yake ya kugombea urais, ubunge na udiwani. Lakini kuweka nia leo ya kugombea urais, ubunge na udiwani ni kuvuruga utaratibu wa Chama.

Mikakati au mechanism ya kuwabaini vinara wa makundi haya tayari tunayo. Ni kuwafungulia faili hapa ofisini na kuanza kufuatilia nyendo zao na matendo yao watakayoyafanya kuanzia sasa, na endapo mtu huyo (aliyefunguliwa faili na kufuatiliwa) atachukua fomu ya kuomba uongozi, tutamwita ndani ya vikao vyetu vya kuchuja wagombea na kumsomea madhambi yake aliyoyafanya katika harakati zake za kusaka nafasi aliyoomba kabla ya wakati.

Kamati zetu za Maadili na Usalama zitamfuatilia mhusika, na si wale tu walioko kwenye makundi ya kusaka urais, bali hata wanaosaka ubunge na udiwani kabla ya wakati nao tutawafungulia mafaili hapa. Mbunge akilalamika kwetu moja kwa moja, au kupitia vyombo vya habari kwamba kuna mwanachama mwenzake anamfanyia faulo jimboni kwake kipindi hiki cha utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015, tunafungua mafaili mawili, na juu tunaandika jina la Jimbo na wahusika, halafu tunaanza kuwafuatilia nyendo zao.

Haiwezekani mbunge, badala ya kutumia muda wake kutekeleza Ilani ya Chama chetu jimboni kwake, aanze kupoteza muda wake huo kuhangaika na mwanachama mwenzake anayelitaka jimbo husika. Vivyo hivyo kwa urais 2015. Wote hao wanaotajwatajwa kuutaka urais, wanakabiliwa na majukumu ya kutekeleza Ilani ya CCM kwa sasa. Ilani yetu ndio mkataba baina ya chama chetu na wananchi, tusipoitekeleza watatuhukumu kwa kutukataa 2015.

Kwa hiyo, haiwezekani leo, mtu mwenye matamanio ya urais wa 2015, aanze kuhangaika na mbio hizo na kusahau wajibu wake wa msingi wa kutekeleza yale tuliyoahidi 2010, halafu mtu huyo ategemee kushinda. Ili 2015 wananchi waendelee kutuamini watupe tena ridhaa yao, lazima kila kiongozi na kila mwanachama atumie nguvu na uwezo wake wote kutekeleza Ilani yetu.

Msingi wa yote haya ni mmoja tu. Ili tuweze kuandika Ilani ya 2015 hadi 2020 ambayo tutainadi kwa wananchi, lazima kama Chama tufanye kwanza tathimini ya utekelezaji wa Ilani iliyopita, kwa maana ya 2010 hadi 2015 kwa sababu Ilani hiyo ndiyo itakayokuwa hukumu yetu 2015. Kuanzia sasa, lazima vikao vyetu vyote, kuanzia ngazi ya shina, tawi, kata, jimbo, wilaya, mkoa hadi taifa vijielekeze katika kuangalia utekelezaji wa Ilani na ahadi zetu tulizoahidi.

Ilani itakayofuata (2015-2020) ieleze ni wapi tulishindwa kutekeleza ahadi yetu na ni kwa sababu gani. Yale ambayo utekelezaji wake umekwama katikati tuwe na majibu nayo. Kazi hii ya utekelezaji wa Ilani iliyopo sasa ni kazi ya muda mrefu na ni kazi ya kudumu.

Raia Mwema: Una ujumbe gani kwa wanachama na viongozi wenzako. 2015 watarajie ushindi chini ya Sekretarieti yenu mpya hii?

Mangula: Ujumbe wangu ni mmoja tu, si kwa wanachama na viongozi wenzangu tu, bali hata kwa wapinzani wetu na Watanzania kwa ujumla. Jeshi letu (wanachama wa CCM) tunafika milioni sita. Hili ni jeshi kubwa mno ukilinganisha na majeshi ya vyama vingine vinavyoshindana nasi. Kila mmoja katika jeshi hili akitimiza wajibu wake na akafanya kazi zake za kichama kwa umahiri na umakini, mwaka 2015 tutapata ushindi wa kishindo!

