Maneno yanayonikera siasa za CCM: uchochezi, uchonganishi, kutishia amani na uvunjifu wa amani

mkuu ulianza vizuri sna mwanzo but umemalizia vibaya thread yako, kuikosoa ccm ambacho ni chama kimekulea na mpaka leo hii unaijua JF ni makosa makubwa.

kwani kukulea kitu gani sembese mama au baba waloko na uchungu wa kila aina na mimi wanakosea na kuwakosoa sasa hii ccm ambayo sina hata undugu wala msaada wowote kwangu ntashindwa je kuikosoa!?
 
mkuu ulianza vizuri sna mwanzo but umemalizia vibaya thread yako, kuikosoa ccm ambacho ni chama kimekulea na mpaka leo hii unaijua JF ni makosa makubwa.



"Watanzania wanataka mabadiliko. Wasipoyaona, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM."

Sosi: Mwl Nyerere, Chimwaga 1995 alipompiga chini Mkwer* akapeta Mmachinga.
 
Kwa maana nyingine CCM wanasema "USIPOTUCHAGUA SISI HAKUTAKUWA NA AMANI" meaning CCM wataanzisha vita.

Ndo maana wanakikosi chao cha vijana wa ccm ambao madhara yake tutayaona ktk chaguzi zijazo ambazo ccm wataanguka na kukitumia hiki kikosi kufanya fujo
 
Mimi sitaki nichague mwizi kwa sababu ya kudanganywa eti amani wakati siku hizi wanataka hadi kutoa roho za watoto wetu,Mimi naona ndo wanaohatarisha amani ya watanzania.

Hiki chama kimeoza kimekuwa cha kijasusi!

Ninachomshukuru Mungu karibia kinakufa kabla hakijatimiza dhima yake
 
Mimi sitaki nichague mwizi kwa sababu ya kudanganywa eti amani wakati siku hizi wanataka hadi kutoa roho za watoto wetu,Mimi naona ndo wanaohatarisha amani ya watanzania.

Hiki chama kimeoza kimekuwa cha kijasusi!

Ninachomshukuru Mungu karibia kinakufa kabla hakijatimiza dhima yake ya kusababisha fujo
 
mkuu ulianza vizuri sna mwanzo but umemalizia vibaya thread yako, kuikosoa ccm ambacho ni chama kimekulea na mpaka leo hii unaijua JF ni makosa makubwa.

mpumbu mkubwa wewe CCM nikiduo cha kulelea watoto kipo mkoa gani na umejua mleta mada alilelewa kwenye kituo hicho..hiyo sera ya ccm imekulea, imekusomesha kawaambia wa..e..ge wenzako
 
kweli kabisa kaka mana CCM inakosa uwajibikaji na utekelezaji wa katiba ya chama. CCM imejikita zaidi kwenye kutetea ufisadi na kuwatetea wanajikita ufisadi na si matatizo ya watanzania mana sasa ni ali mpya, nguvu mpya na kasi mpya kwenye kulinda na kutetea mafisadi

Hivi waliishia wapi ule mpango wao wa kubadili katiba lao?
 
AMANI YA TANZANIA NI KWA KILA MWANADAMU


Habari za hivi karibuni, zinaeleza kuwa watanzania wenye ulemavu wa ngozi au albino wananyimwa haki yao ya kufurahia amani katika nchi yangu Tanzania. Watu wasio na utu wamewaua wananchi wenzetu walemavu 71 mpaka sasa. Mbali na hilo, wananchi 28 wameshambuliwa kwa kusudi la kuwadhuru kwa imani za kishenzi na kishetani. Tena naona ni heri kuwaita wauaji na wakatili hawa wa kijinsia ni mashetani kabisa. Matisho dhidi ya usalama wa watanzania wenzetu mkubwa. Maisha ya Albino yapo katika mashaka!

Nawalilia waliouawa na wale waliojeruhiwa, na wanaopata mateso kwa namna yoyote ile. Nimesikia kwamba hivi karibuni kuna albino, mtanzania mwenzangu; aliokotwa mkoani Arusha akiwa amekufa na baadhi ya viungo vyake kuondolewa.


Maswali mengi yapo ndani ya moyo wangu:



  • Ni nani anahusika au wanahusika na maovu haya?
  • Je! Sheria kali inaweza kuondoa mauaji na mateso haya ya ndugu zetu?

  • Ni amani gani uliyonayo katika kumnyima mwanadamu mwenzako haki ya kuishi?
  • Je! Watendayo mambo haya si watu wenye dini na imani zenye kuzuia kuua au kutesa watu?
  • Mwanadamu hajui mali mengi haziwezi kumfanya mtu kuishi milele duniani humu?
  • Ni nani awajibishwe kwa kosa hili la kuwanyima amani jamii ya albino nchini Tanzania?

Inauma jamani!!




Source: Habari, Channel Ten(Tz)=> Wednesday 13, June 2012
 
Nimekuwa nikitafuta Tafsiri Halisi ya neno Amani, lakini sikupata kuona amani katika nchi huashiriwa na nini haswa kati ya hivi vifuatavyo
1. Nchi yenye chakula cha kutosha,
2. Utawala bora,
3. Selikali sikivu
4. Yenye kujali elimu na watoa elimu
5. Yenye kujali Afya na watoa huduma ya Afya
6. Yenye kujali Kazi na wafanyakazi
7. Yenye kujali mapato na watoa mapato
8. Yenye kujali Usalama wa raia na mali Asili ya nchi.(Rasilimali)

Naamini kuwa nchi ikiweza kuvithibiti hicho vitu vyote, Basi ina qualify kuitwa nchi ya amani, ni kadili ya Mtazamo wangu.
Sasa Nchi yetu ina walipa kodi na wanalipa kodi, ila Kodi ile haitumiki vile inavyo takiwa kwa manufaa ya walipa kodi hao, ina vituo vya afya na watoa huduma, lakini Watoa huduma hawa jaliwi wala kupewa vifaa vya kufanyia kazi Mpaka wagome na pengine vitisho na utekwaji nyara kwa wale watakao onekana wanachochea migomo hiyo. Nchi hii ina shule, na Vyuo pia ila watoa elimu wenyewe halapewi haki yao..
Selikali bora iko wapi? Wabunge nao hawako nyuma kula Rushwa, Mawaziri ndo wameiibia Selikali mpaka wamechoka wana tazamwa tu

Hivi kweli kweli Tanzania inaweza Kufananishwa na nchi yenye Amani?
 
Ki ukweli kwa mwenendo wa migomo inayo endelea hapa nchini, kwangu hii ni vita kubwa kuliko ile ya mabomu na mizinga. kama wananchi wanaishi kwa manunguniko na bila kuridhika, sidhani kama kuna amani yeyote. WAZO LANGU! TUKUBALI KUWA TUPO VITANI NA HAKUNA AMANI YA MOYO!
NAWASILISHA!!
 
Nakubali hoja!! Tumeona jinsi serikali inavyotumia mbinu zinazofanana kijeshi za kulaghai watu wake kwa propaganda na taarifa zisizo sahihi! Lakini pamoja na hayo wananchi wameendelea kuwapinga viongozi na hata vyombo vya usalama vimekuwa vikipambana vikali na wananchi wasioviamini. Hivyo, hitimisho langu! kweli tuko vitani kumtokomeza mkoloni mweusi tulio naye majumbani mwetu!!
 
Back
Top Bottom