Maneno yanayonikera siasa za CCM: uchochezi, uchonganishi, kutishia amani na uvunjifu wa amani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maneno yanayonikera siasa za CCM: uchochezi, uchonganishi, kutishia amani na uvunjifu wa amani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Jul 30, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wanasayansi wamefanya utafiti na kugundua kila binadamu anayezaliwa chini ya uso wa dunia yetu hiii ni Mwanasiasa kwa kuzaliwa kwa kuwa asilimia kubwa ya maisha yake yanaimarika na kustawika au kuathirika kwa sababu ya siasa.

  Ndio maana kuna chaguzi ambazo ni haki yake ya msingi ya kuchaguliwa yeye au kumchagua mtu yoyote ambae yeye kwa imani yake anaona anastahiki kumuongoza ili kumuonyesha njia apate ustawi binafis wa maisha yake, familia yake na Taifa lake kwa ujumla.Hivyo Viongozi Serikali na Wanasiasa wa CCM siasa ni sehemu ya maisha ya Watanzania wote Millioni 40.7.

  Kupitia utafiti huo wa Wanasayansi hao hata mimi nae ni Mwanasiasa kwa kiwango changu. Kinachonikera katika siasa za chama cha Mapinduzi ni maneno ambayo viongozi wake wa kisiasa na wale walioko Serikali wanavyopenda kuyatumia sana kiasi kuwa kwa mwelevu yoyote yule maneno hayo yamesemwa sana kiasi kuwa Wananchi wameshagundua nyuma ya pazia ya matumizi ya maneno hayo kwa Viongozi na Wanasiasa hao. Japo kwa upofu wa Viongozi wetu wa Kisiasa na Serikali wanajisau na kuona Wananchi hawalijui hilo na wala hawaoni matendo yao.

  Maneno kama Uchochezi, Uchonganishi, Kutishia Amani, Uvunjifu wa Amani,hizo ni hisia ,Uthibitisho,upotoshaji wa Wananchi,Wivu,Wapinga Maendeleo,fikra potofu, Intelegensia nk.

  Yamekuwa ni maneno ambayo yameifikisha CCM hapo ilipo sasa ya kupoteza imani kwa Wananchi,kwa kuwa yamefikia kuwa yanasemwa na Viongozi wa Kichama na Serikali ambao Watu [Wananchi] huku site [Makongoro] wanawajua kuwa si wenye hadhi ya kuyatamka hayo.

  Wananchi sio kuwa hawajui adui yao ni nani, wasichonacho ni nyenzo na mbinu za kupambana na adui wao huyo.Kwa kuwa wengi wa maadui zao wako ndani ya mfumo hivyo kuwakabili inakuwa kazi ngumu njia iliyopo kwa Wananchi ni kukwangua gamba la juu la Kobe taratibuuu!! Mpaka kufikia kichwa cha Kobe.Kwa wanaojua jinsi ya kutibu virus wa TB ,dawa yake ndio itakayotumiwa na Wananchi kama TIBA ya tatizo lao hivyo nguvu ya umma ndio siraha waliyonayo mkononi.

  Chama cha Mapinduzi kitambue kuwa maneno hayo yanakera [Irritate] sana yanapotumika kwa sasa, yanaongeza ufa dhidi ya chama hicho dhidi ya Umma.Yangesemwa hivyo wakati Nchi na Wananchi wake wako kwenye ustawi yaani maisha BORA hakika kila Mwananchi angesimama kuyaunga mkono kama ambavyo Wananchi walivyounga mkono azimio la Arusha huko nyuma.

  Viongozi wa CCM na Serikali Kwa faida yao waepuke nakuacha kabisa matumizi ya maneno hayo,kwa kuwa ndio yanayoongeza moto, kama ni wimbo basi ni mwimbo wa Mwaka 47. Kama mnabisha endeleeni kuyatumia muuone moto wake.

  Sooooooooooon and very soooonnnnn!!!