Sehemu ya Waraka wa Tathimini ya Uchaguzi wa CCM NJombe 2012 :

TATHIMINI YA UCHAGUZI WA MKOA WA NJOMBE 2012
CHAGUZI ZA WILAYA
Chaguzi za Wilaya ziliingiliwa na Wimbi la rushwa kutoka kwa baadhi ya Viongozi waliopo Madarakani kwa sababu ya kupanga Safu ya Mwaka 2015 wakiwemo wabunge Wafuatao:
Mhe Gerson Lwenge(Waziri) amepanga safu katika jimbo la Magharibi ambalo limo katika Wilaya ya Wanging'ombe kwa Jumuiya zote za Chama Cha Mapinduzi bila kujali aliyepata nafasi ana uwezo katika nafasi hiyo au la kwa kutumia fedha nyingi ikiwemo jumuiya ya wanawake(UWT) wakishirikiana na Mhe. Diwanai wa kata ya Mdandu ANNA UPENDO GOMBELA ambaye ni rafiki yake wa Kimapenzi (nyumba ndogo) wakati pia ni mke wa Mhe CHAMBILE .

Mhe Jofrey Nyagawa ambaye ni diwani ambaye ni diwani wa kata ya Wanging'ombe na pia ni katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Wanging'ombe alihusika kugawa fedha za rushwa kupitia mtandao wa Gerson Lwenge.
Nafasi nyingine iliyogharimu fedha nyingi za rushwa ni ya Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa (NEC) na katika RUSHWA hiyo Mzee Philipo Mangula hakuwa na uwezo wa kutoa hivyo akajiondoa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuhofia Kuangushwa vibaya.
Mhe Gerson Lwenge alikuwa anatoa Rushwa kwa wapiga kura ili NEBCHARD CHARLES MSIGWA achaguliwe katika nafasi hiyo na baadaye Mzee Philipo Mangula aliungana na Gerson Lwenge katika Mtandao huo wa Rushwa ili kumwangusha Yono Kevela ambaye ana ugomvi wa mda mrefu na Mzee Mangula.

Taarifa kutoka kwa Madereva wa magari ya waliowachukua wajumbe wa CCM Wilaya ya Wangng'ombe wajumbe walipata Shs 25,000/= kila Mjumbe Wakiwemo Kwenye magari ya USALULE TRANS na Magari matatu yaliyochukua wajumbe kwa siku ya Uchaguzi.Taarifa zaidi zimebaini kuwa Magari yaliyokithiri kwa ugawaji Rushwa huku Mzee Philipo Mangula akipewa taarifa hizo ni pamoja na

1.Dreva wa Amani : ERASTO MNYONGA (T 377ADA)
2.Dreva wa Sikinde :Fred (T481 BVJ)
3.Dreva Usalule: Bonny Kadege (T329 BED & T573ASL)
Wahusika waliokuwa wanatoa rushwa ndani ya magari hayo walikuwa wanaelekeza yafuatayo:
1. Nafasi ya Mwenyekiti achaguliwe Msigwa (asichaguliwe Hamis Nurdin)
2. Nafasi ya NEC achaguliwe NEBCHARD MSIGWA
3. Nafasi ya uenezi achaguliwe JEOFREY NYAGAWA.
Waliokuwa wanatoa fedha hizo walieleza bayana kuwa zimetoka kwa Mhe Gerson Lwenge (Waziri) na taarifa hizo zipo TAKUKURU na wanaendelea na Uchunguzi.
 
Ahahahahahaha, nilikuwa napita tu,
 
CHICHIDODO. Remember it in the Beautyful Ones Are Not Yet Born by Ayi Kwei Armah. Unachukia uchafu ule lakini unakula vitu vinavyotokana na huo uchafu. Uchaguzi wa CCM umelalamikia mpaka na mweneykiti kuwanrushwa iliyamalaki, which means, wajumbe waliompendekeza Mangula wametokana na rushwa, kwa kuhonga ama kuhongwa, waliompigiankura Mangula, wametokana na rushwa ile ile iliyotamalaki, kwa kuhongwa au kuhonga! Sasa anataka kushughulikia akina nani wakati yeye hakutokea hewani?

Alichukua hatua gani ndani ya chama pale uongozi uliponunuliwa kama mnadani bila kuwepo na tangazonla mauzo, wakati wa uchaguzi wao pale Iringa, akiwania kuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa.

Mangula aseme anawezaje, katika mazingira haya, kuepuka kubatizwa jina la Chichidodo, kama lilivyoelezewa kwa mwanafasihi huyo wa Ghana katika lugha ya picha!

Lakini bado jukumu ambalo limewashinda CCM ni kupambana na kuzuia ufisadi mkubwa serikalini ambao unahusisha rasilimali za umma. Rushwa ndani ya CCM tena wakati wa uchaguzi ni matokeo tu ya tatizo kubwa, hatutaki chama au viongozi wanaotaka tuwaamini kwa sababu tu wanashughulikia matokeo, wakiamini au wakitaka kutuaminisha kuwa hilo ndilo tatizo letu la msingi. No way.
 
