Maneno yanaumba, malipo ni hapa hapa duniani

Midazolam

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
806
1,337
Niseme tu ukweli kwamba mimi sijawahi kumfanyia mtu ubaya na mara nyingi sana naambiwa nina roho nzuri na najiituma kwenye kazi.

Mimi ni mojawapo wa watu ninayependa kazi yangu ya kuhudumia wagonjwa, na wapo wengi sana nimejitoa hata wale walioonekana wana corona sikuwahi hata siku moja kumnyanyapaa hata moja niliyowasaidia wanajua ndani ya mioyo yao.

Na kwenye kazi yangu sikuwahi kuomba rushwa ili tu nimsaidie mtu hapana naamini wote ni sawa, ukinipa shukrani uwa nachukua ila nakuwa makini na anayenipa hiyo ela, mara nyingi sana macho haidanganyi nikikutazama kwenye jicho nafahamu hiyo ela haiwezi kuniletea shidaa.

Nimejaribu tu kuelezea tu ukweli jinsi nilivyo na kutowahi kumfanyia mtu ubaya.

Sasa kwa nini mimi mtu tena ninayemfahamu ambaye hata kwangu tena magetoni kwangu nilishawahi kumkaribisha kwa nini aniingize mkenge na kuniibia pesa zangu na kushirikiana na mtu wake ambaye kwa akili zangu napata picha ni mke wake.

Nafanya kazi ili nipate ela ila yeye anatumia njia anazojua na kuniibia fedha zangu.

Sasa natambua kuwa Mungu yupo na sijawahi kumfanyia mtu ubaya na hata kuiba pesa ya mtu sijawahi ,

Sitaki kwenda kwa mganga na sitaenda kwa sababu sifungamani katika hayo mambo , naamini Mungu hata niacha kwa kuwa nilipiga magoti na kumlilia Mungu sana kwa nini nifanyiwe hivi wakati mimi sijamfanyia mtu ubaya, kwa nini mimi nifanyiwe hivi na mtu ninayemjua?

Hitimisho , nimetamka maneno mazito sana juu yake naamini hayatapita bure

Na labda tu mpaka pale atakapo kuja kuniombaa msamaha maana nimeanza kuona majibu yake.

Niseme tu usimfanyie mtu ubaya kwa mtu ambaye hajawahi kumfanyia mtu mwingine kitu kibaya.

Maneno yangu yana nguvu sana na nimeanza kuona matokeo yake.
 
Hapa kila mtu anaupeo wake imani zake na taratibu zake,ipo hivi mkuu ili uishi vizuri kwenye hii dunia unatakiwa uwe ni mtu muelewa!.

Yakupasa uelewe tunaishi na watu wa hulka tofauti tofauti,hivyo ulivyo wewe sivyo wengine walivyo. Ukilijua hili utajua na wapi ufanye wema kwa kiasi gani na wapi panahitajika security maana Kuna watu wa hulka tofauti na yako.

Sikushauri au sikutaki umchukulie hatua mbaya aliekukosea la hasha!,sawa wewe umewatendea wema wengine lakini si kigezo Cha wengine wakutendee wewe wema. Kiuhalisia mambo hayapo hivyo,hivyo basi wema wako usizidi mpk kuishinda security yako!.

Huyo Mungu aliwapa akili pia ilikusudi mambo mengine muyamalize kwa hekima ya akili.
Lengo la komenti yangu ni inahitajika uwe muelewa ili ujue uende vipi na Kariba za watu mbalimbali,usisadiki tu wema wako wa leo basi utakuwa majibu kwa watu wote. Pia wema wako usizidi mipaka ya security yako,mkuu jilinde afya yako bado tunahitaji huduma yako.
 
Mkwara wa mbuzi tu huoo,
We akubali tu umeshapigwa na umeshindwa kumfanya lolote aliyekupiga,pambana tu kivingine
 
Pole sana. Hakika kama unayosema ni kweli. Majibu utayaona tu. Mtu aliyekutendea hayo mabaya lazima atapata malipo yake. Nguvu ya aliyetuumba ni ya ajabu.
 
Mkuu jaribu kusamehe ukisamehe basi hutua moyo wako juu chuki na kisasi licha ya makosa mengi tunayo ya tenda mwenyez mungu hutusamehe iweje sisi tushindewe kusamehe mkuu narudia tena samehe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom