Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,802
- 11,961
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JF Kenedi Jijini New York Marekani leo Sept 19,2021 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UN unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 Sept 2021.
RAIS Samia Suluhu Hassan yupo New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN).
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ilisema pia kwamba Septemba 23, mwaka huu Rais Samia anatarajiwa kulihutubia Baraza hilo la UN.
Pamoja na mkutano huo, taarifa ilisema kwamba Rais Samia pia atahudhuria mikutano ya kilele ya kujadili masuala ya mabadiliko ya tabianchi, usalama wa chakula na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Aidha, Rais Samia anatarajiwa pia kukutana na wakuu wa nchi nyingine na viongozi wa mashirika ya kimataifa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na nchi hizo pamoja na mashirika hayo.