Nimesoma Gzt la Raia Mwema la Tarehe 28Nov 2o12 na kushangazwa sana na Kauli ya Mangula kuwa Waziri Gerdon Lwenge ni Mwaadilifu Wakati Taarifa ya Tathimini ya Uchaguzi wa NJOMBE imemtaja kuwa ametoa Rushwa na tarifa zipo TAKUKURU watu wanaendelea kutoa Ushahidi hadi sasa.

Hata hivyo taarifa za TAKUKURU NJOMBE zinaonyesha kuwa Kamanda wa PCCB aitwaye Richard Samila alimukamata Gerson Lwenge katika mazingira ya Rushwa na kuhojiwa kwa masaa kadhaa mnamo tarehe 31/7/2010.
Pia Kamanda huyo wa PCCB alifanikiwa kuwakamata Wafuasi wa Waziri Gerson Lwenge (SAMSON KIWEHELO,BENITO MSOVELA,HENNRY MAWATA) wakiwa na gari T542 AUJ mali ya Waziri Gerson Lwenge.

Wafuasi hao walikamatwa wakiwa na mipira ,nguo,fedha ambapo walikuwa wanagawa kwa wapiga kura ili Waziri Lwenge apite. Picha zinaonyesha wazi katika magazeti ya Mwananchi . Sasa ni kwa Vipi Philipo Mangula aseme kuwa Gerson Lwenge ni muadilifu wakati hata vyombo vya habari vimeandika kuwa alikamatwa na Rushwa?? Mangula anashughulika na Rushwa Ipi ??;

Mangula anasema alimushuhudia YONO KEVELA kwa macho yake akitoa Rushwa lakini hakutoa taarifa PCCB. Lakini pia Mangula huyo huyo ambaye ni muumini wa Nyerere alishindwa kumushuhudia GERSON LWENGE akitoa Rushwa na wala hana taarifa kuwa alikamatwa na rushwa wala hajasoma magazeti ya Mwananchi yaliyo andika habari za Rushwa.
Mimi nimefuatilia habari katika magazeti na hata PCCB hakuna taarifa zinazo onyesha kuwa Nyimbo na Kevela wametoa Rushwa au wamekamatwa na Rushwa!!!

Kama Kweli Mangula anataka kusafisha Wala Rushwa basi ni bora anze na Nyumbani kwake Njombe ambako na yeye ni Mtuhumiwa.
Nyaraka kadha za Malalamiko zinamtaja Mangula katika kashifa.
Mangula ondoa kwanza Kibanzi kwenye jicho lako Kumbuka usafi lazima uanzie nyumbani kwako Njombe na Si Arusha kama unavyo elekezwa na Summaye.

Hiii Ni habari ya mahojiano ya Mangula katika Raia Mwema:

Mwaka 2010, jimboni kwangu kwenyewe, Njombe Magharibi. Kulikuwa na wagombea watatu; Thomas Nyimbo, Kevela (Stanley Kevela ‘Yono') na Mhandisi mmoja(Gerson Lwenge), ambaye alikuwa ni mgeni kabisa katika siasa za chama chetu, lakini Mhandisi Msomi. Nyimbo na Kevela ni wazoefu, na Nyimbo alikuwa anatetea kiti chake.

Wawili hawa (Nyimbo na Kevela) walitumia fedha nyingi kuhonga ili wapate ushindi. Ni jimboni kwangu, nami niliviona kwa macho yangu vitendo vile vya rushwa. Watu wakalalamika, chama kikajiridhisha kwamba kweli wawili hawa wameshinda kwa sababu ya rushwa. Nyimbo ndiye aliyeongoza kwa kupata kura zaidi ya 7,000, akanyang'anywa ushindi.

Baada ya kunyang'anywa ushindi, baadhi ya viongozi wetu walionufaika na fedha zake za rushswa, wakamshawishi aende upande wa pili. Wakasema NEC ya CCM yenye wajumbe wasiofika 2000 imeshindwa kuheshimu uamuzi wa viongozi wake wa ngazi ya jimbo pamoja na wanachama wake wanaofikia 7,000, kwamba hiyo ni kuwadharau viongozi na wanachama, wakamshauri (Nyimbo) agombee kupitia chama kingine.

Chama kikarejesha jina la yule Injinia. Kwa kweli alikuwa hawezi hata kumiliki jukwaa wakati wa kampeni kwa hiyo walichokuwa wakifanya wapiga debe wake, ni wao kumsemea kwa muda mrefu na kisha yeye kupewa muda mfupi tu wa kusalimia wapiga kura. Nilisema jimbo langu haliwezi kuongozwa na mbunge mtoa rushwa ili kupata uongozi. Tulipambana na Nyimbo na hatimaye tukashinda kwa asilimia zaidi ya 70, yeye akaambulia asilimia 26. Kwa hiyo, ninaposema walioingia madarakani kwa njia ya rushwa katika uchaguzi wetu huu wa ndani watanyang'anywa ushindi namaanisha hivyo, hatutanii. Tayari tumepokea malalamiko kibao hapa, tutayachambua, tutawaita wahusika wajieleze, na ikithibitika kweli kwamba ushindi wao ulipatikana kwa sababu ya rushwa, watanyang'anywa.

