Mangingi na Mangungo (Utumwa wa kisichojulikana)

Annael

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,828
2,000
Mkutano ulifanyika ukihusisha viongozi wa sayari mbili. Waliamua kuanza utafiti wa kujua kama sayari zingine kunauwezekano wa kuishi. Wataalamu wa vinasaba walikuwepo wakielezea namna ya kuweza kutengeneza kiumbe na kuweza kuishi kulingana na mazingira. Wataalamu wa kosimolojia nao walitoa utaalamu wao kuhusu sayari zilizombali na mazingira yake.

Hakika mkutano huo ulikuwa wa kimkakati. Kila mwenye taaluma yake alikuwa huru kuielezea. Wengine waliezea kwa vitendo na wengine walitoa maelezo kwa nadhalia tu. Mabishano ya kiujuzi yalikuwa yakitokea, kila mmoja akivutia kwake.

........ Naendelea...
 

Annael

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,828
2,000
Kiongozi wa sayari ya Nibaru alisimama huku ameshikilia fimbo yake nyeusi kama kawaida yake. Alianza kwa kusema, "ndungu zangu na jamaa zangu kutoka sayari ya Nepto na wenzangu kutoka sayari hii ya Nibaru. Nimesimama mbele yenu kuelezea hatua tulizokubaliana na mwenzagu mheshimiwa Negrond, kwamba utafiti huu lazima ufanyike kwa uwazi kila mmoja wa raia wetu ajue. Tumekubaliana kwamba huu utafiti utachukua miaka elfu tatu ya Nibaru. Kwakuwa Sayari hii ya Nibaru ipo na vyanzo vingi vya uhai itabidi utafiti wote ufanyikie hapa. Nawashukuru kwa kunisikiliza ninamkaribisha mheshimiwa Negrond aendelee na maelezo mengine.

Mheshimiwa Negrond alisimama na kuanza kisema, najua mnafahamu mimi na kaka yangu Denintro tulikabidhiwa sayari hizi mbili kuweza kuzilinda mpaka watakapo rudi kutoka safari walioenda. Wazazi wetu walisafiri kwenda kwenye Galaksi zingine kuhudhulia mkutano wa laki nane wa Stella mbalimbali. Watachukua mda wa miaka laki sita ya Nibaru. Kwa hiyo tunatakiwa kuwa na umoja mpaka watakapo rudi. Wametuachia mamlaka ya kufanya chochote. Ndio maana leo tunatangaza kuanza utafiti wa jambo hili. Asanteni sana na karibuni kwenye sherehe."
 

Annael

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,828
2,000
Sherehe ilipamba moto. Matukio na maonesho ya hapa na pale vilitokea. Wengine walionesha ujuzi wao wa kutengeneza viumbe kwa mda mfupi sana na wengine waliweza kuongea tu na mambo yanatendeka. Huku wengine walikuwa na uwezo wa kukokotoa hesabu ngumu sana kwa mda mfupi sana. Kusema kweli sherehe ilifana maana ilisheheni kila namna ya ujuzi.

Baadae lilifuata onesho la virusi. Onesho hili lilikuwa la kipekee na maalumu kwa siku hiyo. Virusi aina saba walitolewa kisha kifaa cha kuwarutubisha nacho kikaletwa. Virusi waliingizwa kwenye kifaa cha kurutubishia. Baada ya muda kidogo tu walibadilika na kuwa protini. Watu walishangilia na kusema hakika hii ni hatua moja wapo.
Wengine walipiga vigelegele wakisema, twaweza kuunda
Wengine wakisema galaksi yetu inaujuzi kuliko zingine.
Kila mmoja aliongea alivyoona.

Baada ya sherehe kila mmoja alienda nyumbani kwake. Kusema kweli teknolojia ya huko ilikuwa juu sana. Majengo yalikuwa ya kifahari mno. Yalijengwa angani yakielea tu bila kugusa chini. Funguo za nyumba zimeambatanishwa na hisia ya mwenye nyumba. Barabara za angani zilizo pambwa vizuri mno mithili ya dhahabu inayong'aa sana. Hakika teknolojia ilikuwa juu sana.

Tarumbeta lilipigwa kisha jua liliacha kuwaka na watu wote wakaingia kwenye nyumba zao. Mawe yaliyokuwa yakiwaka moto yalionekana kila kona. Huku manyunyu ya mvua ya moto yalianza kutokea.
 

Annael

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,828
2,000
Sauti za ndege zilisikika wakiimba. Upepo ulivuma huku miungurumo ya mashine mbalimbali ilisikika. Hii ilikuwa ni ishara kwamba kumepambazuka. Watu walikuwa wakijiandaa na shughuli zao za kila siku.

Wasomi, wanafunzi na wajuzi wa mambo mbalimbali walikusanyika katika jengo kuu la kisayansi lililopo katika sayari ya Nibaru kwenye mji wa Naksito uliopo katika nchi ya Uraneus. Lengo lilikuwa ni kuanza kwa mradi wa utengenezaji wa viumbe na utafiti wa kujua sayari zipi zingine zenye uwezekano wa viumbe kuishi.

Wataalamu wa kosmolojia walikuwepo, lengo la hawa ni kufundisha jamii kuhusu nishati ya giza. Nishati ya giza ni ujuzi wa kujua vitu vilivyo mbali sana na sayari, vinavyoonekana na visivyoonekana. Jukumu la wataalamu hawa lilikuwa ni kuieleza jamii kinagaubaga kuhusu nishati ya giza.

Walikuwepo wataalumu wa biolojia, fizikia, hisabati, astrolojia, falsafa na kadhalika. Kila mmoja alijipanga kwa sehemu yake kuhakikisha anatoa elimu hiyo kwa umma. Kila mmoja asiyejua jambo moja alitakiwa kujua mambo yote.

Watu wote waliingia kwenye darasa la technolojia. Wataalamu wa teknolojia walianza kufundisha namna ya kutengeneza virusi. Walianza kwa kuelezea kwamba kwenye miili ya watu kuna vinasaba elfu ishirini na tano. Kila kinasaba ni protini iliyotengenezwa kutikana na virusi. Waliendelea kusema kwamba, ni muhimu kuanza kujifunza kutengeneza virusi kwansa halafu hatimaye tunatengeneza protini na mwisho tunatengeneza vinasaba.

Katika kinasaba kimoja kuna mkusanyiko wa virusi wengi. Virusi hao huungana na kutengeneza taarifa ya kuhusu kinasaba hicho kifanye kazi gani. Ili kuweza kusoma taarifa zote ya vinasaba vyote kwenye mwili unatakiwa kujua kusoma genome.

Genome ni mkusanyiko wa taarifa zote za vinasaba. Kwenye mwili zipo taarifa bilioni thelathini. Kwa hiyo kila taarifa imebeba ujumbe fulani. Ni muhimu sana kuzielewa taarifa hizo.
 

IGWE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
9,206
2,000
Hii ingekuwa intelligentsia ingeeleweka saana mkuu...hapa sijui kama watu wataelewa kitu achilia mbali kuvutiwa nayo...ni nzuri sana inakoelekea ingawa ina code nyingi-zinazoeleweka ukitulia kuzisoma.
 

Annael

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,828
2,000
Naomba Mod. Muhamishie uzi huu kwenye Jukwaa la Intelligence.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom