Mangi aamua kupiga kiberiti nyumba yake mara baada ya kubaini mke anasaliti penzi lao

Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
13,084
2,000
Pata
Nyumba ya familia moja huko mtaa wa ugombolwa Kata ya Segerea ikiwa inateketea kwa moto usiku huu mara baada ya Baba wa familia hiyo kuhisi kuwa mke ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mmoja na kuamua kuichoma moto nyumba hiyo sababu ya wivu wa mapenzi.
Nyumba ikiendelea kuteketea kwa moto mkali
Kwa moto huu hakuna kilichoweza kuokolewa mpaka sasa
Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea Wilaya ya Ilala Jijini Dar wakishuhudia nyumba hiyo ikiteketea kwa moto.
Segerea, Dar Es Salaam, Nyumba moja iliyopo Mtaa Ugombolwa Kata ya segerea Jijini Dar imeteketea kwa moto mara baada ya baba wa familia ya nyumba hiyo kuhisi kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

Hali hiyo imetokea usiku huu majira ya Saa tano Kasoro usiku katika Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea, Wilaya ya Ilala Jijini Dar Es Salaam ambapo inasemekana baba wa familia hiyo alichukua uamuzi huo mara baada ya kusikia kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine nje na mara baada ya kutokuelewa kwao ndipo alipochukua uamuzi huo wa kuitia moto nyumba hiyo.

Mmoja wa shuhuda alisikika akisema kuwa "Hawa Wachaga wana matatizo sana Ebu Ona Sasa mwanaume Mzima Anateketeza Nyumba yake aliyoijenga kwa mamilioni ya Shilingi kisa Mkewe anatembea nje ya ndoa Sasa ona watoto wake wataishi wapi?..watu wengine ni wajinga sana Kama mwanamke anatembea nje ya ndoa si umpe talaka tu" alisikika akiongea Shuhuda huyo.

Mpaka Mtandao huu unaondoka eneo la tukio nyumba hiyo ilikuwa bado ikiteketea kwa moto na hakuna dalili zozote zile zilizokuwa zikichukuliwa kwaajili ya kupambana na moto huo huku ikiwa haijafahamika kama wakati nyumba hiyo ikitiwa kiberiti familia ya huyo baba ilikuwepo ndani ya nyumba au laah huku ikikadiriwa kuwa mali zote zilizomo ndani ya nyumba hiyo zimeteketea kwa moto kwani mpaka tunaondoka hakuna kikosi cha zimamoto kilichofik eneo la tukio wala majirani hawakuonyesha dalili zozote zile za kuuzima mot huo.

Mpaka tunaondoka eneo la tukio hakuna taarifa yoyote ile ya majeruhi wala watu kupoteza maisha katika ajali hiyo ya moto.
 
Uledi

Uledi

JF-Expert Member
583
500
Huyu ndugu yangu hakuwa na Bereta, vinginevyo angeleta madhara kama ya kina Munisi
 
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
13,084
2,000
mbaya zaidi hakuna ata jirani aliojisumbua kuzima moto
 
E

emike

JF-Expert Member
346
195
huyu naona hana bastola angekua nayo huyu angefanya kama yule mchaga wa sudan!!!
 
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
13,084
2,000
haaa,hasira gani hizo jamani?naona siku hizi wachaga wanawashinda wa musoma.nyumba yote imeungua,kujenga kazi,kuanza upya hapo shuhuli,labda huyo jamaa awe milionea
pata picha jamaa angekuwa na bastola
 
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
13,084
2,000
Duh! Wachaga vp tena? Just mapenzi tu au kuna mengine?
na hapo jamaa amesikia tu tetesi mke wake anatembea na jamaa mwingine sipati picha angefumania live 6 kwa 6
 
Rejao

Rejao

JF-Expert Member
9,238
1,500
na hapo jamaa amesikia tu tetesi mke wake anatembea na jamaa mwingine sipati picha angefumania live 6 kwa 6
Lakin sababu ya kuchoma nyumba ni hiyo tu ama kuna sababu nyingine? Msishangae hapo nyumba ilipochomwa likaoteshwa jumba la hatari. Chezea wachaga wewe.
 
Mauza uza

Mauza uza

JF-Expert Member
2,110
2,000
​Akina mangi ni majanga kwenye suala la mapenzi...
 
ndetichia

ndetichia

JF-Expert Member
27,664
2,000
mapenzi mapenzi mabaya naona alijua akimfukuza watagawana mali kaona bora yeshee afu amfukuze vizuri..
 
Mahmood

Mahmood

JF-Expert Member
7,840
2,000
Kumbe sisis wehehe tuna afadhali hawa akina mangi ni wapuuzi sana kama una hasira si ujidhuru mwenyewe tu
Kwa nini ajidhuru Mwenyewe?

1) Dawa ya matatizo haya ni kuhakikisha kwanza kwa kushuhudia kitendo hicho cha Zinaa kwa macho yako kisha mpe talaka yake mzinifu huyo.

Hakikisha kwanza kabla ya kutoa talaka kwamba kweli anazini nje ya ndoa (inaweza kuwa shetani tu anakutanganya katika mawazo yako)

Ukihakikisha kwa macho yako kama kweli anazini hapo ndio mpe talaka yake.

2) Kisha owa mwingine mwenye kujiheshimu na mwenye kuheshimu familia yake (wanawake wema wapo wengi tu).
 
ndetichia

ndetichia

JF-Expert Member
27,664
2,000
Lakin sababu ya kuchoma nyumba ni hiyo tu ama kuna sababu nyingine? Msishangae hapo nyumba ilipochomwa likaoteshwa jumba la hatari. Chezea wachaga wewe.
hapo ugumu ni kwenye kugawana tu ila hakuna jingine ndo mana ikaishia kuchomwa moto.
 

Forum statistics


Threads
1,425,226

Messages
35,085,100

Members
538,249
Top Bottom