Raia Mwema: Suala la rushwa umelizungumza kwa mifano. Wasiwasi wangu uko kwenye kumaliza makundi, na hasa makundi ya kwenye mbio za urais 2015. Miongoni mwa wanaotajwa kuongoza makundi hayo, wanadaiwa kuwa na nguvu nyingi ndani ya chama chenu kiasi kwamba endapo mtawagusa tu, basi huo unaweza ukawa ndiyo mwisho wa CCM kushika dola. Tuambie; mtatumia njia gani kuwabaini vinara wa makundi hayo na wapambe wao, na kisha kuchukua hatua dhidi ya watu kama hao wenye nguvu ya fedha na ufuasi mkubwa ndani ya chama chenu?

Mangula: Hakuna mtu yeyote anayeweza kuchukua nguvu ya kikao. Vikao ndivyo vina uwezo usio na kikomo. Chama ni vikao. Kwa hiyo, kama kuna mwanachama yeyote ndani ya CCM au mpambe wake anayejiona ana nguvu kuliko vikao vya chama, huyo anajidanganya. Ilani ya sasa ya CCM, utekelezaji wake unaishia 2015. Utaratibu wa Chama chetu ni kwamba ikifika Mei, 2015, mwanachama yeyote anaweza sasa kuanza kutangaza nia yake ya kugombea urais, ubunge na udiwani. Lakini kuweka nia leo ya kugombea urais, ubunge na udiwani ni kuvuruga utaratibu wa Chama.

Mikakati au mechanism ya kuwabaini vinara wa makundi haya tayari tunayo. Ni kuwafungulia faili hapa ofisini na kuanza kufuatilia nyendo zao na matendo yao watakayoyafanya kuanzia sasa, na endapo mtu huyo (aliyefunguliwa faili na kufuatiliwa) atachukua fomu ya kuomba uongozi, tutamwita ndani ya vikao vyetu vya kuchuja wagombea na kumsomea madhambi yake aliyoyafanya katika harakati zake za kusaka nafasi aliyoomba kabla ya wakati.

Kamati zetu za Maadili na Usalama zitamfuatilia mhusika, na si wale tu walioko kwenye makundi ya kusaka urais, bali hata wanaosaka ubunge na udiwani kabla ya wakati nao tutawafungulia mafaili hapa. Mbunge akilalamika kwetu moja kwa moja, au kupitia vyombo vya habari kwamba kuna mwanachama mwenzake anamfanyia faulo jimboni kwake kipindi hiki cha utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015, tunafungua mafaili mawili, na juu tunaandika jina la Jimbo na wahusika, halafu tunaanza kuwafuatilia nyendo zao.

Haiwezekani mbunge, badala ya kutumia muda wake kutekeleza Ilani ya Chama chetu jimboni kwake, aanze kupoteza muda wake huo kuhangaika na mwanachama mwenzake anayelitaka jimbo husika. Vivyo hivyo kwa urais 2015. Wote hao wanaotajwatajwa kuutaka urais, wanakabiliwa na majukumu ya kutekeleza Ilani ya CCM kwa sasa. Ilani yetu ndio mkataba baina ya chama chetu na wananchi, tusipoitekeleza watatuhukumu kwa kutukataa 2015.

Kwa hiyo, haiwezekani leo, mtu mwenye matamanio ya urais wa 2015, aanze kuhangaika na mbio hizo na kusahau wajibu wake wa msingi wa kutekeleza yale tuliyoahidi 2010, halafu mtu huyo ategemee kushinda. Ili 2015 wananchi waendelee kutuamini watupe tena ridhaa yao, lazima kila kiongozi na kila mwanachama atumie nguvu na uwezo wake wote kutekeleza Ilani yetu.

Msingi wa yote haya ni mmoja tu. Ili tuweze kuandika Ilani ya 2015 hadi 2020 ambayo tutainadi kwa wananchi, lazima kama Chama tufanye kwanza tathimini ya utekelezaji wa Ilani iliyopita, kwa maana ya 2010 hadi 2015 kwa sababu Ilani hiyo ndiyo itakayokuwa hukumu yetu 2015. Kuanzia sasa, lazima vikao vyetu vyote, kuanzia ngazi ya shina, tawi, kata, jimbo, wilaya, mkoa hadi taifa vijielekeze katika kuangalia utekelezaji wa Ilani na ahadi zetu tulizoahidi.