  Nawasilisha.
   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Umeanza vizuri sana mwisho ukaharibu kila kitu, sidhani kama tuliwahi kuyasikia hayo kutoka CCM kabla hawajakuwa "triggered".
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Kuna watu bado wamenuna baada ya mtu wao waliyetaka awe rais( na sisitiza sio chama walichotaka kishike dola) kushindwa, hii itaendelea kuwa tesa na mtakuwa mnalalamika kila kukicha. Mtalia na Kibonde, mtalia na Zembwela, mtalia na waislamu, mtalia na polisi lakini ukweli unabakia kuwa mtu wenu hakuwa mtu sahihi kuliongoza taifa hili kwa sasa. BHAAAAASI
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wabunge wa chama cha Mapinduzi wameyazungumza haya Bungeni jana,juzi hao sio CCM.
   
 5. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  kweli blue mkuu umenena tatizo jingine walilonalo ccm ni hao watu wao wanaowatuma mitaa kufanya tathimini na kuwapa taarifa za uongo
  kwa mtu anaye ishi tanzania anajua wazi msimamo wa umama kwa sasa ni CHADEMA,
  Cha kushangaza hawa magamba hawajiulizi kwa nini sio wao au CUF
   
 6. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  CCM wao siku zote utetezi wao umekuwa ni amani, uchochezi, uchonganishi tu. Kumbe wanataka watz waendelee kuwa vipofu tu siku zote? Lakini hata yesu alipoanza kazi walimzushia kila neno mara mchonganish, mchochezi oh anawaambia watu wasilipe kodi, oh mara wanafunzi wako wanapiga kelele nk. Amani inavunjika kutokana na gap kuwa kubwa kati ya walionacho ambao ni wachache (wengi ni wanamagamba) na wasionacho ambao ni wengi na ambao sasa hawataki CCM tena.
   
 7. L

  Luiz JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magamba umeme jamani tusilete siasa za maji taka tatueni matatizo ya wanainchi ili tuondokane na maneno kama uchochezi,uvunjifu wa amani.
   
 8. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nazani waendelee kuona huo wao wanao uona ni uchochezi kupitia makongamano kama hile la leo Katiba ni jibu.Ingwa Mwenyekiti wa tume ya walimu kasahihisha na kusema KATIBA NI JAWABU.

  Waswahili wanasema Jawabu la Kesho huandaa leo.CCM endeleeni kuamini kuwa mambo muhimu kwa umma ni uchochezi
   
 9. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,601
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Kwenye msafara wa mamba na kenge wamo! Mtoa mada amesema anakerwa na maneno wanayotumia viongozi wa CCM, wewe ndugu unasema kuna watu sijui bado wamenuna kutokana na mtu wao sijui kutokuwa rais! Hivi unadhani urais ni nini hasa, fahamu kuwa wewe unaedai kuna watu bado wamenuna ni miongoni mwa watanzania 40mil ambao ni mafukara wa kutupwa waliozungukwa na rasimali za kutosha tena nyingi mno.

  Watanzania tunahitaji uongozi/kiongozi mwenye uchungu na rasimali za nchi hii na zitumike kuwanufaisha watanzania. Na mtu huyo hata awe muislmu au mkristo,mpagani ni sawa tu.

  Naomba kuwasilisha.
   
 10. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  ni kweli kuwa kuwa wapinzani ni wachochezi??
   
 11. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Maisha yako wewe kama yako bora basi haya yanayoendelea ya ukosefu wa umeme haikuhusu,lakini kama unajua umuhiumu wa umeme na barabara,maji na afya kufika sehemu za vijijini,basi huo ndio uchochezi watu wanaona CCM ina kuhukumu nao wale wote wenye kulalamika kutaka kuzifikisha tuhuma hizo za ukosefu wa huduma kwa Watanzania.
   
 12. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Pia jiulize kuwa kwanini vichaa wengi wana vichwa vidogo? Ubongo wao kichwani ni mdogo so hawawezi kufikiri mambo makubwa. Ndo maana kila mtu anaimani yake, na Dr. W. P. Slaa ni rais wa moyoni wa watanzania na sio huyo Vasco da Gama.
   
 13. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Naona ujumbe utaendelea kusambaa kuhusu Mapokeo ya sasa ya Wananchi.Naona ujumbe kutoka kwa Vijana walioudhulia tamasha la Fiesta pale Leaders Club Kinondoni la kumzomea Bushoke kwa kumpongeza Jakaya Kikwete hapo ni ishara kuwa vijana hao ni Wapinzani au ni Wananchi Watanzania?
   
