Maneno ya sokoine jinamizi ni jinamizi linaloitafuna serikali ya ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maneno ya sokoine jinamizi ni jinamizi linaloitafuna serikali ya ccm

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Apr 27, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mwenyezi Mungu katika uumbaji wake aliumba viumbe mbalimbali miongoni mwao wakiwapo wanyama,ndege wa angani na binadamu.Katika uumbaji wa binadamu alimpa akili za kujua mwema na mabaya na akili ya kuwatawala viumbe vyote viishivyo ndani ya dunia.Kwa mantiki hii tuliumbwa kuwa viongozi kwa viumbe wengine lakini tumetelekeza amri ya Mungu ya kuwa viongozi.

  Nimeanza kwa maneno haya kutokana na watawala wetu kukosa haya na kuamua kutelekeza kwa makusudi maazimio tuliyopewa na Mungu katika kuiongoza dunia hii.Wako wapi viongozi aina ya Sokoine,tuna muenzi vipi ikiwa tunashindwa kutekeleza yale aliyoyaamini bila kumung'unya maneno.Aliwahi kusema "viongozi wazembe na wabadhirifu waanze kuhesabu siku zao.Labda tusiwajue.Hawa,hatuna sababu ya kuwapa imani kuwa tutawalinda katika vitendo vyao vibovu"

  Maneno haya mazito yameachwa kama yatima kwa kuwa tu hakuna anaye thubutu kuyasimamia.Nchi imejaa kubebana, kila mmoja analinda maslahi ya mkubwa wake,na kila anayeachia madaraka anaandaa wa kumrithi kwa ajili ya kuficha madhambi yake.Jinamizi hili la maneno mazito ya Sokoine yanahitajika sana katika kipindi hiki ambacho ufisadi umetamalaki ndani ya nchi yetu.
   
Loading...