Ilani itakayofuata (2015-2020) ieleze ni wapi tulishindwa kutekeleza ahadi yetu na ni kwa sababu gani. Yale ambayo utekelezaji wake umekwama katikati tuwe na majibu nayo. Kazi hii ya utekelezaji wa Ilani iliyopo sasa ni kazi ya muda mrefu na ni kazi ya kudumu.

Raia Mwema: Una ujumbe gani kwa wanachama na viongozi wenzako. 2015 watarajie ushindi chini ya Sekretarieti yenu mpya hii?

Mangula: Ujumbe wangu ni mmoja tu, si kwa wanachama na viongozi wenzangu tu, bali hata kwa wapinzani wetu na Watanzania kwa ujumla. Jeshi letu (wanachama wa CCM) tunafika milioni sita. Hili ni jeshi kubwa mno ukilinganisha na majeshi ya vyama vingine vinavyoshindana nasi. Kila mmoja katika jeshi hili akitimiza wajibu wake na akafanya kazi zake za kichama kwa umahiri na umakini, mwaka 2015 tutapata ushindi wa kishindo!

Sehemu ya Waraka wa Tathimini ya Uchaguzi wa CCM NJombe 2012 :

TATHIMINI YA UCHAGUZI WA MKOA WA NJOMBE 2012
CHAGUZI ZA WILAYA
Chaguzi za Wilaya ziliingiliwa na Wimbi la rushwa kutoka kwa baadhi ya Viongozi waliopo Madarakani kwa sababu ya kupanga Safu ya Mwaka 2015 wakiwemo wabunge Wafuatao:
Mhe Gerson Lwenge(Waziri) amepanga safu katika jimbo la Magharibi ambalo limo katika Wilaya ya Wanging'ombe kwa Jumuiya zote za Chama Cha Mapinduzi bila kujali aliyepata nafasi ana uwezo katika nafasi hiyo au la kwa kutumia fedha nyingi ikiwemo jumuiya ya wanawake(UWT) wakishirikiana na Mhe. Diwanai wa kata ya Mdandu ANNA UPENDO GOMBELA ambaye ni rafiki yake wa Kimapenzi (nyumba ndogo) wakati pia ni mke wa Mhe CHAMBILE .

Mhe Jofrey Nyagawa ambaye ni diwani ambaye ni diwani wa kata ya Wanging'ombe na pia ni katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Wanging'ombe alihusika kugawa fedha za rushwa kupitia mtandao wa Gerson Lwenge.
Nafasi nyingine iliyogharimu fedha nyingi za rushwa ni ya Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa (NEC) na katika RUSHWA hiyo Mzee Philipo Mangula hakuwa na uwezo wa kutoa hivyo akajiondoa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuhofia Kuangushwa vibaya.
Mhe Gerson Lwenge alikuwa anatoa Rushwa kwa wapiga kura ili NEBCHARD CHARLES MSIGWA achaguliwe katika nafasi hiyo na baadaye Mzee Philipo Mangula aliungana na Gerson Lwenge katika Mtandao huo wa Rushwa ili kumwangusha Yono Kevela ambaye ana ugomvi wa mda mrefu na Mzee Mangula.

Taarifa kutoka kwa Madereva wa magari ya waliowachukua wajumbe wa CCM Wilaya ya Wangng'ombe wajumbe walipata Shs 25,000/= kila Mjumbe Wakiwemo Kwenye magari ya USALULE TRANS na Magari matatu yaliyochukua wajumbe kwa siku ya Uchaguzi.Taarifa zaidi zimebaini kuwa Magari yaliyokithiri kwa ugawaji Rushwa huku Mzee Philipo Mangula akipewa taarifa hizo ni pamoja na

1.Dreva wa Amani : ERASTO MNYONGA (T 377ADA)
2.Dreva wa Sikinde :Fred (T481 BVJ)
3.Dreva Usalule: Bonny Kadege (T329 BED & T573ASL)
Wahusika waliokuwa wanatoa rushwa ndani ya magari hayo walikuwa wanaelekeza yafuatayo:
1. Nafasi ya Mwenyekiti achaguliwe Msigwa (asichaguliwe Hamis Nurdin)
2. Nafasi ya NEC achaguliwe NEBCHARD MSIGWA
3. Nafasi ya uenezi achaguliwe JEOFREY NYAGAWA.
Waliokuwa wanatoa fedha hizo walieleza bayana kuwa zimetoka kwa Mhe Gerson Lwenge (Waziri) na taarifa hizo zipo TAKUKURU na wanaendelea na Uchunguzi.
Mangula na hata kikwete hawawezi kujibu hoja hizi>
Kama kweli wana dhamila ya kupambana na Rushwa basi Mangula anze na rufaa za Jimbo la Njombe ambazo zimeanza kwa kumutuhumu yeye
 
[h=1]Waliopita, waliobebwa kura za maoni CCM[/h]
picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 18 August 2010

Gumzo

HALMASHAURI Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imepitisha wanachama 238 kugombea ubunge wa majimbo Tanzania Bara na Visiwani.