 14. IrDA

  IrDA JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Wadau habari zenu,hili limenikaa kooni kwa muda mrefu sasa ngoja niliteme hapa.....
  Kila siku wanasiasa wetu wanaropoka majukwaani ooo Tanzania inaongoza kwa amani,sijui hivi na hivi..uongo mtupu,infact unatia kichefuchefu.Nadhani wengi mnashangaa kwanini nasema hivi.
  Kwa uchunguzi wangu nimegundua kwamba kilichopo Tanzania si amani,bali ni utulivu utokanao na uoga wa serikali yetu ambayo imejijaza maguvu tele.Amani iliyopo Tanzania naweza kuifananisha na kimya cha watoto pale baba mkorofi aingiapo ndani.Kiukweli watanzania hatuna
  kauli,hatuwezi kujitetea tunanyonya,tunaonewa huku tunaona.
  Hivi ni magazeti mangapi yanafungiwa tukakaa kimya,waandishi wa habari akina Jerry Muro wananyamazishwa kwa hila za viongozi na tukakaa kimya tu.Lengo langu sio kuanzisha machafuko Tanzania kama Libya,Tunisia au Misri kwa sababu kimsingi hayana maana.Lakini lengo langu ni kuwahimiza watanzania kuwa tusiwe watu wa kukaa kimya tu.Tuongee,tuikemee na tuikosoe waziwazi serikali pale inapokosea kwasababu ni haki yetu kikatiba.
  Ni hayo tu
   
 15. m

  mharakati JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ujamaa ulitupumbaza wengi, wachache wajanja wakaanza kutafuna nchi kupitia sera ya ubepari uchwara lakini kwa namna moja au nyingine hii ndiyo anti-thesis ya huu mfumo unyonyaji na amani itabidi ichafuke kidogo kwa mpito wa kudai haki na baada ya hapo amani ya kweli na ya kudumu itapatikana
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Yes kweli hili limekukaa hata ukashindwa kujua kwamba amani hakuna kwa wepesi wake hadi ufanye uchunguzi au utafiti .Pole sana ndiyo Tanzania hii waropokaji wengi .Mwimgine juzi kaitisha kutano na kusema enough is enough .Eti ndilo alilo waitia mh .
   
 17. KIRING'OTI

  KIRING'OTI Member

  #17
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe huna lengo la kuanzisha machafuko lakini wenzako ambao tunapiga counter attack(mlo mmoja kwa siku) tunaelekea huko tunasubiri ushauri mmoja tu kutoka CDM tuingie mtaani.Ama zetu ama zao
   
 18. IrDA

  IrDA JF-Expert Member

  #18
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  eti wadau nini maana ya CDM
   
 19. Poriposha

  Poriposha JF-Expert Member

  #19
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Ulichoandika kina ukweli mwing ila tatizo ukisimama ukaongea ukaonekana upo opp na serikal kaz unayo ndio maana weng tunaishia kuzungumza chinichini
   
 20. Sr. Magdalena

  Sr. Magdalena JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 770
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  Wakuu heshima mbele sana,

  Hivi hii habari ya nchi yetu kuwa ya amani na utulivu inatusaidia nini, au ni propaganda za viongozi wachache, kama nchi yetu ni kisiwa cha amani na utulivu kwa nini na sisi hatufanikiwi kama wenzetu au hata kuwapita, hebu tazama hapa chini, je Tanzania tunasimama wapi na AMANI NA UTULIVU wetu tunaouimba kila kukicha.

  1. EA headquarters Nairobi, Kenya

  EA Portland Cement
  UN Habitat
  Heineken
  Security Group
  UNODC
  Microsoft
  Aljazeera
  HP
  WWF

  2. African Headquarters in Nairobi, Kenya

  UNEP
  Red Cross
  Image Africa
  Nokia Siemens Networks
  Bharti airtel
  Google
  General Electric
  Xinhua News Agency
  China Radio International
  China Centre Television
  Standard Chartered
  Citibank
  IUCN
  Pricewaterhouse

  Etc, Etc,Etc...ziko nyingi hizo ni baadhi tu.
   
Loading...