Miongoni mwa waliopitishwa, wapo waliotabiliwa na wale waliobebwa. Baadhi ya waliobebwa, ni Hamisi Kigwangala, aliyepitishwa kuwania ubunge katika jimbo la Nzega mkoani Tabora.

NEC imepitisha jina la Kigwangala baada ya kumuondoa katika kinyang'anyiro hicho, Hussein Bashe aliyeibuka kidedea katika kura za maoni.

Kuondolewa kwake kulitokana na kile Rais Jakaya Kikwete alichoita, "utata wa uraia wake." Kwenye kinyang'anyiro cha kura za maoni, Kigwangala alishika nafasi ya tatu nyuma ya Bashe na Lucas Selelii.

Hivyo basi, aliyestahili kupitishwa kuchukua nafasi ya Bashe, alikuwa Selelii ambaye alishika nafasi ya pili katika kinyang'anyiro cha kura za maoni.

Hadi sasa, hakuna anayejua sababu za NEC kutompitisha Selelii na kumbeba Kigwangala. Kinachofahamika kwa wengi ni kwamba Kigwangala ni mtumishi wa WAMA – taasisi inayoongozwa na mke wa rais, Mama Salma Kikwete.

Wengine wanasema uamuzi wa Kikwete wa kutomrudisha Selelii umelenga kufurahisha maswahiba zake, Rostam Aziz na Edward Lowassa, ambao wamedaiwa kusikika wakiapa kuwa Selelii hatarejea tena bungeni.

Sasa wachunguzi wa masuala ya siasa ndani ya CCM wanasema Kikwete aliona kwamba hatua yeyote ya kumrejesha Selelii, ingepanua ufa kati yake na maswahiba zake hao wawili.

Mbali na Bashe, mwingine ambaye hakutarajiwa kuteuliwa ni Justin Salakana aliyepitishwa kuwania jimbo la Moshi Mjini.
Kwanza, katika kinyang'anyiro cha kura za maoni, Salakana alishika nafasi ya tatu nyuma ya Athuman Ramole na Thomas Ngawaiya.

Pili, Salakana hana ubavu wa kupambana na mbunge wa CHADEMA katika jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo.

Tatu, kumpitisha mtu ambaye si chaguo la wanachama wenzake na ikitiliwa maanani kwamba hana ubavu wa kushindana, ni kudhoofisha chama na kudidimiza demokrasia.

Nne, mwaka 1995 Salakana alikuwa mbunge wa Rombo kupitia CHADEMA, lakini katika uchaguzi uliofuata alishindwa vibaya na mbunge wa sasa, Basil Mramba kutokana na kile kilichodaiwa kuwa "kugeuza ubunge wake kuwa sehemu ya familia yake."

Wachunguzi wa siasa wanasema Salakana kwa Ndesamburo, hata kama waliwahi kuwa chama kimoja, ni sindano na shoka. Wanasema amewekwa ili ashindwe na kupotea kisiasa.

Mwingine ambaye amepitishwa baada ya kumwagwa katika kura za maoni, ni Gerson Lwenge anayewania ubunge jimboni Njombe Magharibi. Alikuwa mtu wa tatu nyuma ya Thomas Nyimbo na Yono Kevela.

Hatua ya NEC ya kumuengua Nyimbo ambaye aliibuka kidedea, tayari imeleta kizaazaa ndani ya chama hicho. Nyimbo na wanachama wenzake kadhaa wa chama hicho, wamejiengua na kujiunga na upinzani ambako akigombea, hasa kupitia CHADEMA, ana uwezekano mkubwa wa kushinda.

Kwa zaidi ya miaka 10 Nyimbo amekuwa akituhumiwa na viongozi wake ngazi ya taifa kwa kudhoofisha chama, tuhuma ambazo zimekanushwa na viongozi wake wa mkoa.

Hata hivyo, hata kama madai ya Nyimbo yamebaki hai, NEC haikuwa na sababu za msingi za kutompitisha Kevela ambaye amekuwa mbunge katika jimbo hilo kwa kipindi kimoja tu. Badala yake imembeba aliyeshika mkia.

Orodha ya waliopitishwa na ambao hawakustahili ni ndefu. Lakini kubwa zaidi hapa ni hili: Kinyang'nyiro hiki, kimethibitisha kwa mara nyingine tena, kwamba rushwa ni dondandugu ndani ya CCM.

Hata ndani ya mkutano wa NEC, madai ya rushwa yaliibuka. Baadhi ya viongozi wa CCM, akiwamo mtendaji mkuu wa chama, Yusuph Makamba walituhumiwa kuvuruga uchaguzi kwa maslahi binafsi.

Tuhuma dhidi ya Makamba zilitolewa na wajumbe wengi akiwamo mwanasiasa machachari, Nape Nnauye. Akiongea kwa lengo la kukinusuru chama chake, Nape alisema Makamba alijipa mamlaka ya kubadilisha taratibu za uchaguzi bila idhini ya NEC.

Alisema jambo hilo linatafsiriwa na wengi kuwa mtendaji wa chama "alihongwa" ili kubeba baadhi ya wagombea. Makamba hakujibu tuhuma hizo.

Hata hivyo, wiki moja kabla ya mkutano wa NEC Makamba alinukuriwa akisema, "Kila mgombea wa ubunge na udiwani ametoa rushwa, isipokuwa walizidiana viwango."

Ukiondoa haya mawili, jingine linaloonekana katika mchakato huu, ni kuwa wagombea wengi waliopitishwa ni wapya.

Kwa mfano, katika mkoa wa Morogoro, kati ya wabunge 10 waliokuwapo katika Bunge lililopita, ni wabunge watatu tu waliorejeshwa kuwania tena ubunge.

Waliorejeshwa ni Celina Kombani (Ulanga Mashariki), Shabiby Ahmed (Gairo) na Mustafa Mkullo (Kilosa).

Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge lililopita, Dk. Lucy Nkya kutoka mkoa wa Morogoro, sasa amepata jimbo. Amepitishwa kuwania ubunge katika jimbo la Morogoro Mashariki.

Wabunge ambao wameshindwa katika kura za maoni na ambao NEC imebariki kutokomea kwao kisiasa, ni Dk. Juma Ngasongwa (Ulanga Magharibi) na Dk. Omari Mzeru (Morogoro Mjini).

Wengine ni Sulemani Sadiq (Mvomero), Clemence Liyamba (Mikumi), Casto Ligalama (Kilombelo), Hamza Mwenegoha (Morogoro Kusini Mashariki) na Sameer Lotto (Morogoro Mashariki).

Wabunge wapya waliopitishwa kuwania nafasi hiyo, ni Aziz Abood (Morogoro Mjini), Lucy Nkya (Morogoro Mashariki), Innocent Kalogeris (Morogoro Kusini),
Amos Makala (Mvomero), Abdulsalaam SAS (Mikumi), Hadji Mponda (Ulanga Magharibi) na Abdul Rajabu Mteketa (Kilombero).

Katika mkoa wa Kagera, kati ya wabunge 10 waliokuwapo katika Bunge lililopita ni wabunge watano tu, waliopitishwa kuwania tena nafasi zao.

Hao ni pamoja na John Magufuli (Chato), Balozi Khamis Kagasheki (Bukoba Mjini), Eustace Katagira (Kyerwa), Gosbert Blandes (Karagwe) na Oscar Mukasa (Biharamulo).

Waliofungiwa nje ni Willison Masilingi (Muleba Kusini), Diodorus Kamala (Nkenge), Nazir Karamagi (Bukoba Vijijini), Ruth Msafiri (Muleba Kaskazini) na Profesa Fetham Banyikwa (Ngara).

Katika majimbo hayo wagombea waliopitishwa ni Assumpter Mshama (Nkenge), Jasson Rwekiza (Bukoba Vijijini), Charles Mwijage (Muleba Kaskazini), Profesa Anna Tibaijuka (Muleba Kusini) na Deogratias Ntukamazina (Ngara).

Mkoani Tabora, kati ya wabunge wanane wa zamani, ni watatu tu waliorejeshwa katika kinyang'nyiro. Hao ni Samwel John Sitta (Urambo Mashariki), Said Nkumba (Sikonge) na Rostam Aziz (Igunga).

Dk. James Msekela (Tabora Kaskazini), Teddy Kasela-Bantu (Bukene), Siraju Kaboyonga (Tabora Mjini), Lucas Selelii (Nzega) na Tatu Ntimizi (Igalula), hawakurejeshwa kutetea nafasi zao.

Wagombea waliopitishwa kuchukua nafasi za wabunge hao wa zamani, ni Ismail Aden Rage (Tabora), Rostam Abdulrasul Aziz (Igunga), Athuman Mfutakamba (Igalula), Sumar Mamlo (Tabora Kaskazini), Seleman Zedi (Bukene) na Hamisi Kigwangala (Nzega).

Profesa Juma Kapuya ambaye alikuwa mbunge wa Urambo Magharibi jimbo lake limehamishiwa mkoa mpya wa Katavi. Jimbo lake linafahamika kama jimbo la Kaliua.

Mkoa mwingine ambao umevunja rekodi ya kupata wagombea wapya ni Iringa. Wabunge wa zamani waliopita katika kinyang'anyiro cha sasa ni watano tu kati ya 11 waliokuwapo katika bunge lililopita.

Waliorejea ni Monica Mbega (Iringa Mjini), Peter Msolla (Kilolo), William Lukuvi (Ismani), Binilith Mahenge (Makete) na Anne Makinda (Njombe Kusini).

Wagombea wapya, ni Wiliam Augustino Mgimwa (Kalenga), Deo Filikunjombe (Ludewa), Hassan Mohamed Mgimwa (Mufindi Kaskazini), Mendrad Lutengano Kigola (Mufindi Kusini), Deo Sanga – Jahpeople – (Njombe Kaskazini) na Gerson Hosea Lwenge (Njombe Magharibi).

Je, hatua hii ina maana gani? Kwanza, inaonyesha kwamba kinyang'anyiro cha uspika kitakuwa kikali baada ya uchaguzi. Hii ni kwa sababu, kila anayetaka nafasi hiyo atalazimika kushawishi wabunge wapya watakaoingia baada ya uchaguzi.

Hata hivyo, iwapo atatokea mgombea mwanamke kujitosa katika kinyang'anyiro hicho, kuna uwezekano mkubwa wa mgombea huyo kushinda, hasa iwapo ataungwa mkono na wanawake wenzake.

Tayari naibu spika wa sasa, Anne Makinda amenukuliwa akiwaambia baadhi ya marafiki zake, kwamba amekataa ofa aliyopewa na kundi la wapinzani wa spika wa sasa Samwel Sitta.

Makinda amenukuliwa akisema alifuatwa ili kuombwa kugombea nafasi hiyo, lakini kutokana na mahusiano yake mazuri na Sitta, amekataa ombi hilo.

Haijulikani kundi hilo litamfuata nani baada ya karata yao hiyo ya kwanza kuchanika. Bali kwa ushindi mkubwa wa upinzani na wingi wa wabunge wapya ambao wanaelewa alichokuwa akifanya Sitta, uwezekano wa spika wa zamani kurudi kwenye nafasi yake bado upo palepale.

Pili, vigogo wanaotaka kujiimarisha kufanikisha malengo yao ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 wanakabiliwa na kibarua kigumu cha kujijenga kwa wabunge wapya.

Tatu, CCM kitakabiliwa na kibarua kigumu mbele ya wananchi, pale wagombea wake watakapokutana na wagombea wa upinzani.

Hii ni kwa sababu, katika orodha ya wagombea waliopitishwa na NEC, wengi watakuwa hawana rasilimali za kutosha, hasa majigambo ya kufanikisha miradi ya maendeleo.

Sita, katika orodha iliyopitishwa, wagombea wengi wana uwezo mdogo wa kuchambua na kuainisha mambo, jambo litakalofanya CCM kupata wakati mgumu wa kuuza wagombea wake. Wanafahamika hata kwa majina.

Saba, kupitishwa kwa wagombea hawa kunaweza kuwa ni anguko jingine kwa Lowassa. Tofauti na mwaka 2005 ambapo wagombea wengi waliopitishwa walitokana na kundi la mtandao, waliopitishwa katika kinyang'anyiro hiki ama hawana upande, au ni vigumu kuwatambulisha na kundi lake.

Jingine ambalo limejitokeza katika mchakato huu, ni kuibuka kwa mbunge wa zamani wa jimbo la Tarime, Kisyeri Chambiri ambaye sasa amepitishwa kuwania ubunge katika jimbo la Babati Mjini.

Haikutarajiwa kwa kiongozi ambaye anadaiwa kuvuruga mkoa wa Mara, hadi kuotesha makundi yaliyosababisha mtafaruku mkubwa wa uongozi, kupitishwa kuwania ubunge katika jimbo hili.

Ni Chambiri huyuhuyu aliyesababisha jimbo la Tarime Mjini kuangukia upinzani. Ni yeye na kaka yake, Enock Chambiri waliokuwa wanatuhumiwa kuhubiri "ukabila na uzawa."

Yawezekana yaliyomkumba Chambiri huko Tarime yakamrudia Babati ambako ni mhamiaji. Bali harakati zake za kurejea bungeni kupitia mbali na nyumbani, zimeonyesha ujanja au ujasiri wa aina yake.
 
Back
Top Bottom